Kumbukumbu la Torati 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 8 (Swahili) Deuteronomy 8 (English)

Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki. Kumbukumbu la Torati 8:1

All the commandment which I command you this day shall you observe to do, that you may live, and multiply, and go in and possess the land which Yahweh swore to your fathers.

Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Kumbukumbu la Torati 8:2

You shall remember all the way which Yahweh your God has led you these forty years in the wilderness, that he might humble you, to prove you, to know what was in your heart, whether you would keep his commandments, or not.

Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Kumbukumbu la Torati 8:3

He humbled you, and allowed you to hunger, and fed you with manna, which you didn't know, neither did your fathers know; that he might make you know that man does not live by bread only, but by everything that proceeds out of the mouth of Yahweh does man live.

Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. Kumbukumbu la Torati 8:4

Your clothing didn't grow old on you, neither did your foot swell, these forty years.

Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo. Kumbukumbu la Torati 8:5

You shall consider in your heart that as a man chastens his son, so Yahweh your God chastens you.

Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha. Kumbukumbu la Torati 8:6

You shall keep the commandments of Yahweh your God, to walk in his ways, and to fear him.

Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; Kumbukumbu la Torati 8:7

For Yahweh your God brings you into a good land, a land of brooks of water, of springs and springs, flowing forth in valleys and hills;

nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali; Kumbukumbu la Torati 8:8

a land of wheat and barley, and vines and fig trees and pomegranates; a land of olive trees and honey;

nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba. Kumbukumbu la Torati 8:9

a land in which you shall eat bread without scarceness, you shall not lack anything in it; a land whose stones are iron, and out of whose hills you may dig copper.

Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Kumbukumbu la Torati 8:10

You shall eat and be full, and you shall bless Yahweh your God for the good land which he has given you.

Jihadhari, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. Kumbukumbu la Torati 8:11

Beware lest you forget Yahweh your God, in not keeping his commandments, and his ordinances, and his statutes, which I command you this day:

Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; Kumbukumbu la Torati 8:12

lest, when you have eaten and are full, and have built goodly houses, and lived therein;

na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; Kumbukumbu la Torati 8:13

and when your herds and your flocks multiply, and your silver and your gold is multiplied, and all that you have is multiplied;

basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; Kumbukumbu la Torati 8:14

then your heart be lifted up, and you forget Yahweh your God, who brought you forth out of the land of Egypt, out of the house of bondage;

aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, Kumbukumbu la Torati 8:15

who led you through the great and terrible wilderness, [in which were] fiery serpents and scorpions, and thirsty ground where was no water; who brought you forth water out of the rock of flint;

aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. Kumbukumbu la Torati 8:16

who fed you in the wilderness with manna, which your fathers didn't know; that he might humble you, and that he might prove you, to do you good at your latter end:

Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. Kumbukumbu la Torati 8:17

and [lest] you say in your heart, My power and the might of my hand has gotten me this wealth.

Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. Kumbukumbu la Torati 8:18

But you shall remember Yahweh your God, for it is he who gives you power to get wealth; that he may establish his covenant which he swore to your fathers, as at this day.

Lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka. Kumbukumbu la Torati 8:19

It shall be, if you shall forget Yahweh your God, and walk after other gods, and serve them, and worship them, I testify against you this day that you shall surely perish.

Kama vile mataifa yale ambayo Bwana anawaangamiza mbele yenu, ndivyo mtakavyoangamia; kwa sababu hamkutaka kuisikiliza sauti ya Bwana, Mungu wenu. Kumbukumbu la Torati 8:20

As the nations that Yahweh makes to perish before you, so shall you perish; because you wouldn't listen to the voice of Yahweh your God.