Warumi 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 4 (Swahili) Romans 4 (English)

Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? Warumi 4:1

What then will we say that Abraham, our forefather, has found according to the flesh?

Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. Warumi 4:2

For if Abraham was justified by works, he has something to boast about, but not toward God.

Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki. Warumi 4:3

For what does the Scripture say? "Abraham believed God, and it was accounted to him for righteousness."

Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. Warumi 4:4

Now to him who works, the reward is not counted as grace, but as debt.

Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. Warumi 4:5

But to him who doesn't work, but believes in him who justifies the ungodly, his faith is accounted for righteousness.

Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo, Warumi 4:6

Even as David also pronounces blessing on the man to whom God counts righteousness apart from works,

Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao. Warumi 4:7

"Blessed are they whose iniquities are forgiven, Whose sins are covered.

Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi. Warumi 4:8

Blessed is the man whom the Lord will by no means charge with sin."

Basi je! Uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki. Warumi 4:9

Is this blessing then pronounced on the circumcised, or on the uncircumcised also? For we say that faith was accounted to Abraham for righteousness.

Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa. Warumi 4:10

How then was it counted? When he was in circumcision, or in uncircumcision? Not in circumcision, but in uncircumcision.

Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki; Warumi 4:11

He received the sign of circumcision, a seal of the righteousness of the faith which he had while he was in uncircumcision, that he might be the father of all those who believe, though they be in uncircumcision, that righteousness might also be accounted to them.

tena awe baba ya kutahiriwa, kwa wale ambao si waliotahiriwa tu, bali pia wanazifuata nyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa. Warumi 4:12

The father of circumcision to those who not only are of the circumcision, but who also walk in the steps of that faith of our father Abraham, which he had in uncircumcision.

Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani. Warumi 4:13

For the promise to Abraham and to his seed that he should be heir of the world wasn't through the law, but through the righteousness of faith.

Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika. Warumi 4:14

For if those who are of the law are heirs, faith is made void, and the promise is made of no effect.

Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa. Warumi 4:15

For the law works wrath, for where there is no law, neither is there disobedience.

Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; Warumi 4:16

For this cause it is of faith, that it may be according to grace, to the end that the promise may be sure to all the seed, not to that only which is of the law, but to that also which is of the faith of Abraham, who is the father of us all.

(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. Warumi 4:17

As it is written, "I have made you a father of many nations." This is in the presence of him whom he believed: God, who gives life to the dead, and calls the things that are not, as though they were.

Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Warumi 4:18

Who in hope believed against hope, to the end that he might become a father of many nations, according to that which had been spoken, "So will your seed be."

Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Warumi 4:19

Without being weakened in faith, he didn't consider his own body, already having been worn out, (he being about a hundred years old), and the deadness of Sarah's womb.

Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; Warumi 4:20

Yet, looking to the promise of God, he didn't waver through unbelief, but grew strong through faith, giving glory to God,

huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Warumi 4:21

and being fully assured that what he had promised, he was able also to perform.

Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki. Warumi 4:22

Therefore it also was "reckoned to him for righteousness."

Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; Warumi 4:23

Now it was not written that it was accounted to him for his sake alone,

bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; Warumi 4:24

but for our sake also, to whom it will be accounted, who believe in him who raised Jesus, our Lord, from the dead,

ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki. Warumi 4:25

who was delivered up for our trespasses, and was raised for our justification.