Warumi 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 2 (Swahili) Romans 2 (English)

Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. Warumi 2:1

Therefore you are without excuse, O man, whoever you are who judge. For in that which you judge another, you condemn yourself. For you who judge practice the same things.

Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Warumi 2:2

We know that the judgment of God is according to truth against those who practice such things.

Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Warumi 2:3

Do you think this, O man who judges those who practice such things, and do the same, that you will escape the judgment of God?

Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Warumi 2:4

Or do you despise the riches of his goodness, forbearance, and patience, not knowing that the goodness of God leads you to repentance?

Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, Warumi 2:5

But according to your hardness and unrepentant heart you are treasuring up for yourself wrath in the day of wrath, revelation, and of the righteous judgment of God;

atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; Warumi 2:6

who "will pay back to everyone according to their works:"

wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; Warumi 2:7

to those who by patience in well-doing seek for glory and honor and incorruptibility, eternal life;

na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; Warumi 2:8

but to those who are self-seeking, and don't obey the truth, but obey unrighteousness, will be wrath and indignation,

dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; Warumi 2:9

oppression and anguish, on every soul of man who works evil, on the Jew first, and also on the Greek.

bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; Warumi 2:10

But glory and honor and peace to every man who works good, to the Jew first, and also to the Greek.

kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. Warumi 2:11

For there is no partiality with God.

Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. Warumi 2:12

For as many as have sinned without law will also perish without the law. As many as have sinned under the law will be judged by the law.

Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. Warumi 2:13

For it isn't the hearers of the law who are righteous before God, but the doers of the law will be justified

Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Warumi 2:14

(for when Gentiles who don't have the law do by nature the things of the law, these, not having the law, are a law to themselves,

Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; Warumi 2:15

in that they show the work of the law written in their hearts, their conscience testifying with them, and their thoughts among themselves accusing or else excusing them)

katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu. Warumi 2:16

in the day when God will judge the secrets of men, according to my Gospel, by Jesus Christ.

Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu, Warumi 2:17

Indeed you bear the name of a Jew, and rest on the law, and glory in God,

na kuyajua mapenzi yake, na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati, Warumi 2:18

and know his will, and approve the things that are excellent, being instructed out of the law,

na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani, Warumi 2:19

and are confident that you yourself are a guide of the blind, a light to those who are in darkness,

mkufunzi wa wajinga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati; Warumi 2:20

a corrector of the foolish, a teacher of babies, having in the law the form of knowledge and of the truth.

basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? Warumi 2:21

You therefore who teach another, don't you teach yourself? You who preach that a man shouldn't steal, do you steal?

Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu? Warumi 2:22

You who say a man shouldn't commit adultery, do you commit adultery? You who abhor idols, do you rob temples?

Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? Warumi 2:23

You who glory in the law, through your disobedience of the law do you dishonor God?

Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa. Warumi 2:24

For "the name of God is blasphemed among the Gentiles because of you," just as it is written.

Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. Warumi 2:25

For circumcision indeed profits, if you are a doer of the law, but if you are a transgressor of the law, your circumcision has become uncircumcision.

Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa? Warumi 2:26

If therefore the uncircumcised keep the ordinances of the law, won't his uncircumcision be accounted as circumcision?

Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati? Warumi 2:27

Won't the uncircumcision which is by nature, if it fulfills the law, judge you, who with the letter and circumcision are a transgressor of the law?

Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; Warumi 2:28

For he is not a Jew who is one outwardly, neither is that circumcision which is outward in the flesh;

bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu. Warumi 2:29

but he is a Jew who is one inwardly, and circumcision is that of the heart, in the spirit not in the letter; whose praise is not from men, but from God.