Lyrics
"Sawa Na Bahari" by Papi Clever & Dorcas ft. Merci Pianist.
Verse 1
Nataka kupokea baraka yake Mungu
Nataka kubatizwa kwa Roho takatifu
Juu ya ahadi yake napumzika sana
Aliahidi mimi kupata Roho yake
Chorus
Sawa na bahari, sawa na bahari
Ni neema yake anileteayo
Anayenijaliza, anayeniponyesha
Ni Mwokozi wangu, Asifiwe sana!
Verse 2
Kanisa lake Mungu linapata mvua
Vijito vya baraka vinamiminwa sasa
Furaha ya uzima ni kubwa kati yetu
Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!
Chorus
Sawa na bahari, sawa na bahari
Ni neema yake anileteayo
Anayenijaliza, anayeniponyesha
Ni Mwokozi wangu, Asifiwe sana!
Verse 3
Mawimbi ya wokovu yanatujia sasa
E Mungu, tunaomba: Ujaze sisi sote!
Watakatifu wako watakasike sana!
Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!
Chorus
Sawa na bahari, sawa na bahari
Ni neema yake anileteayo
Anayenijaliza, anayeniponyesha
Ni Mwokozi wangu, Asifiwe sana!
Verse 4
Mawimbi ya wokovu yaliyofika kwetu
E Mungu, uyatume ulimwenguni mwote
Maelfu kati watu wapate kuokoka
Waimbe haleluya, wamshukuru Yesu!
Chorus
Sawa na bahari, sawa na bahari
Ni neema yake anileteayo
Anayenijaliza, anayeniponyesha
Ni Mwokozi wangu, Asifiwe sana!