Warumi 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 5 (Swahili) Romans 5 (English)

Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, Warumi 5:1

Being therefore justified by faith, we have peace with God through our Lord Jesus Christ;

ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Warumi 5:2

through whom we also have our access by faith into this grace in which we stand. We rejoice in hope of the glory of God.

Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; Warumi 5:3

Not only this, but we also rejoice in our sufferings, knowing that suffering works perseverance;

na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; Warumi 5:4

and perseverance, proven character; and proven character, hope:

na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Warumi 5:5

and hope doesn't disappoint us, because God's love has been poured out into our hearts through the Holy Spirit who was given to us.

Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Warumi 5:6

For while we were yet weak, at the right time Christ died for the ungodly.

Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Warumi 5:7

For one will hardly die for a righteous man. Yet perhaps for a righteous person someone would even dare to die.

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Warumi 5:8

But God commends his own love toward us, in that while we were yet sinners, Christ died for us.

Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Warumi 5:9

Much more then, being now justified by his blood, we will be saved from God's wrath through him.

Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Warumi 5:10

For if, while we were enemies, we were reconciled to God through the death of his Son, much more, being reconciled, we will be saved by his life.

Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho. Warumi 5:11

Not only so, but we also rejoice in God through our Lord Jesus Christ, through whom we have now received the reconciliation.

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; Warumi 5:12

Therefore, as sin entered into the world through one man, and death through sin; and so death passed to all men, because all sinned.

maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; Warumi 5:13

For until the law, sin was in the world; but sin is not charged when there is no law.

walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Warumi 5:14

Nevertheless death reigned from Adam until Moses, even over those whose sins weren't like Adam's disobedience, who is a foreshadowing of him who was to come.

Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Warumi 5:15

But the free gift isn't like the trespass. For if by the trespass of the one the many died, much more did the grace of God, and the gift by the grace of the one man, Jesus Christ, abound to the many.

Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. Warumi 5:16

The gift is not as through one who sinned: for the judgment came by one to condemnation, but the free gift came of many trespasses to justification.

Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Warumi 5:17

For if by the trespass of the one, death reigned through the one; so much more will those who receive the abundance of grace and of the gift of righteousness reign in life through the one, Jesus Christ.

Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. Warumi 5:18

So then as through one trespass, all men were condemned; even so through one act of righteousness, all men were justified to life.

Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. Warumi 5:19

For as through the one man's disobedience many were made sinners, even so through the obedience of the one will many be made righteous.

Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; Warumi 5:20

The law came in besides, that the trespass might abound; but where sin abounded, grace did abound more exceedingly;

ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Warumi 5:21

that as sin reigned in death, even so might grace reign through righteousness to eternal life through Jesus Christ our Lord.