Kumbukumbu la Torati 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 4 (Swahili) Deuteronomy 4 (English)

Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu niwafundishazo, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wa baba zenu. Kumbukumbu la Torati 4:1

Now, Israel, listen to the statutes and to the ordinances, which I teach you, to do them; that you may live, and go in and possess the land which Yahweh, the God of your fathers, gives you.

Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo. Kumbukumbu la Torati 4:2

You shall not add to the word which I command you, neither shall you diminish from it, that you may keep the commandments of Yahweh your God which I command you.

Macho yenu yameona aliyoyatenda Bwana kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, Bwana, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako. Kumbukumbu la Torati 4:3

Your eyes have seen what Yahweh did because of Baal Peor; for all the men who followed Baal Peor, Yahweh your God has destroyed them from the midst of you.

Bali ninyi mlioambatana na Bwana, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo. Kumbukumbu la Torati 4:4

But you who did cleave to Yahweh your God are alive everyone of you this day.

Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama Bwana, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki. Kumbukumbu la Torati 4:5

Behold, I have taught you statutes and ordinances, even as Yahweh my God commanded me, that you should do so in the midst of the land where you go in to possess it.

Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. Kumbukumbu la Torati 4:6

Keep therefore and do them; for this is your wisdom and your understanding in the sight of the peoples, who shall hear all these statutes, and say, Surely this great nation is a wise and understanding people.

Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? Kumbukumbu la Torati 4:7

For what great nation is there, that has a god so near to them, as Yahweh our God is whenever we call on him?

Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo. Kumbukumbu la Torati 4:8

What great nation is there, that has statutes and ordinances so righteous as all this law, which I set before you this day?

Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako; Kumbukumbu la Torati 4:9

Only take heed to yourself, and keep your soul diligently, lest you forget the things which your eyes saw, and lest they depart from your heart all the days of your life; but make them known to your children and your children's children;

siku ile uliyosimama mbele za Bwana wako huko Horebu, Bwana aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawasikizisha maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao. Kumbukumbu la Torati 4:10

the day that you stood before Yahweh your God in Horeb, when Yahweh said to me, Assemble me the people, and I will make them hear my words, that they may learn to fear me all the days that they live on the earth, and that they may teach their children.

Mkakaribia, mkasimama chini ya ule mlima; mlima ukawaka moto mpaka kati ya mbinguni, kwa giza na mawingu, na giza kuu. Kumbukumbu la Torati 4:11

You came near and stood under the mountain; and the mountain burned with fire to the heart of the sky, with darkness, cloud, and thick darkness.

Bwana akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu. Kumbukumbu la Torati 4:12

Yahweh spoke to you out of the midst of the fire: you heard the voice of words, but you saw no form; only [you heard] a voice.

Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe. Kumbukumbu la Torati 4:13

He declared to you his covenant, which he commanded you to perform, even the ten commandments; and he wrote them on two tables of stone.

Bwana akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki. Kumbukumbu la Torati 4:14

Yahweh commanded me at that time to teach you statutes and ordinances, that you might do them in the land where you go over to possess it.

Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto; Kumbukumbu la Torati 4:15

Take therefore good heed to yourselves; for you saw no manner of form on the day that Yahweh spoke to you in Horeb out of the midst of the fire.

msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke, Kumbukumbu la Torati 4:16

Lest you corrupt yourselves, and make yourself an engraved image in the form of any figure, the likeness of male or female,

mfano wa mnyama ye yote aliye duniani, au mfano wa ndege ye yote arukaye mbinguni, Kumbukumbu la Torati 4:17

the likeness of any animal that is on the earth, the likeness of any winged bird that flies in the sky,

au mfano wa kitu cho chote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki ye yote aliye majini chini ya nchi; Kumbukumbu la Torati 4:18

the likeness of anything that creeps on the ground, the likeness of any fish that is in the water under the earth;

tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. Kumbukumbu la Torati 4:19

and lest you lift up your eyes to the sky, and when you see the sun and the moon and the stars, even all the host of the sky, you are drawn away and worship them, and serve them, which Yahweh your God has allotted to all the peoples under the whole sky.

