Kumbukumbu la Torati 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 18 (Swahili) Deuteronomy 18 (English)

Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake. Kumbukumbu la Torati 18:1

The priests the Levites, [even] all the tribe of Levi, shall have no portion nor inheritance with Israel: they shall eat the offerings of Yahweh made by fire, and his inheritance.

Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia. Kumbukumbu la Torati 18:2

They shall have no inheritance among their brothers: Yahweh is their inheritance, as he has spoken to them.

Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo. Kumbukumbu la Torati 18:3

This shall be the priests' due from the people, from those who offer a sacrifice, whether it be ox or sheep, that they shall give to the priest the shoulder, and the two cheeks, and the maw.

Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, umpe. Kumbukumbu la Torati 18:4

The first fruits of your grain, of your new wine, and of your oil, and the first of the fleece of your sheep, shall you give him.

Kwani Bwana, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele. Kumbukumbu la Torati 18:5

For Yahweh your God has chosen him out of all your tribes, to stand to minister in the name of Yahweh, him and his sons for ever.

Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua Bwana; Kumbukumbu la Torati 18:6

If a Levite comes from any of your gates out of all Israel, where he lives as a foreigner, and comes with all the desire of his soul to the place which Yahweh shall choose;

na atumike kwa jina la Bwana, Mungu wake, kama wafanyavyo ndugu zake wote, Walawi wasimamao huko mbele za Bwana. Kumbukumbu la Torati 18:7

then he shall minister in the name of Yahweh his God, as all his brothers the Levites do, who stand there before Yahweh.

Wawe na fungu sawasawa la kula, pamoja na haya yaliyomfikilia kwa kuuzwa urithi wa baba zake. Kumbukumbu la Torati 18:8

They shall have like portions to eat, besides that which comes of the sale of his patrimony.

Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. Kumbukumbu la Torati 18:9

When you are come into the land which Yahweh your God gives you, you shall not learn to do after the abominations of those nations.

Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, Kumbukumbu la Torati 18:10

There shall not be found with you anyone who makes his son or his daughter to pass through the fire, one who uses divination, one who practices sorcery, or an enchanter, or a sorcerer,

wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kumbukumbu la Torati 18:11

or a charmer, or a consulter with a familiar spirit, or a wizard, or a necromancer.

Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. Kumbukumbu la Torati 18:12

For whoever does these things is an abomination to Yahweh: and because of these abominations Yahweh your God does drive them out from before you.

Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. Kumbukumbu la Torati 18:13

You shall be perfect with Yahweh your God.

Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo. Kumbukumbu la Torati 18:14

For these nations, that you shall dispossess, listen to those who practice sorcery, and to diviners; but as for you, Yahweh your God has not allowed you so to do.

Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Kumbukumbu la Torati 18:15

Yahweh your God will raise up to you a prophet from the midst of you, of your brothers, like me; to him you shall listen;

Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. Kumbukumbu la Torati 18:16

according to all that you desired of Yahweh your God in Horeb in the day of the assembly, saying, Let me not hear again the voice of Yahweh my God, neither let me see this great fire any more, that I not die.

Bwana akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Kumbukumbu la Torati 18:17

Yahweh said to me, They have well said that which they have spoken.

Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Kumbukumbu la Torati 18:18

I will raise them up a prophet from among their brothers, like you; and I will put my words in his mouth, and he shall speak to them all that I shall command him.

Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Kumbukumbu la Torati 18:19

It shall happen, that whoever will not listen to my words which he shall speak in my name, I will require it of him.

Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. Kumbukumbu la Torati 18:20

But the prophet, who shall speak a word presumptuously in my name, which I have not commanded him to speak, or who shall speak in the name of other gods, that same prophet shall die.

Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? Kumbukumbu la Torati 18:21

If you say in your heart, How shall we know the word which Yahweh has not spoken?

Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope Kumbukumbu la Torati 18:22

when a prophet speaks in the name of Yahweh, if the thing doesn't follow, nor happen, that is the thing which Yahweh has not spoken: the prophet has spoken it presumptuously, you shall not be afraid of him.