Sifa Lyrics

Pokea Sifa (Uhimidiwe) by Kidum cover art

Kidum - Pokea Sifa (Uhimidiwe) Lyrics

Artist:
Kidum

Lyrics

Oh oh oh, ah ah ah
Oh oh oh, ah ah ah


Nimekuja hapa mbele zako bwana
Kukupee sifa
Ninajua kwamba niko mwenye dhambi
Naomba unisamehe


Utukufu wako hauna kifani
Huruma na upendo wako kwa walimwengu
Hulinganishwi na chochote 
Baba wetu


Unapea mvua, wabaya na wazuri
Na mwangaza wa jua kwa wabaya na wazuri
Hubagui baba


Baba Baba pokea sifa, uhimidiwe
Baba Baba pokea sifa, uabudiwe


Watu wengi duniani wamekata tamaa
Wanadhani wakija kwako utawafukuza
Wanasema wewe ni Mungu wa walio wema tu
Wanasema wewe ni Mungu wa matajiri tu
Wanasema wewe ni Mungu wa mataifa yenye nguvu
Lakini


Kumbe wamekosa mwenye kuwapa ukweli
Kumbe hawajui wewe ni mwenye huruma
Kumbe wamekosa mwenye kuwapa ukweli
Kumbe hawajui wewe ni mwenye huruma


Niko hapa kutoa ushuhuda 
Na kukupa sifa zako baba


Baba Baba pokea sifa, uhimidiwe
Baba Baba pokea sifa, uabudiwe
Baba Baba pokea sifa, uhimidiwe
Baba Baba pokea sifa, uabudiwe


Kumbe wamekosa mwenye kuwapa ukweli
Kumbe hawajui wewe ni mwenye huruma
Kumbe wamekosa mwenye kuwapa ukweli
Kumbe hawajui wewe ni mwenye huruma


Baba Baba pokea sifa, uhimidiwe
Baba Baba pokea sifa, uabudiwe
Baba Baba pokea sifa, uhimidiwe
Baba Baba pokea sifa, uabudiwe


Video