PaPi Clever & Dorcas - E’ Mungu Mwenye Haki Lyrics

E’ Mungu Mwenye Haki Lyrics

E’ Mungu mwenye haki, uniongoze huku
Katika mambo yote yanayokupendeza
Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka
Yananitia tetemeko mpaka kufa
Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka
Yananitia tetemeko mpaka kufa

Ni heri siku zote kutegemea Yesu
Na kuenenda sawa katika nyayo zake
Kwa kuwa yeye ni mchunga anayeniongoza vema
Nipate kuingia katika raha yake
Kwa kuwa yeye ni mchunga anayeniongoza vema
Nipate kuingia katika raha yake

Safari yangu sasa yaelekea mbingu
Mwokozi yuko huko, lazima nifikeko
Na siku nitakapofika ‘tashangilia kwa furaha
Kuona yeye aliyeninunua kwake
Na siku nitakapofika ‘tashangilia kwa furaha
Kuona yeye aliyeninunua kwake

Ulimwenguni humu, matata na kuchoka
Nikihitaji kitu nafadhahika bure
Lakini siku ile kuu nita’pomwona Mwokozi
Natumaini sitakosa dhawabu yangu
Lakini siku ile kuu nita’pomwona Mwokozi
Natumaini sitakosa dhawabu yangu

Mbinguni sitaona adui zangu tena
Hayatakuwa mambo yakupokonya pale
Mbinguni sitaona adui zangu tena
Hayatakuwa mambo yakupokonya pale
Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya
Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu
Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya
Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu

E’ Mungu Mwenye Haki Video

PaPi Clever & Dorcas Songs

Related Songs