Warumi 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 14 (Swahili) Romans 14 (English)

Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake. Warumi 14:1

Now receive one who is weak in faith, but not for disputes over opinions.

Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. Warumi 14:2

One man has faith to eat all things, but he who is weak eats only vegetables.

Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali. Warumi 14:3

Don't let him who eats despise him who doesn't eat. Don't let him who doesn't eat judge him who eats, for God has received him.

Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha. Warumi 14:4

Who are you who judge another's servant? To his own lord he stands or falls. Yes, he will be made to stand, for God has power to make him stand.

Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Warumi 14:5

One man esteems one day as more important. Another esteems every day alike. Let each man be fully assured in his own mind.

Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu. Warumi 14:6

He who observes the day, observes it to the Lord; and he who does not observe the day, to the Lord he does not observe it. He who eats, eats to the Lord, for he gives God thanks. He who doesn't eat, to the Lord he doesn't eat, and gives God thanks.

Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. Warumi 14:7

For none of us lives to himself, and none dies to himself.

Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. Warumi 14:8

For if we live, we live to the Lord. Or if we die, we die to the Lord. If therefore we live or die, we are the Lord's.

Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia. Warumi 14:9

For to this end Christ died, rose, and lived again, that he might be Lord of both the dead and the living.

Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Warumi 14:10

But you, why do you judge your brother? Or you again, why do you despise your brother? For we will all stand before the judgment seat of Christ.

Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu. Warumi 14:11

For it is written, "'As I live,' says the Lord, 'to me every knee will bow. Every tongue will confess to God.'"

Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. Warumi 14:12

So then each one of us will give account of himself to God.

Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. Warumi 14:13

Therefore let's not judge one another any more, but judge this rather, that no man put a stumbling block in his brother's way, or an occasion for falling.

Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. Warumi 14:14

I know, and am persuaded in the Lord Jesus, that nothing is unclean of itself; except that to him who considers anything to be unclean, to him it is unclean.

Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. Warumi 14:15

Yet if because of food your brother is grieved, you walk no longer in love. Don't destroy with your food him for whom Christ died.

Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. Warumi 14:16

Then don't let your good be slandered,

Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Warumi 14:17

for the Kingdom of God is not eating and drinking, but righteousness, peace, and joy in the Holy Spirit.

Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. Warumi 14:18

For he who serves Christ in these things is acceptable to God and approved by men.

Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. Warumi 14:19

So then, let us follow after things which make for peace, and things by which we may build one another up.

Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. Warumi 14:20

Don't overthrow God's work for food's sake. All things indeed are clean, however it is evil for that man who creates a stumbling block by eating.

Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa. Warumi 14:21

It is good to not eat meat, drink wine, nor do anything by which your brother stumbles, is offended, or is made weak.

Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali. Warumi 14:22

Do you have faith? Have it to yourself before God. Happy is he who doesn't judge himself in that which he approves.

Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi. Warumi 14:23

But he who doubts is condemned if he eats, because it isn't of faith; and whatever is not of faith is sin. (14:24) Now to him who is able to establish you according to my Gospel and the preaching of Jesus Christ, according to the revelation of the mystery which has been kept secret through long ages, (14:25) but now is revealed, and by the Scriptures of the prophets, according to the commandment of the eternal God, is made known for obedience of faith to all the nations; (14:26) to the only wise God, through Jesus Christ, to whom be the glory forever! Amen.{TR places verses 24-26 after Romans 16:24 as verses 25-27.}