Roho Yangu Naikuimbie

Roho Yangu Naikuimbie Lyrics

Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu. .

Bwana Mungu nashangaa kabisa,
Nikifikiri jinsi ulivyo,
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia,
Viumbavyo kwa uwezo wako. .

Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu. .

Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba nawasikia,
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia. .

Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu. .Nikikumbuka vile wewe Mungu,
Ulivyompeleka mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno. .

Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu. .

Yesu Mwokozi atakaporudi,
Kunichukua kwenda mbinguni,
Nitaimba sifa zako milele,
Wote wajue jinsi ulivyo. .

Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu. .


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Roho Yangu Naikuimbie:

0 Comments/Reviews