Kumbukumbu la Torati 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 9 (Swahili) Deuteronomy 9 (English)

Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni, Kumbukumbu la Torati 9:1

Hear, Israel: you are to pass over the Jordan this day, to go in to dispossess nations greater and mightier than yourself, cities great and fortified up to the sky,

watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki? Kumbukumbu la Torati 9:2

a people great and tall, the sons of the Anakim, whom you know, and of whom you have heard say, Who can stand before the sons of Anak?

Basi jua siku hii ya leo kuwa Bwana, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia Bwana. Kumbukumbu la Torati 9:3

Know therefore this day, that Yahweh your God is he who goes over before you as a devouring fire; he will destroy them, and he will bring them down before you: so shall you drive them out, and make them to perish quickly, as Yahweh has spoken to you.

Usiseme moyoni mwako, Bwana, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia Bwana niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya Bwana awafukuza nje mbele yako. Kumbukumbu la Torati 9:4

Don't speak in your heart, after that Yahweh your God has thrust them out from before you, saying, For my righteousness Yahweh has brought me in to possess this land; whereas for the wickedness of these nations Yahweh does drive them out from before you.

Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo. Kumbukumbu la Torati 9:5

Not for your righteousness, or for the uprightness of your heart, do you go in to possess their land; but for the wickedness of these nations Yahweh your God does drive them out from before you, and that he may establish the word which Yahweh swore to your fathers, to Abraham, to Isaac, and to Jacob.

Basi jua ya kuwa Bwana, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu. Kumbukumbu la Torati 9:6

Know therefore, that Yahweh your God doesn't give you this good land to possess it for your righteousness; for you are a stiff-necked people.

Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana Kumbukumbu la Torati 9:7

Remember, don't forget, how you provoked Yahweh your God to wrath in the wilderness: from the day that you went forth out of the land of Egypt, until you came to this place, you have been rebellious against Yahweh.

Tena mlimkasirisha Bwana katika Horebu, Bwana akakasirika nanyi hata akataka kuwaangamiza. Kumbukumbu la Torati 9:8

Also in Horeb you provoked Yahweh to wrath, and Yahweh was angry with you to destroy you.

Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano Bwana alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji. Kumbukumbu la Torati 9:9

When I was gone up onto the mountain to receive the tables of stone, even the tables of the covenant which Yahweh made with you, then I stayed on the mountain forty days and forty nights; I did neither eat bread nor drink water.

Bwana akanipa zile mbao mbili za mawe zimeandikwa kwa kidole cha Mungu; na juu yake yameandikwa maneno mfano wa yote aliyosema nanyi Bwana mle mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano. Kumbukumbu la Torati 9:10

Yahweh delivered to me the two tables of stone written with the finger of God; and on them [was written] according to all the words, which Yahweh spoke with you on the mountain out of the midst of the fire in the day of the assembly.

Ikawa mwisho wa siku arobaini usiku na mchana, Bwana alinipa zile mbao mbili za mawe, nazo ni mbao za agano. Kumbukumbu la Torati 9:11

It came to pass at the end of forty days and forty nights, that Yahweh gave me the two tables of stone, even the tables of the covenant.

Bwana akaniambia, Ondoka huko, shuka upesi; kwa kuwa watu wako uliowatoa Misri wamejiharibu; wamekengeuka mara katika njia niliyowaamuru; wamejifanyia sanamu ya kusubu. Kumbukumbu la Torati 9:12

Yahweh said to me, Arise, get you down quickly from hence; for your people whom you have brought forth out of Egypt have corrupted themselves; they have quickly turned aside out of the way which I commanded them; they have made them a molten image.

Tena Bwana akasema nami zaidi, akaniambia, Nimeliona taifa hili; na tazama, ni taifa lenye shingo ngumu; Kumbukumbu la Torati 9:13

Furthermore Yahweh spoke to me, saying, I have seen this people, and, behold, it is a stiff-necked people:

niache, nipate kuwaangamiza, na kulifuta jina lao chini ya mbingu; nami nitakufanya wewe uwe taifa kubwa lenye nguvu kuwapita wao. Kumbukumbu la Torati 9:14

let me alone, that I may destroy them, and blot out their name from under the sky; and I will make of you a nation mightier and greater than they.

Basi nikageuka nikashuka mle mlimani, mlima ukawaka moto; na zile mbao mbili za agano zilikuwa katika mikono yangu miwili. Kumbukumbu la Torati 9:15

So I turned and came down from the mountain, and the mountain was burning with fire: and the two tables of the covenant were in my two hands.

