Sifa Lyrics

Maisha Katika Dunia by PaPi Clever & Dorcas cover art

PaPi Clever & Dorcas - Maisha Katika Dunia Lyrics

Artist:
PaPi Clever & Dorcas
Album:
AMENIWEKA HURU KWELI (Nyimbo za wokovu) ALBUM 2
Official Release:
30 Jun 2023

Lyrics

Maisha katika dunia ni kama kupanda na ‘vuna
Apandaye katika mwili atavuna uharibifu
Tukitumikia Mwokozi tutapata thawabu mbinguni
Yafaa kuishi na kufa katika maneno ya Mungu

Kwa neema kubwa kabisa tumekubaliwa na Mungu
Kwa neema kubwa zaidi twapata kumtumikia
Kuishi kwa ‘jili ya yesu kati’ yote ya dunia hii
Na kuitangaza injili ni faida kwetu kabisa

Wakristo wata’poingia mbinguni kusifu Mwokozi
Na mimi nataka kufika kuimba pamoja na wao
Tutamshukuru mwokozi aliyetununua kwa damu
Waliohudumu kwa pendo watamhimidi milele

Video