Kumbukumbu la Torati 33 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 33 (Swahili) Deuteronomy 33 (English)

Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. Kumbukumbu la Torati 33:1

This is the blessing, with which Moses the man of God blessed the children of Israel before his death.

Akasema,Bwana alitoka Sinai,Akawaondokea kutoka Seiri;Aliangaza katika kilima cha Parani,Akaja Meribath-Kadeshi.Upande wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao. Kumbukumbu la Torati 33:2

He said, Yahweh came from Sinai, Rose from Seir to them; He shined forth from Mount Paran, He came from the ten thousands of holy ones: At his right hand was a fiery law for them.

Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako. Kumbukumbu la Torati 33:3

Yes, he loves the people; All his saints are in your hand: They sat down at your feet; [Everyone] shall receive of your words.

Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. Kumbukumbu la Torati 33:4

Moses commanded us a law, An inheritance for the assembly of Jacob.

Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja. Kumbukumbu la Torati 33:5

He was king in Jeshurun, When the heads of the people were gathered, All the tribes of Israel together.

Reubeni na aishi, asife; Lakini watu wake na wawe wachache. Kumbukumbu la Torati 33:6

Let Reuben live, and not die; Nor let his men be few.

Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee Bwana, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake. Kumbukumbu la Torati 33:7

This is [the blessing] of Judah: and he said, Hear, Yahweh, the voice of Judah, Bring him in to his people. With his hands he contended for himself; You shall be a help against his adversaries.

Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba. Kumbukumbu la Torati 33:8

Of Levi he said, Your Thummim and your Urim are with your godly one, Whom you did prove at Massah, With whom you did strive at the waters of Meribah;

Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona; Wala nduguze hakuwakubali; Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe; Maana wameliangalia neno lako, Wamelishika agano lako. Kumbukumbu la Torati 33:9

Who said of his father, and of his mother, I have not seen him; Neither did he acknowledge his brothers, Nor knew he his own children: For they have observed your word, Keep your covenant.

Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako, Wataweka uvumba mbele zako, Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako. Kumbukumbu la Torati 33:10

They shall teach Jacob your ordinances, Israel your law: They shall put incense before you, Whole burnt offering on your altar.

Ee Bwana, ubariki mali zake, Utakabali kazi ya mikono yake; Uwapige viuno vyao waondokao juu yake, Na wenye kumchukia, wasiinuke tena. Kumbukumbu la Torati 33:11

Bless, Yahweh, his substance, Accept the work of his hands: Smite through the loins of those who rise up against him, Of those who hate him, that they not rise again.

Akamnena Benyamini, Mpenzi wa Bwana atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake. Kumbukumbu la Torati 33:12

Of Benjamin he said, The beloved of Yahweh shall dwell in safety by him; He covers him all the day long, He dwells between his shoulders.

Na Yusufu akamnena, Nchi yake na ibarikiwe na Bwana; Kwa vitu vya thamani vya mbinguni, kwa huo umande, Na kwa kilindi kilalacho chini, Kumbukumbu la Torati 33:13

Of Joseph he said, Blessed of Yahweh be his land, For the precious things of the heavens, for the dew, For the deep that couches beneath,

Na kwa vitu vilivyo bora vya matunda ya jua, Na kwa vitu vilivyo bora vya maongeo ya miezi, Kumbukumbu la Torati 33:14

For the precious things of the fruits of the sun, For the precious things of the growth of the moons,

Na kwa vitu viteule vya milima ya kale, Na kwa vitu vilivyo bora vya vilima vya milele, Kumbukumbu la Torati 33:15

For the chief things of the ancient mountains, For the precious things of the everlasting hills,

Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze. Kumbukumbu la Torati 33:16

For the precious things of the earth and the fullness of it, The good will of him who lived in the bush. Let [the blessing] come on the head of Joseph, On the crown of the head of him who was separate from his brothers.

Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase. Kumbukumbu la Torati 33:17

The firstborn of his herd, majesty is his; His horns are the horns of the wild-ox: With them he shall push the peoples all of them, [even] the ends of the earth: They are the ten thousands of Ephraim, They are the thousands of Manasseh.

Na Zabuloni akamnena, Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako; Kumbukumbu la Torati 33:18

Of Zebulun he said, Rejoice, Zebulun, in your going out; Issachar, in your tents.

Watayaita mataifa waje mlimani; Wakasongeze huko sadaka za haki; Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari, Na akiba zilizofichamana za mchangani. Kumbukumbu la Torati 33:19

They shall call the peoples to the mountain; There shall they offer sacrifices of righteousness: For they shall suck the abundance of the seas, The hidden treasures of the sand.

Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa. Kumbukumbu la Torati 33:20

Of Gad he said, Blessed be he who enlarges Gad: He dwells as a lioness, Tears the arm, yes, the crown of the head.

Akajichagulia sehemu ya kwanza, Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria; Akaja pamoja na wakuu wa watu, Akaitekeleza haki ya Bwana, Na hukumu zake kwa Israeli. Kumbukumbu la Torati 33:21

He provided the first part for himself, For there was the lawgiver's portion reserved; He came [with] the heads of the people; He executed the righteousness of Yahweh, His ordinances with Israel.

Na Dani akamnena, Dani ni mwana-simba, Arukaye kutoka Bashani. Kumbukumbu la Torati 33:22

Of Dan he said, Dan is a lion's cub, That leaps forth from Bashan.

Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na baraka ya Bwana; Umiliki magharibi na kusini. Kumbukumbu la Torati 33:23

Of Naphtali he said, Naphtali, satisfied with favor, Full with the blessing of Yahweh, Possess you the west and the south.

Na Asheri akamnena, Na abarikiwe Asheri kwa watoto; Na akubaliwe katika nduguze, Na achovye mguu wake katika mafuta. Kumbukumbu la Torati 33:24

Of Asher he said, Blessed be Asher with children; Let him be acceptable to his brothers, Let him dip his foot in oil.

Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako. Kumbukumbu la Torati 33:25

Your bars shall be iron and brass; As your days, so shall your strength be.

Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake. Kumbukumbu la Torati 33:26

There is none like God, Jeshurun, Who rides on the heavens for your help, In his excellency on the skies.

Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza. Kumbukumbu la Torati 33:27

The eternal God is [your] dwelling-place, Underneath are the everlasting arms. He thrust out the enemy from before you, Said, Destroy.

Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande. Kumbukumbu la Torati 33:28

Israel dwells in safety, The fountain of Jacob alone, In a land of grain and new wine; Yes, his heavens drop down dew.

U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.

Kumbukumbu la Torati 33:29

Happy are you, Israel: Who is like you, a people saved by Yahweh, The shield of your help, The sword of your excellency! Your enemies shall submit themselves to you; You shall tread on their high places.