Sifa Lyrics

Mtetezi Wangu by Christina Shusho cover art

Christina Shusho - Mtetezi Wangu Lyrics

Artist:
Christina Shusho
Album:
Unikumbuke
Official Release:
21 Mar 2008

Lyrics

Chorus


Mtetezi wangu Yesu anaishi leo
Mtetezi wangu yu hai
(x4)


Verse 1


Ukienda kwa wanyama anaitwa Simba wa Yuda
Mtetezi wangu yu hai
Ukienda kwenye miti anaitwa mti wa uzima
Mtetezi wangu yu hai
Ukienda kwenye maji anaitwa maji yaliyo hai
Mtetezi wangu yu hai
Wewe usiye na chakula Yesu anaitwa mkate wa uzima
Mtetezi wangu yu hai
Ukifika kwenye miamba anaitwa mwamba imara
Mtetezi wangu yu hai
Hata kwa watawala Yesu anaitwa Mfalme wa Wafalme
Mtetezi wangu yu hai
Mtetezi mtetezi wetu
Mtetezi wangu yu hai
Mtetezi wa maisha mtetezi wa kanisa
Mtetezi wangu yu hai (tuimbe)


Chorus


Mtetezi wangu Yesu anaishi leo
Mtetezi wangu yu hai
(x4)


Verse 2


Ukienda kwa wagonjwa anaitwa mponyaji
Mtetezi wangu yu hai
Hata wenye huzuni anaitwa mfariji
Mtetezi wangu yu hai
Uliyesongwa na shida yeye anaitwa msaada
Mtetezi wangu yu hai
Mjane usifadhaike Yesu anaitwa mume wa wajane
Mtetezi wangu yu hai
Yatima usilie yeye anaitwa Baba wa yatima
Mtetezi wangu yu hai
Kwenye biashara yako muite Yesu mshauri wa ajabu
Mtetezi wangu yu hai


Bridge


Mtetezi mtetezi Yesu
Mtetezi wetu yu hai
Mtetezi mtetezi Yesu
Mtetezi wetu yu hai (tuimbe)


Chorus


Mtetezi wangu Yesu anaishi leo
Mtetezi wangu yu hai
(x4)


Verse 3


Ewe mama usilie na ndoa yako mama
Mtetezi wako yu hai
Ewe baba usilie umefukuzwa kazi
Mtetezi wako yu hai
Kijana usilie mchumba amekukataa
Mtetezi wangu yu hai
Watumishi wa Mungu msifadhaike
Mtetezi wetu yu hai
Fanyeni kazi ya Mungu huyo aliyewaita
Mtetezi wetu yu hai
Hata kama mkibezwa, mkisemwa na kutukanwa
Mtetezi wetu yu hai (tuimbe)


Outro


Mtetezi wangu Yesu anaishi leo
Mtetezi wangu yu hai
(x8)


Credits & Song Information

Performed By
Christina Shusho
Community reviewed · Apple Music
Release Date
March 21, 2008
Community reviewed · Apple Music

Add song information · Add a supporting source

Video

Meaning & Inspiration

“Mtetezi Wangu” is a worship declaration centered on Jesus as the singer’s defender. Its call-and-response pattern keeps returning to that assurance, while the verses deepen the song’s tone of trust and dependence.