Nikaangalia, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wenu; mmefanya ndama ya ng'ombe ya kusubu; mmekengeuka upesi katika njia aliyowaamuru Bwana. Kumbukumbu la Torati 9:16

I looked, and, behold, you had sinned against Yahweh your God; you had made you a molten calf: you had turned aside quickly out of the way which Yahweh had commanded you.

Nikazishika zile mbao mbili, nikazitupa kutoka katika mikono yangu miwili, nikazivunja mbele ya macho yenu. Kumbukumbu la Torati 9:17

I took hold of the two tables, and cast them out of my two hands, and broke them before your eyes.

Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kwa kumkasirisha. Kumbukumbu la Torati 9:18

I fell down before Yahweh, as at the first, forty days and forty nights; I did neither eat bread nor drink water; because of all your sin which you sinned, in doing that which was evil in the sight of Yahweh, to provoke him to anger.

Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia Bwana kutaka kuwaangamiza. Lakini Bwana alinisikiza wakati huo nao. Kumbukumbu la Torati 9:19

For I was afraid of the anger and hot displeasure, with which Yahweh was angry against you to destroy you. But Yahweh listened to me that time also.

Bwana akamkasirikia sana Haruni akataka kumwangamiza; nikamwombea Haruni naye wakati huo. Kumbukumbu la Torati 9:20

Yahweh was very angry with Aaron to destroy him: and I prayed for Aaron also at the same time.

Kisha nikaitwaa ile dhambi yenu, huyo ndama mliyemfanya, nikamteketeza kwa moto, nikamponda, nikamsaga tikitiki, hata akawa laini kama vumbi; nikalitupa vumbi lake katika kijito kilichoshuka kutoka mlimani. Kumbukumbu la Torati 9:21

I took your sin, the calf which you had made, and burnt it with fire, and stamped it, grinding it very small, until it was as fine as dust: and I cast the dust of it into the brook that descended out of the mountain.

Tena huko Tabera, na Masa, na Kibroth-hataava mlimtia Bwana hasira. Kumbukumbu la Torati 9:22

At Taberah, and at Massah, and at Kibroth-hattaavah, you provoked Yahweh to wrath.

Na wakati alipowatuma Bwana kutoka Kadesh-barnea, akiwaambia, Kweeni mkaimiliki nchi niliyowapa; ndipo mkaasi juu ya maagizo ya Bwana, Mungu wenu, hamkumsadiki wala hamkusikiza sauti yake. Kumbukumbu la Torati 9:23

When Yahweh sent you from Kadesh-barnea, saying, Go up and possess the land which I have given you; then you rebelled against the commandment of Yahweh your God, and you didn't believe him, nor listen to his voice.

Mmekuwa na uasi juu ya Bwana tokea siku nilipowajua ninyi. Kumbukumbu la Torati 9:24

You have been rebellious against Yahweh from the day that I knew you.

Ndipo nikaanguka nchi mbele za Bwana siku zile arobaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka nchi; kwa kuwa Bwana alisema atawaangamiza. Kumbukumbu la Torati 9:25

So I fell down before Yahweh the forty days and forty nights that I fell down, because Yahweh had said he would destroy you.

Nikamwomba Bwana, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu. Kumbukumbu la Torati 9:26

I prayed to Yahweh, and said, Lord Yahweh, don't destroy your people and your inheritance, that you have redeemed through your greatness, that you have brought forth out of Egypt with a mighty hand.

Wakumbuke watumwa wako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie upotofu wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao; Kumbukumbu la Torati 9:27

Remember your servants, Abraham, Isaac, and Jacob; don't look to the stubbornness of this people, nor to their wickedness, nor to their sin,

isije nchi uliyotutoa ikasema, Ni kwa sababu Bwana hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowapa ahadi, tena ni kwa kuwa aliwachukia, alivyowatoa nje ili kuwaua jangwani. Kumbukumbu la Torati 9:28

lest the land whence you brought us out say, Because Yahweh was not able to bring them into the land which he promised to them, and because he hated them, he has brought them out to kill them in the wilderness.

Nao ni watu wako, urithi wako, uliowatoa kwa nguvu zako kuu na mkono wako ulionyoka. Kumbukumbu la Torati 9:29

Yet they are your people and your inheritance, which you brought out by your great power and by your outstretched arm.