Kumbukumbu la Torati 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 26 (Swahili) Deuteronomy 26 (English)

Kumbukumbu la Torati 26:1

It shall be, when you are come in to the land which Yahweh your God gives you for an inheritance, and possess it, and dwell therein,

twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko. Kumbukumbu la Torati 26:2

that you shall take of the first of all the fruit of the ground, which you shall bring in from your land that Yahweh your God gives you; and you shall put it in a basket, and shall go to the place which Yahweh your God shall choose, to cause his name to dwell there.

Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa Bwana, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi Bwana aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa. Kumbukumbu la Torati 26:3

You shall come to the priest who shall be in those days, and tell him, I profess this day to Yahweh your God, that I am come to the land which Yahweh swore to our fathers to give us.

Naye kuhani atakipokea kikapu mkononi mwako, akiweke chini mbele ya madhabahu ya Bwana, Mungu wako. Kumbukumbu la Torati 26:4

The priest shall take the basket out of your hand, and set it down before the altar of Yahweh your God.

Nawe ujibu, ukaseme mbele za Bwana, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi. Kumbukumbu la Torati 26:5

You shall answer and say before Yahweh your God, A Syrian ready to perish was my father; and he went down into Egypt, and sojourned there, few in number; and he became there a nation, great, mighty, and populous.

Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito. Kumbukumbu la Torati 26:6

The Egyptians dealt ill with us, and afflicted us, and laid on us hard bondage:

Tukamlilia Bwana, Mungu wa baba zetu; Bwana akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu. Kumbukumbu la Torati 26:7

and we cried to Yahweh, the God of our fathers, and Yahweh heard our voice, and saw our affliction, and our toil, and our oppression;

Bwana akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu; Kumbukumbu la Torati 26:8

and Yahweh brought us forth out of Egypt with a mighty hand, and with an outstretched arm, and with great terror, and with signs, and with wonders;

naye ametuingiza mahali hapa, na kutupa nchi hii, nchi ijaayo maziwa na asali. Kumbukumbu la Torati 26:9

and he has brought us into this place, and has given us this land, a land flowing with milk and honey.

Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee Bwana. Kisha ukiweke chini mbele za Bwana, Mungu wako, ukasujudu mbele za Bwana, Mungu wako; Kumbukumbu la Torati 26:10

Now, behold, I have brought the first of the fruit of the ground, which you, Yahweh, have given me. You shall set it down before Yahweh your God, and worship before Yahweh your God:

ukayafurahie mema yote ambayo Bwana, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako. Kumbukumbu la Torati 26:11

and you shall rejoice in all the good which Yahweh your God has given to you, and to your house, you, and the Levite, and the foreigner who is in the midst of you.

Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba; Kumbukumbu la Torati 26:12

When you have made an end of tithing all the tithe of your increase in the third year, which is the year of tithing, then you shall give it to the Levite, to the foreigner, to the fatherless, and to the widow, that they may eat within your gates, and be filled.

nawe sema mbele ya Bwana, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yo yote, wala sikuyasahau; Kumbukumbu la Torati 26:13

You shall say before Yahweh your God, I have put away the holy things out of my house, and also have given them to the Levite, and to the foreigner, to the fatherless, and to the widow, according to all your commandment which you have commanded me: I have not transgressed any of your commandments, neither have I forgotten them:

katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya Bwana, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru. Kumbukumbu la Torati 26:14

I have not eaten of it in my mourning, neither have I put away of it, being unclean, nor given of it for the dead: I have listened to the voice of Yahweh my God; I have done according to all that you have commanded me.

Uangalie kutoka makazi yako matakatifu mbinguni, uwabarikie watu wako Israeli, na nchi uliyotupa kama ulivyowaapia baba zetu, nchi imiminikayo maziwa na asali. Kumbukumbu la Torati 26:15

Look down from your holy habitation, from heaven, and bless your people Israel, and the ground which you have given us, as you swore to our fathers, a land flowing with milk and honey.

Leo hivi akuamuru Bwana, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na hukumu; basi uzishike na kuzifanya kwa moyo wako wote na roho yako yote. Kumbukumbu la Torati 26:16

This day Yahweh your God commands you to do these statutes and ordinances: you shall therefore keep and do them with all your heart, and with all your soul.

Umemwungama Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake; Kumbukumbu la Torati 26:17

You have declared Yahweh this day to be your God, and that you would walk in his ways, and keep his statutes, and his commandments, and his ordinances, and listen to his voice:

naye Bwana amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; Kumbukumbu la Torati 26:18

and Yahweh has declared you this day to be a people for his own possession, as he has promised you, and that you should keep all his commandments;

na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, kama alivyosema. Kumbukumbu la Torati 26:19

and to make you high above all nations that he has made, in praise, and in name, and in honor; and that you may be a holy people to Yahweh your God, as he has spoken.