Amini

Amini Lyrics

Sijui sababu ya neema aah 
Niliyopewa na Mungu wetu uuh 
Sikustahili pendo lake eeh 
Wala wokovu wa Yesu kristo  .

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini
Maombi yako yako yatajibiwa  .

Sijui jinsi nilivyopewa 
Imani ya kumwamini Yesu kristo 
Neno lake Yesu lilileta amani yake moyoni mwangu  .

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa  .

Sijui jinsi roho wa Mungu 
Awaonyeshavyo watu wake 
Wapate kuzitambua dhambi 
Na kufuata Yesu mkombozi  .

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa  .

Sijui kama mambo yajayo 
Yatakuwa ya salama kwangu 
Lakini ninamwamini Yesu 
Mpaka tutaonana naye  .

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa  .

Sijui siku gani ya Bwana 
Hapa atakaporudi kwetu 
Nitamngojea kwa imani 
Hata kumlaki hewani mwisho  .

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa 


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Amini:

0 Comments/Reviews