Sifa Lyrics

Shukrani by Goodluck Gozbert cover art

Goodluck Gozbert - Shukrani Lyrics

Artist:
Goodluck Gozbert

Lyrics

Nina kushukuru Mungu sababu ya mengi, hata uhai huu sikustahili


Nina kushukuru Mungu tena sababu ya vingi, hata nikiwa nasali unajua namaanisha


Sio kama eti nilitenda wema wakuja linganisha na matendo yako makuu mimi Mungu ningekulipa nini


Ulikonitoa ni siri ya moyo matopeni topeni ukaniketisha na wakuu juu


Nina kushukuru Mungu sababu ya mengi, hata uhai huu sikustahili


Umenipa heshima ukanifuta machozi asante ooh baba


Hata shukurani zangu ni kwako
Shukrani zangu ni kwako
Na shukurani zangu ni kwako
Shukurani zangu ni kwako, asante baba ooh


Aibu umefuta fedheha umefuta
Umenipa amani iliyo ya kweli nakumbuka nalia mimi ni yule ambae


Nilitukanwa na kwa dharau wakasema kwisha habari yake kuna kipindi nilikufa nikawa mifupa inayotembea


Ikiwa kwa siku za usoni walisema tunazika kesho ila kwa huruma uliniponya na kaburi kwa hurumaa na sitosahau wema wako wee baba


Video