Sifa Lyrics

Zangu ni Shukrani by The Saints Ministers cover art

The Saints Ministers - Zangu ni Shukrani Lyrics

Artist:
The Saints Ministers

Lyrics

Nasifu Shani zako Elohim, safari mbali umenileta 


Sina budi kuzishukuru hisani zako kuu. 


Kwa ukarimu wako nabarikiwa 


nitatoa nini kwako Bwana na vyote ni vyako 


miye ni mlinzi ulivyoagiza Edeni..


Zangu zangu, Zangu zangu, 


Zangu ni Shukrani Mungu


Sina neno uwapo karibu, nipatalolote si taabu, 


Kifo na kaburi haviumi nitashinda kwako. 


Nilalapo nikuone wewe, gizani mote nimulikiwe 


nuru za mbinguni kweli hazikomi, 


Siku zangu zote, kaa nami Bwana. 


Zangu zangu, Zangu zangu, 


Zangu ni Shukrani Mungu


Mapenzi yako sasa yatimie, wewe mfinyanzi mimi tope, 


Unihojie dhambi zote, Unisafi Bwana. 


Natoa vitu vyote kwako leo, maisha, mali, moyo vipokee, 


mwili wangu wote ni Hekalu lako, Niongozee Bwana, N'takuimbia. 


Zangu zangu, Zangu zangu, 


Zangu ni Shukrani Mungu


#7thDayAdventist


#TheSaintsMinisters


Video