Goodluck Gozbert - Mungu Hapokei Rushwa Lyrics

Mungu Hapokei Rushwa Lyrics

Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 

Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 

Na wengine tuna damu mbaya  
Mabifu kama yote
Mtu hujamkosea anatamani ufe 
Wengine Bwana wee tulipewaga sura mmh 
Mtu akikuona akalinganisha hufanani 
Wewe unadhani angepewa oxygeni eeh 
Yangu angeminya, angeminya nifie mbali 
Wewe unadhani angepewa kesho yako eeh
Kwanza angefinya angefinya, ufie mbali 
Ila Mungu wee eeeh hajui kukosea 
Ametupa thamani tulioitwa vikaragosi 
Ila Mungu wee eeeh mwingi wa huruma
Ametupa vicheko, vicheko bila manoti 

Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 

Mfano jitu lipate, kama za Laiza
Lingetuchakaza vibaya, au lipate kama za Dangote 
Lipewe kuamua kesho yako eeh 
Wengine baba zetu walala hoi 
Wengine mama zetu hohehahe 
wengine familia zetu choka mbaya 
Wengine ndio kabisa mayatima 
Hakuna anayetujua wala hatuna connection mmh 
Kusema sababu ni elimu mbona wasomi kibao ni jobless 
Tumewekwa mahali kwa neema ya Mungu 
Tunavuka mapito kwa neema ya Mungu 
Huyu Mungu wee eeh hajui kukosea 
Ametupa thamani tulioitwa vikaragosi 
Ila Mungu wee eeeh mwingi wa huruma 
Ametupa vicheko, vicheko bila manoti 

Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 

Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Uzuri ni kwamba Mungu hapokei rushwa 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 
Angepewa mabilioni tungetupwa mbali sana 

Mungu Hapokei Rushwa Video

Mungu Hapokei Rushwa Lyrics -  Goodluck Gozbert

Goodluck Gozbert Songs

Related Songs