2 Samweli 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 16 (Swahili) 2nd Samuel 16 (English)

Naye Daudi alipokipita punde hicho kilele cha mlima, tazama, Siba, mtumwa wa Mefiboshethi, akamkuta, na punda wawili waliotandikwa, na juu yao mikate mia mbili ya ngano, na vishada mia vya zabibu kavu, na matunda mia ya wakati wa hari, na kiriba cha divai. 2 Samweli 16:1

When David was a little past the top [of the ascent], behold, Ziba the servant of Mephibosheth met him, with a couple of donkeys saddled, and on them two hundred loaves of bread, and one hundred clusters of raisins, and one hundred summer fruits, and a bottle of wine.

Mfalme akamwambia Siba, Ni za nini hizi? Siba akasema, Punda ni za jamaa ya mfalme wazipande; na mkate na matunda ni chakula cha hawa vijana; na divai ni kwamba wanywe hao wazimiao nyikani. 2 Samweli 16:2

The king said to Ziba, What do you mean by these? Ziba said, The donkeys are for the king's household to ride on; and the bread and summer fruit for the young men to eat; and the wine, that such as are faint in the wilderness may drink.

Mfalme akasema, Na mwana wa bwana wako yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Angalia, anakaa Yerusalemu; kwani alisema, Leo nyumba ya Israeli watanirudishia ufalme wa baba yangu. 2 Samweli 16:3

The king said, Where is your master's son? Ziba said to the king, Behold, he abides at Jerusalem; for he said, Today will the house of Israel restore me the kingdom of my father.

Ndipo mfalme akamwambia Siba, Tazama, yote yaliyokuwa ni mali ya Mefiboshethi ni yako. Siba akasema, Mimi nasujudu; na nione kibali machoni pako, Ee bwana wangu, mfalme. 2 Samweli 16:4

Then said the king to Ziba, Behold, all that pertains to Mephibosheth is yours. Ziba said, I do obeisance; let me find favor in your sight, my lord, O king.

Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda. 2 Samweli 16:5

When king David came to Bahurim, behold, a man of the family of the house of Saul came out, whose name was Shimei, the son of Gera. He came out, and cursed still as he came.

Tena akamtupia Daudi mawe, na watumishi wote wa mfalme Daudi; na watu wote na mashujaa wote walikuwako mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto. 2 Samweli 16:6

He cast stones at David, and at all the servants of king David: and all the people and all the mighty men were on his right hand and on his left.

Na Shimei alipolaani, alisema hivi, Nenda zako! Nenda zako! Ewe mtu wa damu! Ewe mtu usiyefaa! 2 Samweli 16:7

Thus said Shimei when he cursed, Be gone, be gone, you man of blood, and base fellow:

Bwana amerudisha juu yako damu yote ya nyumba ya Sauli ambaye umetawala badala yake; naye Bwana ametia ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao; kisha, angalia, wewe umetwaliwa katika uovu wako mwenyewe, kwa sababu umekuwa mtu wa damu. 2 Samweli 16:8

Yahweh has returned on you all the blood of the house of Saul, in whose place you have reigned; and Yahweh has delivered the kingdom into the hand of Absalom your son; and, behold, you are [taken] in your own mischief, because you are a man of blood.

Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake. 2 Samweli 16:9

Then said Abishai the son of Zeruiah to the king, "Why should this dead dog curse my lord the king? Please let me go over and take off his head."

Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu Bwana amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya? 2 Samweli 16:10

The king said, What have I to do with you, you sons of Zeruiah? Because he curses, and because Yahweh has said to him, Curse David; who then shall say, Why have you done so?

Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; si zaidi Mbenyamini huyu sasa? Mwacheni alaani, kwa sababu Bwana ndiye aliyemwagiza. 2 Samweli 16:11

David said to Abishai, and to all his servants, Behold, my son, who came forth from my bowels, seeks my life: how much more [may] this Benjamite now [do it]? let him alone, and let him curse; for Yahweh has invited him.

Labda Bwana atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye Bwana atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo. 2 Samweli 16:12

It may be that Yahweh will look on the wrong done to me, and that Yahweh will requite me good for [his] cursing of me this day.

Basi wakaendelea njiani Daudi na watu wake; Shimei naye akaaendelea juu ya ubavu wa kile kilima, kwa kumkabili, huku akiendelea, akilaani, akimtupia mawe, na kurusha mavumbi. 2 Samweli 16:13

So David and his men went by the way; and Shimei went along on the hill-side over against him, and cursed as he went, and threw stones at him, and cast dust.

Naye mfalme na watu wake wote waliokuwa pamoja naye wakafika, wamechoka sana; naye akajiburudisha huko. 2 Samweli 16:14

The king, and all the people who were with him, came weary; and he refreshed himself there.

Absalomu, na hao watu wote wa Israeli, wakafika Yerusalemu, naye Ahithofeli alikuwa pamoja naye. 2 Samweli 16:15

Absalom, and all the people, the men of Israel, came to Jerusalem, and Ahithophel with him.

Ikawa, Hushai, Mwarki, rafiki wa Daudi, alipomjia Absalomu, Hushai akamwambia Absalomu, Na aishi mfalme, aishi mfalme. 2 Samweli 16:16

It happened, when Hushai the Archite, David's friend, was come to Absalom, that Hushai said to Absalom, [Long] live the king, [Long] live the king.

Naye Absalomu akamwambia Hushai, Je! Huu ndio wema wako kwa rafiki yako? Mbona hukutoka pamoja na rafiki yako? 2 Samweli 16:17

Absalom said to Hushai, Is this your kindness to your friend? Why didn't you go with your friend?

Hushai akamwambia Absalomu, La, sivyo; lakini yule Bwana aliyemchagua, na watu hawa, na watu wote wa Israeli, mimi nitakuwa wake, na pamoja naye nitakaa. 2 Samweli 16:18

Hushai said to Absalom, No; but whom Yahweh, and this people, and all the men of Israel have chosen, his will I be, and with him will I abide.

Na tena, Ni nani ambaye yanipasa nimtumikie? Hainipasi kutumika mbele ya mwanawe? Kama nilivyotumika mbele ya baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mbele yako. 2 Samweli 16:19

Again, whom should I serve? Shouldn't I serve in the presence of his son? as I have served in your father's presence, so will I be in your presence.

Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa shauri lako, tufanyeje. 2 Samweli 16:20

Then said Absalom to Ahithophel, Give your counsel what we shall do.

Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe. 2 Samweli 16:21

Ahithophel said to Absalom, Go in to your father's concubines, that he has left to keep the house; and all Israel will hear that you are abhorred of your father: then will the hands of all who are with you be strong.

Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote. 2 Samweli 16:22

So they spread Absalom a tent on the top of the house; and Absalom went in to his father's concubines in the sight of all Israel.

Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.

2 Samweli 16:23

The counsel of Ahithophel, which he gave in those days, was as if a man inquired at the oracle of God: so was all the counsel of Ahithophel both with David and with Absalom.