Solomon Mukubwa - Nimewasamehe Wote Lyrics

Nimewasamehe Wote Lyrics

Mmmh Ooh ,oooh, Nilipokuwa mtoto,
nilizaliwa kama wewe,
viungo vyote vya mwili ,
vilikuwa kama wewe,
ghafla dunia ,mambo yakageuka,
nikajikuta kiugo kimoja kimeniondokea,
mimi nikajua kuwa, mwisho wa mambo yote imefika,
wala sifai nikaona dunia imenitupa ,
nikaona dunia imenidharau,
nikajidharau mwenyewe nikajua sasa mimi,
sifai tena niliwanung’unikia,
wote waliohusika kwa haya mambo,
roho ya kisasi ikaja juu yangu,
nikajua sasa na mimi ,nitalipa kisasi,
kumbe kunaye mungu ,mungu wa visasi
Akaniambia, Solomon nina mpango na wewe ,
lazima piga hatua ,uwasamehe kwanza,
ooh nikabishana na mungu ,
Wote walionitendea mabaya ,
mimi siwezi wasamehe,
Moyoni mwangu ,bwana kaniambia ,
wataka nitumike na wewe,
nina ahadi zuri na wewe,
kuhusu dunia hii ukitaka nitumike na wewe ,
uwaachilie wote,uliowaweka moyoni mwako ,
Nikapiga hatua nikawasamehe, wote walionikosea
Bwana akatumika na mimi ooh
(Refrain)
Nimewasamehe wote nimewasamehe wpte
nimewasamehe kutoka moyoni mwangu,
nimewasamehe wote
nimewachilia kutoka moyoni mwangu

Tumekunywa damu, damu ya yesu
Tumekula na mwili wa yesu ooh,
mwili wa yesu ni msamaha, aah tujikane wenyewe,
Mara nyingi tumeonekana wajinga duniani,
dunia imeshindwa kutuelewa wakristo, eeh
Umetendewa mabaya ,lakini neno linasema,
kubali nenda ukaombe msamaha, ki kawaida ya dunia,
ukinitendea mabaya lazima ooh ieleweke,
Lakini kwetu sisi wakristo ,ukinitendea mabaya ,
mimi lazima nikusamehe,
Sababu nisipokusamehe
Baba yetu wa mbinguni , na yeye hawezi nisamehe,
haijalishi unapitia nini,
kama wewe umeokoka,
huwasamehe waliokukosea ooh eeh
Husifanye moyo walo jela,
kuwafungia wat amua leo uwaondoe,
ili mungu wetu akubariki ,
samehe jirani yako,
mungu na yeye atakusamehe

Nimewasamehe wote nimewasamehe wpte
nimewasamehe kutoka moyoni mwangu,
nimewasamehe wote
nimewachilia kutoka moyoni mwangu

"Ni vigumu jamani mara nyingi ,
kuna mambo ambayo tunapitia ,
mwenzako mwanadamu anakupitisha kwa mambo mazito,
Lakini unapaswa ufanyeje ,
ashurukuriwe mungu sababu neno la mungu linasema tusamehe tu,
Na tumevaa mwili wa yesu,
tumekunywa damu ya yesu,
kumbuka msalabani, yesu aliwaponya watu,
viwete wakatembea mabubu wakaongea,
akawalisha watu, zaidi ya elfu tano,
lakini wale watu ndio walimuweka msalabani,
Mwisho msalabani ikasema baba wasamehe, huwasamehe, ,
kumbuka stephano, Stephano alikuwa anapigwa mawe ,
alipokuwa anapigwa mawe,bibilia inasema ,
stephano kaambia baba huwasamehe,
maana hawajui wanalolitenda bibilia inasema
stephano akaona mbingu zinafunguka ,
kwenye msamaha kuna nguvu,
kwenye msamaha kuna uwezo,
stephano hakujali tena mawe wanayomtupia ,wanayomchapa
Lakini stephano alikuwa ameona mbingu zimefunguka,
na tayari anakwenda kupokelewa, Msamahe jirani yako ,
kusudi uone mkona wa mungu,
Usimfungie kwenye moyo wako ,
utakuwa umujizuilia baraka yako,
msamehe muachilie tu,
Maana tumevaa mwili wa yesu,
na tumekunywa damu ya yesu,
ooh yesu tusaidie kuwasamehe waliotukosea "


Pengine una watu,
ambao umefungia moyoni wala hutaki kuwasamehe,
nakwambia leo, fungua moyo wako,
ili mungu wa mbinguni akusamehae,
husijiwekelee vikwazo ,
maisha ni mafupi yesu yu karibu kuja,
Uwasamehe wote waliokukosea,
Ili uone mbingu ooh, hatujui ya kesho ,
ya kesho ni ya mungu ,
fungua moyo wako leo ,yule uliye mkopa hela ,
kashindwa kurudisha, sasa leo amekutusi ,
na yeye umsamehe,
uwe safi mbele ya mungu yesu yu karibu kuja

Nimewasamehe wote nimewasamehe wpte
nimewasamehe kutoka moyoni mwangu,
nimewasamehe wote
nimewachilia kutoka moyoni mwangu


Nimewasamehe Wote Video

Nimewasamehe Wote Lyrics -  Solomon Mukubwa

Solomon Mukubwa Songs

Related Songs