Bali Bwana amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi. Kumbukumbu la Torati 4:20

But Yahweh has taken you, and brought you forth out of the iron furnace, out of Egypt, to be to him a people of inheritance, as at this day.

Tena Bwana alinikasirikia kwa ajili yenu, akaapa ya kwamba sitavuka Yordani, na ya kwamba sitaingia nchi ile njema, awapayo Bwana, Mungu wenu, iwe urithi. Kumbukumbu la Torati 4:21

Furthermore Yahweh was angry with me for your sakes, and swore that I should not go over the Jordan, and that I should not go in to that good land, which Yahweh your God gives you for an inheritance:

Lakini mimi nitakufa katika nchi hii, sina ruhusa kuvuka Yordani; bali ninyi mtavuka, na kuimiliki nchi ile njema. Kumbukumbu la Torati 4:22

but I must die in this land, I must not go over the Jordan; but you shall go over, and possess that good land.

Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la Bwana, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na Bwana, Mungu wenu, Kumbukumbu la Torati 4:23

Take heed to yourselves, lest you forget the covenant of Yahweh your God, which he made with you, and make you an engraved image in the form of anything which Yahweh your God has forbidden you.

kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu. Kumbukumbu la Torati 4:24

For Yahweh your God is a devouring fire, a jealous God.

Utakapozaa wana, na wana wa wana, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu cho chote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, na kumtia hasira; Kumbukumbu la Torati 4:25

When you shall father children, and children's children, and you shall have been long in the land, and shall corrupt yourselves, and make an engraved image in the form of anything, and shall do that which is evil in the sight of Yahweh your God, to provoke him to anger;

nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa. Kumbukumbu la Torati 4:26

I call heaven and earth to witness against you this day, that you shall soon utterly perish from off the land whereunto you go over the Jordan to possess it; you shall not prolong your days on it, but shall utterly be destroyed.

Na Bwana atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu kidogo hesabu yenu kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na Bwana. Kumbukumbu la Torati 4:27

Yahweh will scatter you among the peoples, and you shall be left few in number among the nations, where Yahweh shall lead you away.

Na huko mtatumikia miungu, kazi za mikono ya watu, miti na mawe, ambao hawaoni, wala hawasikii, hawali, wala hawanusi. Kumbukumbu la Torati 4:28

There you shall serve gods, the work of men's hands, wood and stone, which neither see, nor hear, nor eat, nor smell.

Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote. Kumbukumbu la Torati 4:29

But from there you shall seek Yahweh your God, and you shall find him, when you search after him with all your heart and with all your soul.

Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia Bwana, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake; Kumbukumbu la Torati 4:30

When you are in oppression, and all these things are come on you, in the latter days you shall return to Yahweh your God, and listen to his voice:

kwa kuwa Bwana, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakukosa wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia. Kumbukumbu la Torati 4:31

for Yahweh your God is a merciful God; he will not fail you, neither destroy you, nor forget the covenant of your fathers which he swore to them.

Maana uliza sasa siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na toka pembe hii ya mbingu hata pembe hii, kwamba kumetukia neno lo lote kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili? Kumbukumbu la Torati 4:32

For ask now of the days that are past, which were before you, since the day that God created man on the earth, and from the one end of the sky to the other, whether there has been [any such thing] as this great thing is, or has been heard like it?

Je! Watu wakati wo wote wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, wasife? Kumbukumbu la Torati 4:33

Did ever a people hear the voice of God speaking out of the midst of the fire, as you have heard, and live?

Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? Kumbukumbu la Torati 4:34

Or has God tried to go and take him a nation from the midst of [another] nation, by trials, by signs, and by wonders, and by war, and by a mighty hand, and by an outstretched arm, and by great terrors, according to all that Yahweh your God did for you in Egypt before your eyes?

Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. Kumbukumbu la Torati 4:35

To you it was shown, that you might know that Yahweh he is God; there is none else besides him.

Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto. Kumbukumbu la Torati 4:36

Out of heaven he made you to hear his voice, that he might instruct you: and on earth he made you to see his great fire; and you heard his words out of the midst of the fire.

Na kwa sababu aliwapenda baba zenu, kwa sababu hiyo aliwachagua wazao wao baada yao, akakutoa katika Misri kwa kuwako pamoja nawe, kwa uweza wake mwingi, Kumbukumbu la Torati 4:37

Because he loved your fathers, therefore he chose their seed after them, and brought you out with his presence, with his great power, out of Egypt;

ili kufukuza mbele yako mataifa, walio wakubwa, wenye nguvu kukupita wewe, ili kukuingiza, na kukupa nchi yao iwe urithi, kama ilivyo leo. Kumbukumbu la Torati 4:38

to drive out nations from before you greater and mightier than you, to bring you in, to give you their land for an inheritance, as at this day.

Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. Kumbukumbu la Torati 4:39

Know therefore this day, and lay it to your heart, that Yahweh he is God in heaven above and on the earth beneath; there is none else.

Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele. Kumbukumbu la Torati 4:40

You shall keep his statutes, and his commandments, which I command you this day, that it may go well with you, and with your children after you, and that you may prolong your days in the land, which Yahweh your God gives you, forever.

Ndipo Musa akabagua miji mitatu ng'ambo ya Yordani upande wa matokeo ya jua; Kumbukumbu la Torati 4:41

Then Moses set apart three cities beyond the Jordan toward the sunrise;

ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo; Kumbukumbu la Torati 4:42

that the manslayer might flee there, who kills his neighbor unawares, and didn't hate him in time past; and that fleeing to one of these cities he might live:

nayo ni hii, Beseri ya barani iliyo katika nchi tambarare, kwa Wareubeni; na Ramothi iliyo Gileadi, kwa Wagadi; na Golani iliyo Bashani, kwa Wamanase. Kumbukumbu la Torati 4:43

[namely], Bezer in the wilderness, in the plain country, for the Reubenites; and Ramoth in Gilead, for the Gadites; and Golan in Bashan, for the Manassites.

Na torati Musa aliyowawekea wana wa Israeli ni hii; Kumbukumbu la Torati 4:44

This is the law which Moses set before the children of Israel:

haya ndiyo mashuhudizo, na amri, na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri; Kumbukumbu la Torati 4:45

these are the testimonies, and the statutes, and the ordinances, which Moses spoke to the children of Israel, when they came forth out of Egypt,

ng'ambo ya Yordani, katika bonde lililoelekea Beth-peori, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni ndiye aliyepigwa na Musa na wana wa Israeli, walipotoka Misri; Kumbukumbu la Torati 4:46

beyond the Jordan, in the valley over against Beth Peor, in the land of Sihon king of the Amorites, who lived at Heshbon, whom Moses and the children of Israel struck, when they came forth out of Egypt.

wakaishika nchi yake, ikawa milki yao, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, ndio wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa ng'ambo ya Yordani upande wa matokeo ya jua; Kumbukumbu la Torati 4:47

They took his land in possession, and the land of Og king of Bashan, the two kings of the Amorites, who were beyond the Jordan toward the sunrise;

toka Aroeri, iliyo juu ya ukingoni pa bonde la Arnoni, hata mpaka mlima wa Sioni (nao ndio Hermoni), Kumbukumbu la Torati 4:48

from Aroer, which is on the edge of the valley of the Arnon, even to Mount Sion (the same is Hermon),

na Araba yote iliyo ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, hata mpaka bahari ya Araba, chini ya matelemko ya Pisga.

Kumbukumbu la Torati 4:49

and all the Arabah beyond the Jordan eastward, even to the sea of the Arabah, under the slopes of Pisgah.