Hata nikiwa sina chakula
Isinifanye kusahau
Ulinilisha nikasaza
Hata nikiwa sina mavazi
Isinifanye nifukuru
Na kusahau umeniweka hai
Ona wapo marafiki
Wanakosa kula na kuvaa
Hawalalamiki, wanakushukuru tu
Mimi eh, nilikupa nini Baba
Cha kunipa kibali
Kwa siku zilizofurahisha?
Taabu kidogo zisinifanye nikusahau
Umeshatenda mengi – nikiwa hapa
Shida itapita, bado kidogo
Ikiwa nitachoka niiunue
Refrain:
Nipe kukumbuka wema
Nipe kukumbuka wema
Nipe kukumbuka wema
Nipe kumbuka wema wako
Hata kwenye bonde hili la mauti
Nakumbuka nilikuita,
Na wewe ukaitika Baba
Kutegemea akili zangu, na mawazo yangu
Kutanifanya niendelee
niendelee kulalamika
Kuna kipindi najisahau
na kujivunia mafanikio
Wengine naona takataka
Nikumbushe mi ni mtu tu
na dunia tunapita
Uhai wangu si faida bila wewe
Mungu wewe ni mkuu
kuliko vile nakutazama Baba
Unisamehe, unisamehe
Kuna nyakati nadhani
hii dunia labda ni ya ushindani
Natumia akili zangu za ndani
Ila bado nashindwa kuendelea
Nikimbushe nisidhani
Wakifanikiwa tuna upinzani
Nifundishe kuwaombea amani
Na utatenda kwa wakati
Na ikiwa Kama nikisahau
Unikumbushe mi mtoto wako
Nipe kukumbuka wema
Nipe kukumbuka wema
Nipe kukumbuka wema
Nipe kumbuka wema wako