Mifulizo Ya Baraka

Mifulizo Ya Baraka Lyrics

Mungu, Elshadai wetu, matendo yako makuu, 
umetukamilisha twajivunia (mifulizo) ya baraka zako. .

Twala, twanywa, twalala, twaamka, 
uaminifu wako kwetu mkuu, 
Hitaji letu tunalo 
baraka zako zafululiza twashukuru kwazo. .

1. Hannah alibezwa kwa kukosa mtoto, 
hakukataa tamaa, aliomba, wakati wa Mungu ulipofika 
Samweli kazaliwa baraka nyumbani mwake. .

2. Waangalieni Ndege wa angani, hawapandi wala hawavuni, 
hawakusanyi ghalani, ila Baba wa mbinguni huwalisha hao. .

Twala, twanywa, twalala, twaamka, uaminifu wako kwetu mkuu, 
Hitaji letu tunalo baraka zako zafululiza twashukuru kwazo. .

Wengine walala hoi nawe wala na kusaaza wahitaji nini? 
Mbona walilia cheo wengine hawana kazi, wahitaji nini? 
Wengine wamelazwa na wewe una afya.. Mshukuru Mungu.. .

Hesabu mibaraka moja moja, aogeleavyo papa baharini,  
Mwanga wa jua hung'aa kote mvua ya masika hutunyea ilivyo baraka zake.  .

Ilivyo nyota angani ndivyo baraka zake, Utukuzwe Mungu.  .

Mungu, Elshadai wetu, matendo yako makuu, 
umetukamilisha twajivunia (mifulizo) ya baraka


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Mifulizo Ya Baraka:

0 Comments/Reviews