Mathayo 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 21 (Swahili) Matthew 21 (English)

Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia, Mathayo 21:1

When they drew near to Jerusalem, and came to Bethsphage,{TR reads "Bethphage" instead of "Bethsphage"} to the Mount of Olives, then Jesus sent two disciples,

Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee. Mathayo 21:2

saying to them, "Go into the village that is opposite you, and immediately you will find a donkey tied, and a colt with her. Untie them, and bring them to me.

Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka. Mathayo 21:3

If anyone says anything to you, you shall say, 'The Lord needs them,' and immediately he will send them."

Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Mathayo 21:4

All this was done, that it might be fulfilled which was spoken through the prophet, saying,

Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda. Mathayo 21:5

"Tell the daughter of Zion, Behold, your King comes to you, Humble, and riding on a donkey, On a colt, the foal of a donkey."

Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, Mathayo 21:6

The disciples went, and did just as Jesus commanded them,

wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake. Mathayo 21:7

and brought the donkey and the colt, and laid their clothes on them; and he sat on them.

Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. Mathayo 21:8

A very great multitude spread their clothes on the road. Others cut branches from the trees, and spread them on the road.

Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni. Mathayo 21:9

The multitudes who went before him, and who followed kept shouting, "Hosanna to the son of David! Blessed is he who comes in the name of the Lord! Hosanna in the highest!"

Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Mathayo 21:10

When he had come into Jerusalem, all the city was stirred up, saying, "Who is this?"

Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya. Mathayo 21:11

The multitudes said, "This is the prophet, Jesus, from Nazareth of Galilee."

Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; Mathayo 21:12

Jesus entered into the temple of God, and drove out all of those who sold and bought in the temple, and overthrew the money-changers' tables and the seats of those who sold the doves.

akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. Mathayo 21:13

He said to them, "It is written, 'My house shall be called a house of prayer,' but you have made it a den of robbers!"

Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya. Mathayo 21:14

The blind and the lame came to him in the temple, and he healed them.

Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika, Mathayo 21:15

But when the chief priests and the scribes saw the wonderful things that he did, and the children who were crying in the temple and saying, "Hosanna to the son of David!" they were indignant,

wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa? Mathayo 21:16

and said to him, "Do you hear what these are saying?" Jesus said to them, "Yes. Did you never read, 'Out of the mouth of babes and nursing babies you have perfected praise?'"

Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko. Mathayo 21:17

He left them, and went out of the city to Bethany, and lodged there.

Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Mathayo 21:18

Now in the morning, as he returned to the city, he was hungry.

Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. Mathayo 21:19

Seeing a fig tree by the road, he came to it, and found nothing on it but leaves. He said to it, "Let there be no fruit from you forever!" Immediately the fig tree withered away.

Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara? Mathayo 21:20

When the disciples saw it, they marveled, saying, "How did the fig tree immediately wither away?"

Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Mathayo 21:21

Jesus answered them, "Most assuredly I tell you, if you have faith, and don't doubt, you will not only do what is done to the fig tree, but even if you told this mountain, 'Be taken up and cast into the sea,' it would be done.

Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. Mathayo 21:22

All things, whatever you ask in prayer, believing, you will receive."

Hata alipokwisha kuingia hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii? Mathayo 21:23

When he had come into the temple, the chief priests and the elders of the people came to him as he was teaching, and said, "By what authority do you do these things? Who gave you this authority?"

Yesu akajibu akawaambia, Na mimi nitawauliza neno moja; ambalo mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa amri gani ninatenda haya. Mathayo 21:24

Jesus answered them, "I also will ask you one question, which if you tell me, I likewise will tell you by what authority I do these things.

Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mbona basi hamkumwamini? Mathayo 21:25

The baptism of John, where was it from? From heaven or from men?" They reasoned with themselves, saying, "If we say, 'From heaven,' he will ask us, 'Why then did you not believe him?'

Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii. Mathayo 21:26

But if we say, 'From men,' we fear the multitude, for all hold John as a prophet."

Wakamjibu Yesu wakasema, Hatujui. Naye akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa amri gani ninatenda haya. Mathayo 21:27

They answered Jesus, and said, "We don't know." He also said to them, "Neither will I tell you by what authority I do these things.

Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Mathayo 21:28

But what do you think? A man had two sons, and he came to the first, and said, 'Son, go work today in my vineyard.'

Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. Mathayo 21:29

He answered, 'I will not,' but afterward he changed his mind, and went.

Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Mathayo 21:30

He came to the second, and said the same thing. He answered, 'I go, sir,' but he didn't go.

Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Mathayo 21:31

Which of the two did the will of his father?" They said to him, "The first." Jesus said to them, "Most assuredly I tell you that the tax collectors and the prostitutes are entering into the Kingdom of God before you.

Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini. Mathayo 21:32

For John came to you in the way of righteousness, and you didn't believe him, but the tax collectors and the prostitutes believed him. When you saw it, you didn't even repent afterward, that you might believe him.

Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Mathayo 21:33

"Hear another parable. There was a man who was a master of a household, who planted a vineyard, set a hedge about it, dug a winepress in it, built a tower, leased it out to farmers, and went into another country.

Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Mathayo 21:34

When the season for the fruit drew near, he sent his servants to the farmers, to receive his fruit.

Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Mathayo 21:35

The farmers took his servants, beat one, killed another, and stoned another.

Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mathayo 21:36

Again, he sent other servants more than the first: and they treated them the same way.

Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Mathayo 21:37

But afterward he sent to them his son, saying, 'They will respect my son.'

Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Mathayo 21:38

But the farmers, when they saw the son, said among themselves, 'This is the heir. Come, let's kill him, and seize his inheritance.'

Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Mathayo 21:39

So they took him, and threw him out of the vineyard, and killed him.

Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Mathayo 21:40

When therefore the lord of the vineyard comes, what will he do to those farmers?"

Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Mathayo 21:41

They told him, "He will miserably destroy those miserable men, and will lease out the vineyard to other farmers, who will give him the fruit in its season."

Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Mathayo 21:42

Jesus said to them, "Did you never read in the Scriptures, 'The stone which the builders rejected, The same was made the head of the corner. This was from the Lord. It is marvelous in our eyes?'

Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Mathayo 21:43

"Therefore I tell you, the Kingdom of God will be taken away from you, and will be given to a nation bringing forth its fruits.

Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki. Mathayo 21:44

He who falls on this stone will be broken to pieces, but on whoever it will fall, it will scatter him as dust."

Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao. Mathayo 21:45

When the chief priests and the Pharisees heard his parables, they perceived that he spoke about them.

Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.

Mathayo 21:46

When they sought to seize him, they feared the multitudes, because they considered him to be a prophet.