Unaona kama kila unachogusa kimeharibika
UJasiri wa kusema tena umetoweka
Maana kila unalosema wewe kama unakosea
Umechanganyikiwa ni Mungu ajua unayopitia
Na ukisema ueleze wengi kwao ni furaha
Wewe mwombe Mungu ubaki kimya
Na mengi umevumilia moyo umenyong'onyea
Hapo ulipo sasa ng'ang'ania tena
Na Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako.
Imani nusu ongeza utashinda.
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda.
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena usijali, Mungu yupo nawe.
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena usijali, Mungu yupo nawe.
Oooh! Mmmh!
Moyo wako una majeraha haufai
Tena unasubiri kauli ya mwisho ya Mungu
Wapo wanaojua we huna mtoto wa kejeli
Wanaulizaga ana umri gani?
Tena wanaojua umefukuzwa kazi
Kwa kejeli wanaulizaga bosi wako yupo?
Ila nakwambia hayatodumu, ni nyakati tu.
Ila nakwambia hayatodumu, ni nyakati tu,
Hautobaki hapo haya ni mapito jipe moyo
Tazama juu mwombe Mungu ujasiri
Ni mapito tu jipe moyo mkuu
Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu ongeza utashinda.
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda.
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tenA, usijali Mungu yupo nawe.
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena, usijali Mungu yupo nawe.
Hata wakizusha maneno ya uongo
Wakakwambia umemuasi Mungu
Uh ni sawa hawajui unakopita
Wakaja na unabii wakasema
umefika mwisho wako wewe
Ni sawa hawajui unakopita oooh!
Wakainuka ndugu wa karibu, wakakusema ovyo ovyo
Ni sawa hawajui unakopita
Ikawa kila kitu ni kimya marafiki ni kimya ooh
Ni sawa hawajui unakopita
Kama ndoa ni yako lakini ndani ni uadui
Ni sawa hawajui unakopita
Ila
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tenA, usijali Mungu yupo nawe.
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena, usijali Mungu yupo nawe.
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tenA, usijali Mungu yupo nawe.
Laa laa lala!
END