Warumi 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 11 (Swahili) Romans 11 (English)

Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini. Warumi 11:1

I ask then, Did God reject his people? May it never be! For I also am an Israelite, a descendant of Abraham, of the tribe of Benjamin.

Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu, Warumi 11:2

God didn't reject his people, which he foreknew. Or don't you know what the Scripture says about Elijah? How he pleads with God against Israel:

Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu. Warumi 11:3

"Lord, they have killed your prophets, they have broken down your altars; and I am left alone, and they seek my life."

Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali. Warumi 11:4

But how does God answer him? "I have reserved for myself seven thousand men, who have not bowed the knee to Baal."

Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Warumi 11:5

Even so then at this present time also there is a remnant according to the election of grace.

Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema. Warumi 11:6

And if by grace, then it is no longer of works; otherwise grace is no longer grace. But if it is of works, it is no longer grace; otherwise work is no longer work.

Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa uzito. Warumi 11:7

What then? That which Israel seeks for, that he didn't obtain, but the chosen ones obtained it, and the rest were hardened.

Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo. Warumi 11:8

According as it is written, "God gave them a spirit of stupor, eyes that they should not see, and ears that they should not hear, to this very day."

Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao; Warumi 11:9

David says, "Let their table be made a snare, and a trap, A stumbling block, and a retribution to them.

Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote. Warumi 11:10

Let their eyes be darkened, that they may not see. Bow down their back always."

Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu. Warumi 11:11

I ask then, did they stumble that they might fall? May it never be! But by their fall salvation has come to the Gentiles, to provoke them to jealousy.

Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao? Warumi 11:12

Now if their fall is the riches of the world, and their loss the riches of the Gentiles; how much more their fullness?

Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu, Warumi 11:13

For I speak to you who are Gentiles. Since then as I am an apostle to Gentiles, I glorify my ministry;

nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao. Warumi 11:14

if by any means I may provoke to jealousy those who are my flesh, and may save some of them.

Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa? Warumi 11:15

For if the rejection of them is the reconciling of the world, what would their acceptance be, but life from the dead?

Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika. Warumi 11:16

If the first fruit is holy, so is the lump. If the root is holy, so are the branches.

Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, Warumi 11:17

But if some of the branches were broken off, and you, being a wild olive, were grafted in among them, and became partaker with them of the root and of the richness of the olive tree;

usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe. Warumi 11:18

don't boast over the branches. But if you boast, it is not you who support the root, but the root supports you.

Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi. Warumi 11:19

You will say then, "Branches were broken off, that I might be grafted in."

Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope. Warumi 11:20

True; by their unbelief they were broken off, and you stand by your faith. Don't be conceited, but fear;

Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe. Warumi 11:21

for if God didn't spare the natural branches, neither will he spare you.

Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali. Warumi 11:22

See then the goodness and severity of God. Toward those who fell, severity; but toward you, goodness, if you continue in his goodness; otherwise you also will be cut off.

Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena. Warumi 11:23

They also, if they don't continue in their unbelief, will be grafted in, for God is able to graft them in again.

Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe? Warumi 11:24

For if you were cut out of that which is by nature a wild olive tree, and were grafted contrary to nature into a good olive tree, how much more will these, which are the natural branches, be grafted into their own olive tree?

Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. Warumi 11:25

For I don't desire, brothers,{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} to have you ignorant of this mystery, so that you won't be wise in your own conceits, that a partial hardening has happened to Israel, until the fullness of the Gentiles has come in,

Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. Warumi 11:26

and so all Israel will be saved. Even as it is written, "There will come out of Zion the Deliverer, And he will turn away ungodliness from Jacob.

Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. Warumi 11:27

This is my covenant to them, When I will take away their sins."

Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu. Warumi 11:28

Concerning the Gospel, they are enemies for your sake. But concerning the election, they are beloved for the fathers' sake.

Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. Warumi 11:29

For the gifts and the calling of God are irrevocable.

Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; Warumi 11:30

For as you in time past were disobedient to God, but now have obtained mercy by their disobedience,

kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. Warumi 11:31

even so these also have now been disobedient, that by the mercy shown to you they may also obtain mercy.

Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote. Warumi 11:32

For God has shut up all to disobedience, that he might have mercy on all.

Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Warumi 11:33

Oh the depth of the riches both of the wisdom and the knowledge of God! How unsearchable are his judgments, and his ways past tracing out!

Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Warumi 11:34

"For who has known the mind of the Lord? Or who has been his counselor?"

Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Warumi 11:35

"Or who has first given to him, And it will be repaid to him again?"

Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina. Warumi 11:36

For of him, and through him, and to him, are all things. To him be the glory for ever! Amen.