Kumbukumbu la Torati 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 21 (Swahili) Deuteronomy 21 (English)

Aonekanapo mtu ameuawa katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, kuimiliki, amelala kondeni, wala haijulikani ni nani aliyempiga; Kumbukumbu la Torati 21:1

If one be found slain in the land which Yahweh your God gives you to possess it, lying in the field, and it isn't known who has struck him;

na watoke nje wazee wako na waamuzi wako, nao wapime hapo mpaka miji iliyomzunguka huyo aliyeuawa; Kumbukumbu la Torati 21:2

then your elders and your judges shall come forth, and they shall measure to the cities which are round about him who is slain:

na iwe, mji ulio karibu na yule aliyeuawa, wale wazee wake mji huo watwae mtamba katika kundi la ng'ombe, ambaye hajafanya kazi, wala hajakokota jembe la nira; Kumbukumbu la Torati 21:3

and it shall be, that the city which is nearest to the slain man, even the elders of that city shall take a heifer of the herd, which hasn't been worked with, and which has not drawn in the yoke;

wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo yake humo bondeni; Kumbukumbu la Torati 21:4

and the elders of that city shall bring down the heifer to a valley with running water, which is neither plowed nor sown, and shall break the heifer's neck there in the valley.

nao makuhani wana wa Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua Bwana, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la Bwana na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao; Kumbukumbu la Torati 21:5

The priests the sons of Levi shall come near; for them Yahweh your God has chosen to minister to him, and to bless in the name of Yahweh; and according to their word shall every controversy and every stroke be.

na wazee wote wa mji ule, ulio karibu sana na yule aliyeuawa, na waoshe mikono yao juu ya huyo mtamba aliyevunjwa shingo yake humo bondeni; Kumbukumbu la Torati 21:6

All the elders of that city, who are nearest to the slain man, shall wash their hands over the heifer whose neck was broken in the valley;

na wajibizane kwamba, Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuiona. Kumbukumbu la Torati 21:7

and they shall answer and say, Our hands have not shed this blood, neither have our eyes seen it.

Ee Bwana, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao. Kumbukumbu la Torati 21:8

Forgive, Yahweh, your people Israel, whom you have redeemed, and don't allow innocent blood [to remain] in the midst of your people Israel. The blood shall be forgiven them.

Ndivyo utakavyoondoa damu ya asiye makosa katikati yako, utakapofanya yaliyo sawa machoni pa Bwana. Kumbukumbu la Torati 21:9

So shall you put away the innocent blood from the midst of you, when you shall do that which is right in the eyes of Yahweh.

Utakapokwenda vitani kupigana juu ya adui zako, na Bwana, Mungu wako, awatiapo mikononi mwako, nawe uwachukuapo mateka, Kumbukumbu la Torati 21:10

When you go forth to battle against your enemies, and Yahweh your God delivers them into your hands, and you carry them away captive,

ukaona kati ya mateka mwanamke mzuri, ukafanya tamaa kwake, ukawaza kumtwaa kuwa mkeo; Kumbukumbu la Torati 21:11

and see among the captives a beautiful woman, and you have a desire to her, and would take her to you as wife;

ndipo umchukue kwenu nyumbani kwako, naye atanyoa kichwa, akate na kucha; Kumbukumbu la Torati 21:12

then you shall bring her home to your house; and she shall shave her head, and pare her nails;

avue na mavazi ya uteka wake akae nyumbani mwako, awakalie matanga babaye na mamaye mwezi mzima, kisha uingie kwake uwe mumewe, naye awe mkeo. Kumbukumbu la Torati 21:13

and she shall put the clothing of her captivity from off her, and shall remain in your house, and bewail her father and her mother a full month: and after that you shall go in to her, and be her husband, and she shall be your wife.

Tena utakapokuwa huna furaha naye, mpe ruhusa aende atakako; lakini usimwuze kabisa kwa fedha, usimfanye kama mtumwa, kwa kuwa ulimtweza. Kumbukumbu la Torati 21:14

It shall be, if you have no delight in her, then you shall let her go where she will; but you shall not sell her at all for money, you shall not deal with her as a slave, because you have humbled her.

Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa; Kumbukumbu la Torati 21:15

If a man have two wives, the one beloved, and the other hated, and they have borne him children, both the beloved and the hated; and if the firstborn son be hers who was hated;

ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu; Kumbukumbu la Torati 21:16

then it shall be, in the day that he causes his sons to inherit that which he has, that he may not make the son of the beloved the firstborn before the son of the hated, who is the firstborn:

lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye. Kumbukumbu la Torati 21:17

but he shall acknowledge the firstborn, the son of the hated, by giving him a double portion of all that he has; for he is the beginning of his strength; the right of the firstborn is his.

Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, Kumbukumbu la Torati 21:18

If a man have a stubborn and rebellious son, who will not obey the voice of his father, or the voice of his mother, and, though they chasten him, will not listen to them;

ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake; Kumbukumbu la Torati 21:19

then shall his father and his mother lay hold on him, and bring him out to the elders of his city, and to the gate of his place;

wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi. Kumbukumbu la Torati 21:20

and they shall tell the elders of his city, This our son is stubborn and rebellious, he will not obey our voice; he is a glutton, and a drunkard.

Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa. Kumbukumbu la Torati 21:21

All the men of his city shall stone him to death with stones: so shall you put away the evil from the midst of you; and all Israel shall hear, and fear.

Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti; Kumbukumbu la Torati 21:22

If a man have committed a sin worthy of death, and he be put to death, and you hang him on a tree;

mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako. Kumbukumbu la Torati 21:23

his body shall not remain all night on the tree, but you shall surely bury him the same day; for he who is hanged is accursed of God; that you don't defile your land which Yahweh your God gives you for an inheritance.