Eeeh Bwana utete nao wanao teta nami
Upigane nao wanao pigana nami
Eeeh Bwana utete nao wanao teta nami
Upigane nao wanao pigana nami
Ushike ngao na kinga usimame nami unisaidie
Vuta we mkuki uwapige wanaonifuatia
Uambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako
Wananiuliza mambo nisiyoyajua
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami
Pigana nao wanaopigana nami
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami
Pigana nao wanaopigana nami
Wahaibishwe wafedheheshwe
Warudishwe nyuma wanaotafuta nafsi yangu
Wafadhaishwe wawe kama makapi
Mbele yao pepo malaika wa Bwana waangushe chini
Wananilipa mabaya badala ya mema
Kutwa kucha waniwinda ili niteseke ee
Niko ndani yako niweke eeh Mungu
Ubavuni mwako nikumbatie Jehovah wangu
Mkononi mwako niweke eeh Mungu
Ubavuni mwako nikumbatie Jehovah wangu
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami
Upigane nao wanaopigana nami
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami
Upigane nao wanaopigana nami
Njia yao iwe giza na utelezi
Malaika wa Bwana akiwafuatia
Uharibifu uwapate kwa ghafla
Wa uharibifu aanguke ndani yake
Mimi bure wasinisemange bure wasinibonge
Na uovu wao aloficha umnase mwenyewe
Bila sababu amenichimbia shimo nafsi yangu
Mifupa yangu yote itasema
"Bwana ni nani aliye kama wewe?"
Na nafsi yangu itamfurahia Bwana
Wapendeza Bwana wapendeza eeh Bwana wapendeza
Katika hili najua utatenda
Nitetee Bwana nitetee eeh Bwana nitetee
Katika hili najua utatenda