Warumi 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 15 (Swahili) Romans 15 (English)

Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. Warumi 15:1

Now we who are strong ought to bear the weaknesses of the weak, and not to please ourselves.

Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe. Warumi 15:2

Let each one of us please his neighbor for that which is good, to be building him up.

Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi. Warumi 15:3

For even Christ didn't please himself. But, as it is written, "The reproaches of those who reproached you fell on me."

Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. Warumi 15:4

For whatever things were written before were written for our learning, that through patience and through encouragement of the Scriptures we might have hope.

Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; Warumi 15:5

Now the God of patience and of encouragement grant you to be of the same mind one with another according to Christ Jesus,

ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Warumi 15:6

that with one accord you may with one mouth glorify the God and Father of our Lord Jesus Christ.

Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe. Warumi 15:7

Therefore receive one another, even as Christ also received you,{TR reads "us" instead of "you"} to the glory of God.

Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu; Warumi 15:8

Now I say that Christ has been made a minister of the circumcision for the truth of God, that he might confirm the promises given to the fathers,

tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako. Warumi 15:9

and that the Gentiles might glorify God for his mercy. As it is written, "Therefore will I give praise to you among the Gentiles, And sing to your name."

Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake. Warumi 15:10

Again he says, "Rejoice, you Gentiles, with his people."

Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini. Warumi 15:11

Again, "Praise the Lord, all you Gentiles! Let all the peoples praise him."

Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini. Warumi 15:12

Again, Isaiah says, "There will be the root of Jesse, He who arises to rule over the Gentiles; On him will the Gentiles hope."

Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. Warumi 15:13

Now may the God of hope fill you with all joy and peace in believing, that you may abound in hope, in the power of the Holy Spirit.

Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana. Warumi 15:14

I myself am also persuaded about you, my brothers{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}, that you yourselves are full of goodness, filled with all knowledge, able also to admonish others.

Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu, Warumi 15:15

But I write the more boldly to you in part, as reminding you, because of the grace that was given to me by God,

ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu. Warumi 15:16

that I should be a servant of Christ Jesus to the Gentiles, ministering as a priest the Gospel of God, that the offering up of the Gentiles might be made acceptable, sanctified by the Holy Spirit.

Basi, nina sababu ya kuona fahari katika Kristo Yesu mbele za Mungu. Warumi 15:17

I have therefore my boasting in Christ Jesus in things pertaining to God.

Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, Warumi 15:18

For I will not dare to speak of any things except those which Christ worked through me, for the obedience of the Gentiles, by word and deed,

kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu; Warumi 15:19

in the power of signs and wonders, in the power of God's Spirit; so that from Jerusalem, and around as far as to Illyricum, I have fully preached the Gospel of Christ;

kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine; Warumi 15:20

yes, making it my aim to preach the Gospel, not where Christ was already named, that I might not build on another's foundation.

bali kama ilivyoandikwa, Wale wasiohubiriwa habari zake wataona, Na wale wasiojasikia watafahamu. Warumi 15:21

But, as it is written, "They will see, to whom no news of him came. They who haven't heard will understand."

Ndiyo sababu nalizuiwa mara nyingi nisije kwenu. Warumi 15:22

Therefore also I was hindered these many times from coming to you,

Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mingi nina shauku kuja kwenu; Warumi 15:23

but now, no longer having any place in these regions, and having these many years a longing to come to you,

wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana nataraji kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kusafirishwa nanyi, moyo wangu ushibe kwenu kidogo. Warumi 15:24

whenever I journey to Spain, I will come to you. For I hope to see you on my journey, and to be helped on my way there by you, if first I may enjoy your company for a while.

Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu; Warumi 15:25

But now, I say, I am going to Jerusalem, serving the saints.

maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini. Warumi 15:26

For it has been the good pleasure of Macedonia and Achaia to make a certain contribution for the poor among the saints who are at Jerusalem.

Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili. Warumi 15:27

Yes, it has been their good pleasure, and they are their debtors. For if the Gentiles have been made partakers of their spiritual things, they owe it to them also to serve them in fleshly things.

Basi nikiisha kuimaliza kazi hiyo, na kuwatilia muhuri tunda hilo, nitapitia kwenu, kwenda Spania. Warumi 15:28

When therefore I have accomplished this, and have sealed to them this fruit, I will go on by way of you to Spain.

Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa baraka ya Kristo. Warumi 15:29

I know that, when I come to you, I will come in the fullness of the blessing of the Gospel of Christ.

Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu; Warumi 15:30

Now I beg you, brothers, by our Lord Jesus Christ, and by the love of the Spirit, that you strive together with me in your prayers to God for me,

kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu; Warumi 15:31

that I may be delivered from those who are disobedient in Judea, and that my service which I have for Jerusalem may be acceptable to the saints;

nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi. Warumi 15:32

that I may come to you in joy through the will of God, and together with you, find rest.

Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina. Warumi 15:33

Now the God of peace be with you all. Amen.