Mathayo 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 8 (Swahili) Matthew 8 (English)

Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Mathayo 8:1

When he came down from the mountain, great multitudes followed him.

Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. Mathayo 8:2

Behold, a leper came to him and worshiped him, saying, "Lord, if you want to, you can make me clean."

Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika. Mathayo 8:3

Jesus stretched out his hand, and touched him, saying, "I want to. Be made clean." Immediately his leprosy was cleansed.

Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao. Mathayo 8:4

Jesus said to him, "See that you tell nobody, but go, show yourself to the priest, and offer the gift that Moses commanded, as a testimony to them."

Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, Mathayo 8:5

When he came into Capernaum, a centurion came to him, asking him,

akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Mathayo 8:6

and saying, "Lord, my servant lies in the house paralyzed, grievously tormented."

Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. Mathayo 8:7

Jesus said to him, "I will come and heal him."

Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Mathayo 8:8

The centurion answered, "Lord, I'm not worthy for you to come under my roof. Just say the word, and my servant will be healed.

Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. Mathayo 8:9

For I am also a man under authority, having under myself soldiers. I tell this one, 'Go,' and he goes; and tell another, 'Come,' and he comes; and tell my servant, 'Do this,' and he does it."

Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli. Mathayo 8:10

When Jesus heard it, he marveled, and said to those who followed, "Most assuredly I tell you, I haven't found so great a faith, not even in Israel.

Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; Mathayo 8:11

I tell you that many will come from the east and the west, and will sit down with Abraham, Isaac, and Jacob in the Kingdom of Heaven,

bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Mathayo 8:12

but the children of the Kingdom will be thrown out into the outer darkness. There will be weeping and the gnashing of teeth."

Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile. Mathayo 8:13

Jesus said to the centurion, "Go your way. Let it be done for you as you have believed." His servant was healed in that hour.

Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Mathayo 8:14

When Jesus came into Peter's house, he saw his wife's mother lying sick with a fever.

Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia. Mathayo 8:15

He touched her hand, and the fever left her. She got up and served him.{TR reads "them" instead of "him"}

Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, Mathayo 8:16

When evening came, they brought to him many possessed with demons. He cast out the spirits with a word, and healed all who were sick;

ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. Mathayo 8:17

that it might be fulfilled which was spoken through Isaiah the prophet, saying: "He took our infirmities, and bore our diseases."

Naye Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng'ambo. Mathayo 8:18

Now when Jesus saw great multitudes around him, he gave the order to depart to the other side.

Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako. Mathayo 8:19

A scribe came, and said to him, "Teacher, I will follow you wherever you go."

Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. Mathayo 8:20

Jesus said to him, "The foxes have holes, and the birds of the sky have nests, but the Son of Man has nowhere to lay his head."

Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu. Mathayo 8:21

Another of his disciples said to him, "Lord, allow me first to go and bury my father."

Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao. Mathayo 8:22

But Jesus said to him, "Follow me, and leave the dead to bury their own dead."

Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Mathayo 8:23

When he got into a boat, his disciples followed him.

Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Mathayo 8:24

Behold, a great tempest arose in the sea, so much that the boat was covered with the waves, but he was asleep.

Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Mathayo 8:25

They came to him, and woke him up, saying, "Save us, Lord! We are dying!"

Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Mathayo 8:26

He said to them, "Why are you fearful, oh you of little faith?" Then he got up, rebuked the wind and the sea, and there was a great calm.

Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii? Mathayo 8:27

The men marveled, saying, "What kind of man is this, that even the wind and the sea obey him?"

Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Mathayo 8:28

When he came to the other side, into the country of the Gergesenes, two people possessed by demons met him there, coming out of the tombs, exceedingly fierce, so that nobody could pass by that way.

Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? Mathayo 8:29

Behold, they cried out, saying, "What do we have to do with you, Jesus, Son of God? Have you come here to torment us before the time?"

Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. Mathayo 8:30

Now there was a herd of many pigs feeding far away from them.

Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. Mathayo 8:31

The demons begged him, saying, "If you cast us out, permit us to go away into the herd of pigs."

Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini. Mathayo 8:32

He said to them, "Go!" They came out, and went into the herd of pigs: and behold, the whole herd of pigs rushed down the cliff into the sea, and died in the water.

Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia. Mathayo 8:33

Those who fed them fled, and went away into the city, and told everything, including what happened to those who were possessed with demons.

Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao. Mathayo 8:34

Behold, all the city came out to meet Jesus. When they saw him, they begged that he would depart from their borders.