Sifa Lyrics

NINATAKA KUFUATA by PaPi Clever & Dorcas cover art

PaPi Clever & Dorcas - NINATAKA KUFUATA Lyrics

Artist:
PaPi Clever & Dorcas
Album:
MAISHA KATIKA DUNIA
Official Release:
17 Nov 2025

Lyrics

Verse 1
Ninataka kufuata wewe, Yesu, siku zote
kiwa katika furaha au shida na udhia
Unaponitangulia ninakuja nyuma mbio
Ninajua ni karibu kuwasili huko kwako


Verse 2
Haifai niulize: Bwana, unakwenda wapi?
Au kwa kusitasita kuishika njia yako
Kweli hapa kazi moja: Kufuata wewe mbio
Kwenda njia ile moja wewe unionyeshayo


Bridge
Walakini kama kitu kinataka kunifunga
au kuwa mgogoro katika safari yangu
Kate kamba mara moja ifungayo roho yangu!
Ninataka kuwa huru kukutumikia vema.


Verse 3
Bwana Yesu, unilinde, uhifadhi nia yangu!
Nikichoka kwa safari, nong'oneza kwa upendo:
«Mwana, u mtoto wangu, uniandamie punde,
utapumzika sana tena kwangu huko juu»


Video