2 Samweli 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 1 (Swahili) 2nd Samuel 1 (English)

Ikawa baada ya kufa kwake Sauli, hapo Daudi aliporudi katika kuwaua Waamaleki, naye Daudi amekaa siku mbili katika Siklagi; 2 Samweli 1:1

It happened after the death of Saul, when David was returned from the slaughter of the Amalekites, and David had abode two days in Ziklag;

hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia. 2 Samweli 1:2

it happened on the third day, that behold, a man came out of the camp from Saul, with his clothes torn, and earth on his head: and so it was, when he came to David, that he fell to the earth, and did obeisance.

Daudi akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli. 2 Samweli 1:3

David said to him, From whence come you? He said to him, Out of the camp of Israel am I escaped.

Daudi akamwambia, Yalikwendaje? Tafadhali uniambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa. 2 Samweli 1:4

David said to him, How went the matter? Please tell me. He answered, The people are fled from the battle, and many of the people also are fallen and dead; and Saul and Jonathan his son are dead also.

Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa? 2 Samweli 1:5

David said to the young man who told him, How know you that Saul and Jonathan his son are dead?

Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi. 2 Samweli 1:6

The young man who told him said, As I happened by chance on Mount Gilboa, behold, Saul was leaning on his spear; and, behold, the chariots and the horsemen followed hard after him.

Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa. 2 Samweli 1:7

When he looked behind him, he saw me, and called to me. I answered, Here am I.

Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki. 2 Samweli 1:8

He said to me, Who are you? I answered him, I am an Amalekite.

Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu. 2 Samweli 1:9

He said to me, Stand, I pray you, beside me, and kill me; for anguish has taken hold of me, because my life is yet whole in me.

Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu. 2 Samweli 1:10

So I stood beside him, and killed him, because I was sure that he could not live after that he was fallen: and I took the crown that was on his head, and the bracelet that was on his arm, and have brought them here to my lord.

Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; 2 Samweli 1:11

Then David took hold on his clothes, and tore them; and likewise all the men who were with him:

wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga. 2 Samweli 1:12

and they mourned, and wept, and fasted until even, for Saul, and for Jonathan his son, and for the people of Yahweh, and for the house of Israel; because they were fallen by the sword.

Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki. 2 Samweli 1:13

David said to the young man who told him, Whence are you? He answered, I am the son of a foreigner, an Amalekite.

Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? 2 Samweli 1:14

David said to him, How were you not afraid to put forth your hand to destroy Yahweh's anointed?

Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. 2 Samweli 1:15

David called one of the young men, and said, Go near, and fall on him. He struck him, so that he died.

Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa Bwana. 2 Samweli 1:16

David said to him, Your blood be on your head; for your mouth has testified against you, saying, I have slain Yahweh's anointed.

Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; 2 Samweli 1:17

David lamented with this lamentation over Saul and over Jonathan his son

(kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema, Wana wa Yuda na wafundishwe haya, 2 Samweli 1:18

(and he bade them teach the children of Judah [the song of] the bow: behold, it is written in the book of Jashar):

Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka! 2 Samweli 1:19

Your glory, Israel, is slain on your high places! How are the mighty fallen!

Msiyahubiri mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga. 2 Samweli 1:20

Don't tell it in Gath, Don't publish it in the streets of Ashkelon; Lest the daughters of the Philistines rejoice, Lest the daughters of the uncircumcised triumph.

Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta. 2 Samweli 1:21

You mountains of Gilboa, Let there be no dew nor rain on you, neither fields of offerings: For there the shield of the mighty was vilely cast away, The shield of Saul, not anointed with oil.

Kutoka kwa damu yao waliouawa, Kutoka kwa shahamu yao mashujaa, Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, Wala upanga wa Sauli haukurudi bure. 2 Samweli 1:22

From the blood of the slain, from the fat of the mighty, The bow of Jonathan didn't turn back, The sword of Saul didn't return empty.

Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba. 2 Samweli 1:23

Saul and Jonathan were lovely and pleasant in their lives, In their death they were not divided: They were swifter than eagles, They were stronger than lions.

Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu. 2 Samweli 1:24

You daughters of Israel, weep over Saul, Who clothed you in scarlet delicately, Who put ornaments of gold on your clothing.

Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa Juu ya mahali pako palipoinuka 2 Samweli 1:25

How are the mighty fallen in the midst of the battle! Jonathan is slain on your high places.

Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake. 2 Samweli 1:26

I am distressed for you, my brother Jonathan: Very pleasant have you been to me: Your love to me was wonderful, Passing the love of women.

Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita zilivyoangamia! 2 Samweli 1:27

How are the mighty fallen, The weapons of war perished!