Mathayo 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 25 (Swahili) Matthew 25 (English)

Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Mathayo 25:1

"Then the Kingdom of Heaven will be like ten virgins, who took their lamps, and went out to meet the bridegroom.

Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Mathayo 25:2

Five of them were foolish, and five were wise.

Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; Mathayo 25:3

Those who were foolish, when they took their lamps, took no oil with them,

bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Mathayo 25:4

but the wise took oil in their vessels with their lamps.

Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Mathayo 25:5

Now while the bridegroom delayed, they all slumbered and slept.

Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mathayo 25:6

But at midnight there was a cry, 'Behold! The bridegroom is coming! Come out to meet him!'

Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Mathayo 25:7

Then all those virgins arose, and trimmed their lamps.

Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Mathayo 25:8

The foolish said to the wise, 'Give us some of your oil, for our lamps are going out.'

Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Mathayo 25:9

But the wise answered, saying, 'What if there isn't enough for us and you? You go rather to those who sell, and buy for yourselves.'

Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Mathayo 25:10

While they went away to buy, the bridegroom came, and those who were ready went in with him to the marriage feast, and the door was shut.

Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Mathayo 25:11

Afterward the other virgins also came, saying, 'Lord, Lord, open to us.'

Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. Mathayo 25:12

But he answered, 'Most assuredly I tell you, I don't know you.'

Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. Mathayo 25:13

Watch therefore, for you don't know the day nor the hour in which the Son of Man is coming.

Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Mathayo 25:14

"For it is like a man, going into another country, who called his own servants, and entrusted his goods to them.

Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mathayo 25:15

To one he gave five talents, to another two, to another one; to each according to his own ability. Then he went on his journey.

Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Mathayo 25:16

Immediately he who received the five talents went and traded with them, and made another five talents.

Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Mathayo 25:17

In like manner he also who got the two gained another two.

Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Mathayo 25:18

But he who received the one went away and dug in the earth, and hid his lord's money.

Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Mathayo 25:19

"Now after a long time the lord of those servants came, and reconciled accounts with them.

Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. Mathayo 25:20

He who received the five talents came and brought another five talents, saying, 'Lord, you delivered to me five talents. Behold, I have gained another five talents besides them.'

Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Mathayo 25:21

"His lord said to him, 'Well done, good and faithful servant. You have been faithful over a few things, I will set you over many things. Enter into the joy of your lord.'

Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Mathayo 25:22

"He also who got the two talents came and said, 'Lord, you delivered to me two talents. Behold, I have gained another two talents besides them.'

Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Mathayo 25:23

"His lord said to him, 'Well done, good and faithful servant. You have been faithful over a few things, I will set you over many things. Enter into the joy of your lord.'

Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; Mathayo 25:24

"He also who had received the one talent came and said, 'Lord, I knew you that you are a hard man, reaping where you did not sow, and gathering where you did not scatter.

basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Mathayo 25:25

I was afraid, and went away and hid your talent in the earth. Behold, you have what is yours.'

Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; Mathayo 25:26

"But his lord answered him, 'You wicked and slothful servant. You knew that I reap where I didn't sow, and gather where I didn't scatter.

basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Mathayo 25:27

You ought therefore to have deposited my money with the bankers, and at my coming I should have received back my own with interest.

Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Mathayo 25:28

Take away therefore the talent from him, and give it to him who has the ten talents.

Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. Mathayo 25:29

For to everyone who has will be given, and he will have abundance, but from him who has not, even that which he has will be taken away.

Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Mathayo 25:30

Throw out the unprofitable servant into the outer darkness, where there will be weeping and gnashing of teeth.'

Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; Mathayo 25:31

"But when the Son of Man comes in his glory, and all the holy angels with him, then he will sit on the throne of his glory.

na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; Mathayo 25:32

Before him all the nations will be gathered, and he will separate them one from another, as a shepherd separates the sheep from the goats.

atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Mathayo 25:33

He will set the sheep on his right hand, but the goats on the left.

Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; Mathayo 25:34

Then the King will tell those on his right hand, 'Come, blessed of my Father, inherit the Kingdom prepared for you from the foundation of the world;

kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; Mathayo 25:35

for I was hungry, and you gave me food to eat; I was thirsty, and you gave me drink; I was a stranger, and you took me in;

nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Mathayo 25:36

naked, and you clothed me; I was sick, and you visited me; I was in prison, and you came to me.'

Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Mathayo 25:37

"Then the righteous will answer him, saying, 'Lord, when did we see you hungry, and feed you; or thirsty, and give you a drink?

Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Mathayo 25:38

When did we see you as a stranger, and take you in; or naked, and clothe you?

Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Mathayo 25:39

When did we see you sick, or in prison, and come to you?'

Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Mathayo 25:40

"The King will answer them, 'Most assuredly I tell you, inasmuch as you did it to one of the least of these my brothers{The word for "brothers" here may be also correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}, you did it to me.'

Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; Mathayo 25:41

Then he will say also to those on the left hand, 'Depart from me, you cursed, into the eternal fire which is prepared for the devil and his angels;

kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; Mathayo 25:42

for I was hungry, and you didn't give me food to eat; I was thirsty, and you gave me no drink;

nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Mathayo 25:43

I was a stranger, and you didn't take me in; naked, and you didn't clothe me; sick, and in prison, and you didn't visit me.'

Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Mathayo 25:44

"Then they will also answer, saying, 'Lord, when did we see you hungry, or thirsty, or a stranger, or naked, or sick, or in prison, and didn't help you?'

Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Mathayo 25:45

"Then he will answer them, saying, 'Most assuredly I tell you, inasmuch as you didn't do it to one of the least of these, you didn't do it to me.'

Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. Mathayo 25:46

These will go away into eternal punishment, but the righteous into eternal life."