Hauwezi Kushindana

Mp3

Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya 
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya

Kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu
Mbona sasa ngingekuwa na vidonda mwili mzima 
Vita ya maneno kuna watu majemedari 
Ukisema mshindane mbona mikono utainua 
Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue 
Wewe ni mti wenye matunda zoea mawe 

Lia kidogo nyamaza ili uchungu uishe 
Ukiendelea unawapa kichwa hawa 
Vaa silaha za imani rejea vitani 
Wakikuona waseme umeshakua sugu 
Acha waonge acha waseme seme 
Ila yupo Mungu wakuwaziba Midomo  

Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya 

Ikiwa Mungu anahukumu kwa kuskiza maneno 
Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana 
Hivi Mungu angehukumu kwa kuskiza umbeya 
Si ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa 
Mwanadamu mwanadamu shida ni ulimi 
Ungejifunza ukimya haunanga hasara 
Fulani we fulani unashida gani, na uongo wa nini? 
Mwogope Mungu, ukumbuke ni ahadi kuna siku yaja 
Kwa kila neno la kinywa chako utatolea hesabu 
Mimi si Nimeshakwambia kubali uache 
Utajijua na shingo yako ngumu ayaya 
Siwezi kushindana, na mwanadamu mwenye kinywa 

Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya

Yesu huyu Yesu Hakujitetea kabisa 
Japo walimsema kwa ubaya aliwasamehe 
Na wewe uwasamehe uwaombee kwa maana hawajui wasemayo 
Wakifanyanga ubaya uwajibu kwa wema 
Usishindane na mtu wajibu kwa wema 
Hata iwe ni ndugu wa karibu wajibu kwa wema 
Si vizuri wewe usilipe kisasi 
Wajibu kwa wema 
Tenda wema uende 
Wajibu kwa wema 
ah ah ah, wajibu kwa wema 
oh maana maana 

Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Hauwezi Kushindana :

4 Comments/Reviews

 • EKARU SHABAN

  Napenda utunzi wa nyimbo huu,ubarikiwe xna...another one kama io tna.big up 6 months ago

 • Emmanuelwangila

  Barikiwa sana. I love the message in this song ❤️.... Barikiwa sana kaka yangu 10 months ago

 • Jael Maghanga

  Wow... I love the message in this song, barikiwa sana kakangu
  Hakika kuna ujumbe 1 year ago

 • Adam Kwathema

  Barikiwa Sana ....
  Na ukweli halisi ....
  Umewakuna vichwa wengi Sanaa...
  1 year ago


 • Bible Verses for Hauwezi Kushindana

  Leviticus 19 : 16

  Thou shalt not go up and down as a talebearer among thy people: neither shalt thou stand against the blood of thy neighbor: I am Jehovah.

  Psalms 1 : 1

  Blessed is the man that walketh not in the counsel of the wicked, Nor standeth in the way of sinners, Nor sitteth in the seat of scoffers:

  2nd Chronicles 20 : 15

  and he said, Hearken ye, all Judah, and ye inhabitants of Jerusalem, and thou king Jehoshaphat: Thus saith Jehovah unto you, Fear not ye, neither be dismayed by reason of this great multitude; for the battle is not yours, but God's.