Sifa Lyrics

Afadhali Yesu by Goodluck Gozbert cover art

Goodluck Gozbert - Afadhali Yesu Lyrics

Artist:
Goodluck Gozbert

Lyrics

Nikiwa kwa matendo ya mwili
Ulinipenda hukunitupa
Nimekukosea mara nyingi 
Ukanipenda na msamaha


Na bado nakushangaa
Hujanichoka hujanichoka
Nikitazma kwenye list mimi sikudhani ungenisamehe
Sikuwa na faida eeh
Na dunia ilinikataa
Pengine ungeshanizika
Ila ukaniacha nisimulie wema wako wewe


Afadhali wewe tu
Afadhali Yesu
Afadhali wewe tu
Afadhali Yesu


Wema wako na upole wako unanishangaza
Umenipa fursa na udhaifu wangu ukanitakasa
Unaniskia nikikulilia 
Badilisha nia sasa nakutumikia 
Na nikipotea unanionyesha njia
Nakuwa msumbufu ila unanivumilia 


We baba wee
Kama ingekuwa binadamu hangeubeba msalaba
Angeutupa chini tujitegemee
Mzigo wetu tujibe, tujibebee 


We baba wee
Kama ingekuwa binadamu hangeubeba msalaba
Angeutupa chini tujitegemee
Mzigo wetu tujibe, tujibebee 


Afadhali wewe tu
Afadhali Yesu
Afadhali wewe tu
Afadhali Yesu


Nikiwa kwa matendo ya mwili
Ulinipenda hukunitupa
Yesu nimekukosea mara nyingi 
Ukanipenda na msamaha


Afadhali wewe tu
Afadhali Yesu
Afadhali wewe tu
Afadhali Yesu


Mmmmh mmmh....
Aaah aah...
Mmmmh mmmh....


Video