Kumbukumbu la Torati 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 20 (Swahili) Deuteronomy 20 (English)

Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. Kumbukumbu la Torati 20:1

When you go forth to battle against your enemies, and see horses, and chariots, [and] a people more than you, you shall not be afraid of them; for Yahweh your God is with you, who brought you up out of the land of Egypt.

Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu, Kumbukumbu la Torati 20:2

It shall be, when you draw near to the battle, that the priest shall approach and speak to the people,

awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao; Kumbukumbu la Torati 20:3

and shall tell them, Hear, Israel, you draw near this day to battle against your enemies: don't let your heart faint; don't be afraid, nor tremble, neither be scared of them;

kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi. Kumbukumbu la Torati 20:4

for Yahweh your God is he who goes with you, to fight for you against your enemies, to save you.

Na maakida na waseme na watu, na kuwaambia, Ni mtu gani aliye hapa aliyejenga nyumba mpya, wala hajaiweka wakfu? Aende akarudi nyumbani kwake, asije akafa mapiganoni, ikawekwa wakfu na mtu mwingine. Kumbukumbu la Torati 20:5

The officers shall speak to the people, saying, What man is there who has built a new house, and has not dedicated it? let him go and return to his house, lest he die in the battle, and another man dedicate it.

Ni mtu gani aliye hapa aliyepanda shamba la mizabibu, wala hajatumia matunda yake? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, yakatumiwa na mtu mwingine matunda yake. Kumbukumbu la Torati 20:6

What man is there who has planted a vineyard, and has not used the fruit of it? let him go and return to his house, lest he die in the battle, and another man use the fruit of it.

Ni mtu gani aliye hapa aliyemposa mke wala hajaoa? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, huyo mwanamke akaolewa na mume mwingine. Kumbukumbu la Torati 20:7

What man is there who has pledged to be married a wife, and has not taken her? let him go and return to his house, lest he die in the battle, and another man take her.

Tena maakida na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake. Kumbukumbu la Torati 20:8

The officers shall speak further to the people, and they shall say, What man is there who is fearful and faint-hearted? let him go and return to his house, lest his brother's heart melt as his heart.

Itakuwa hapo watakapokwisha wale maakida kusema na watu, na waweke majemadari wa majeshi juu ya watu. Kumbukumbu la Torati 20:9

It shall be, when the officers have made an end of speaking to the people, that they shall appoint captains of hosts at the head of the people.

Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani. Kumbukumbu la Torati 20:10

When you draw near to a city to fight against it, then proclaim peace to it.

Itakuwa utakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo watakufanyia kazi ya shokoa, na kukutumikia. Kumbukumbu la Torati 20:11

It shall be, if it make you answer of peace, and open to you, then it shall be, that all the people who are found therein shall become tributary to you, and shall serve you.

Na kwamba hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uuhusuru; Kumbukumbu la Torati 20:12

If it will make no peace with you, but will make war against you, then you shall besiege it:

na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga; Kumbukumbu la Torati 20:13

and when Yahweh your God delivers it into your hand, you shall strike every male of it with the edge of the sword:

lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako. Kumbukumbu la Torati 20:14

but the women, and the little ones, and the cattle, and all that is in the city, even all the spoil of it, shall you take for a prey to yourself; and you shall eat the spoil of your enemies, which Yahweh your God has given you.

Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya. Kumbukumbu la Torati 20:15

Thus shall you do to all the cities which are very far off from you, which are not of the cities of these nations.

Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho; Kumbukumbu la Torati 20:16

But of the cities of these peoples, that Yahweh your God gives you for an inheritance, you shall save alive nothing that breathes;

lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako; Kumbukumbu la Torati 20:17

but you shall utterly destroy them: the Hittite, and the Amorite, the Canaanite, and the Perizzite, the Hivite, and the Jebusite; as Yahweh your God has commanded you;

wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya Bwana, Mungu wenu. Kumbukumbu la Torati 20:18

that they not teach you to do after all their abominations, which they have done to their gods; so would you sin against Yahweh your God.

Wewe utakapohusuru mji siku nyingi kwa kufanya vita juu yake, upate kuutwaa, usiangamize miti yake kwa kupeleka shoka juu yake, kwani utaweza kula matunda yake; wala usiiteme, kwa maana huo mti wa kondeni, je! Ni mtu, hata ukauzuie? Kumbukumbu la Torati 20:19

When you shall besiege a city a long time, in making war against it to take it, you shall not destroy the trees of it by wielding an axe against them; for you may eat of them, and you shall not cut them down; for is the tree of the field man, that it should be besieged of you?

Ila miti uijuayo si miti ya kuliwa iangamize, na kuitema; ukajenge maburuji juu ya mji ufanyao vita juu yako, hata uanguke. Kumbukumbu la Torati 20:20

Only the trees of which you know that they are not trees for food, you shall destroy and cut them down; and you shall build bulwarks against the city that makes war with you, until it fall.