Sifa Lyrics

Tutazame Kule Mbele by PaPi Clever & Dorcas cover art

PaPi Clever & Dorcas - Tutazame Kule Mbele Lyrics

Artist:
PaPi Clever & Dorcas
Album:
AMENIWEKA HURU KWELI (Nyimbo za wokovu) ALBUM 2
Official Release:
30 Jun 2023

Lyrics

Tutazame kule mbele, asubuhi inakuja
Tuamini Mungu wetu, atafanya kazi yake
Kufukuza mashetani, kumiliki nchi yote
Tutashinda tukiomba, Mungu anatusikia
Tutashinda tukiomba, Mungu anatusikia


Tarumbeta linalia, tuamke wote sasa
Mungu wetu anataka sisi sote tutakaswe
Kila mtu awe safi katika kanisa lake
Uliache nung’uniko, utapata nguvu yake
Uliache nung’uniko, utapata nguvu yake


Imba ninyi, watu wake, Bwana yu pamoja nasi
Tutashinda majaribu kwa uwezo wake Yesu
Twende tumhudumie kwa kumpa mali yake
Hata roho na akili zimtumikie Bwana
Hata roho na akili zimtumikie Bwana


Watu wengi hawajui njia yakufika mbingu
Wanakuwa wamefungwa kwa mikono ya shetani
Twende tukawatafute, tuwavute kwa mwokozi
Na kuomba na kukesha hata kuja kwake Yesu
Na kuomba na kukesha hata kuja kwake Yesu


Video