Sifa Lyrics

Zamu ni Yangu by The Saints Ministers cover art

The Saints Ministers - Zamu ni Yangu Lyrics

Artist:
The Saints Ministers

Lyrics

Zamu ni yangu ya huduma, zamu ni yetu ya huduma, 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma. 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma.


Bridge:


Mwanzilishi wa huduma hii, 


Mwana wa Mungu alihudumu kwa wote. 


Aliyeshuka alipaa juu mbinguni avijaze vyote, Akatoa mitume manabii, wachungaji, wainjilisti, na walimu. 


Zamu ni yangu ya huduma, zamu ni yetu ya huduma, 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma. 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma.


Stanza 2


Kwa kusudi la kuwakamilisha, watakatifu wote, 


Hata kazi ya Huduma, itendeke, hata mwili wa Kristo, ujengwe. 


Bridge:


Mwanzilishi wa huduma hii, mwana wa Mungu alihudumu kwa wote. 


Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa Imani, na kumfahamu sana Mwana wa Mungu mkamilifu, tufikie kimo chake cha utimilifu. 


Zamu ni yangu ya huduma, zamu ni yetu ya huduma, 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma. 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma.


Stanza 3


Kwa maana nilikuwa njaa hukunilisha, Nilikuwa na kiu hukuninywesha


Mgeni kwako mimi sikukaribishwa. 


Uchi wangu hukunivika


Nilikuwa hospitali sikutembelewa, 


Kifungoni nilikuwa hukunijia


Muda ni sasa Mwenzangu hudumu kwa wote, 


ili siku ya mwisho uwe mrithi. 


Zamu ni yangu ya huduma, zamu ni yako ya huduma, 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma. 


sitakimya sitalegea nitasimama niende 


zamu ni yangu ya Huduma.


Video