Solomon Mukubwa - Futa Machozi Lyrics
Lyrics
Nalimngoja Bwana kwa zaburi Akaniinamia akanisikia kilio changu Akanipandisha toka shimo, shimo la uharibifu Akanisimamisha Bwana, toka udongo wa utelezi, Akasimamisha miguu yako mwambani, Bwana wangu wee Akazisimamisha hatua zangu, akazipanga sawa sawa Ili nimtumikie ee eh, ndio sifa zake zimekaa midomoni mwangu Ameweka wimbo mpya midomoni mwangu Ndio maana ninaamba sifa zako Mungu wangu Ndio maana kila siku nashuhudia wema wake Bwana
Futa futa machozi usilie tena, kibali kiko juu yako Simama kama shujaa, ushambulie malango* Sayuni imekukubali
Hatutaki kulia lia sana, hatutaki ukristo wa kulilia sana. Sisi ni washindi, hata tupipitie moto haitatuchoma Hata tukitupwa baharini, samaki haitatumaliza Hata tupitie maji, haitatukarigisha, maaana sisi ni washindi. Mkristo simama kama shujaa, ushambilie malango Umepewa mamlaka na kibali, mbona umeonelewa na adui kiasi hii, ebu simama kama shujaa, mpingeni adui naye atawakimbia, sisi ni washindi zaidi ya washindi.
Futa futa machozi usilie tena, kibali kiko juu yako Simama kama shujaa, ushambulie malango* Sayuni imekukubali
" Lazima tujiamini lazima kujitwaa, tumepewa mamlaka
ya kukanyaga nyoka na yule ibilisi, na kila ufalme wa
ulimwengu wa giza, hazina mamlaka juu Yeu"
Futa futa machozi usilie tena, kibali kiko juu yako Simama kama shujaa, ushambulie malango* Sayuni imekukubali
Video
Futa Machozi by Solomon Mkubwa Official Video 2017