Mathayo 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 17 (Swahili) Matthew 17 (English)

Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; Mathayo 17:1

After six days, Jesus took with him Peter, James, and John his brother, and brought them up into a high mountain by themselves.

akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Mathayo 17:2

He was transfigured before them. His face shone like the sun, and his garments became as white as the light.

Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. Mathayo 17:3

Behold, Moses and Elijah appeared to them talking with him.

Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Mathayo 17:4

Peter answered, and said to Jesus, "Lord, it is good for us to be here. If you want, let's make three tents here: one for you, one for Moses, and one for Elijah."

Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Mathayo 17:5

While he was still speaking, behold, a bright cloud overshadowed them. Behold, a voice came out of the cloud, saying, "This is my beloved Son, in whom I am well pleased. Listen to him."

Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana. Mathayo 17:6

When the disciples heard it, they fell on their faces, and were very afraid.

Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. Mathayo 17:7

Jesus came and touched them and said, "Get up, and don't be afraid."

Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake. Mathayo 17:8

Lifting up their eyes, they saw no one, except Jesus alone.

Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. Mathayo 17:9

As they were coming down from the mountain, Jesus commanded them, saying, "Don't tell anyone what you saw, until the Son of Man has risen from the dead."

Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? Mathayo 17:10

His disciples asked him, saying, "Then why do the scribes say that Elijah must come first?"

Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, Mathayo 17:11

Jesus answered them, "Elijah indeed comes first, and will restore all things,

ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. Mathayo 17:12

but I tell you that Elijah has come already, and they didn't recognize him, but did to him whatever they wanted to. Even so the Son of Man will also suffer by them."

Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji. Mathayo 17:13

Then the disciples understood that he spoke to them of John the Baptizer.

Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, Mathayo 17:14

When they came to the multitude, a man came to him, kneeling down to him, saying,

Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Mathayo 17:15

"Lord, have mercy on my son, for he is epileptic, and suffers grievously; for he often falls into the fire, and often into the water.

Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. Mathayo 17:16

So I brought him to your disciples, and they could not cure him."

Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Mathayo 17:17

Jesus answered, "Faithless and perverse generation! How long will I be with you? How long will I bear with you? Bring him here to me."

Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. Mathayo 17:18

Jesus rebuked him, the demon went out of him, and the boy was cured from that hour.

Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Mathayo 17:19

Then the disciples came to Jesus privately, and said, "Why weren't we able to cast it out?"

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Mathayo 17:20

He said to them, "Because of your unbelief. For most assuredly I tell you, if you have faith as a grain of mustard seed, you will tell this mountain, 'Move from here to there,' and it will move; and nothing will be impossible for you.

[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] Mathayo 17:21

But this kind doesn't go out except by prayer and fasting."

Nao walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. Mathayo 17:22

While they were staying in Galilee, Jesus said to them, "The Son of Man is about to be delivered up into the hands of men,

Wakasikitika sana. Mathayo 17:23

and they will kill him, and the third day he will be raised up." They were exceedingly sorry.

Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa. Mathayo 17:24

When they had come to Capernaum, those who collected the didrachma coins{A didrachma is a Greek silver coin worth 2 drachmas, about as much as 2 Roman denarii, or about 2 days wages. It was commonly used to pay the half-shekel temple tax, because 2 drachmas were worth one half shekel of silver.} came to Peter, and said, "Doesn't your teacher pay the didrachma?"

Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? Mathayo 17:25

He said, "Yes." When he came into the house, Jesus anticipated him, saying, "What do you think, Simon? From whom do the kings of the earth receive toll or tribute? From their children, or from strangers?"

Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. Mathayo 17:26

Peter said to him, "From strangers." Jesus said to him, "Therefore the children are exempt.

Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako. Mathayo 17:27

But, lest we cause them to stumble, go to the sea, and cast a hook, and take up the first fish that comes up. When you have opened its mouth, you will find a stater coin.{A stater is a silver coin equivalent to four Attic or two Alexandrian drachmas, or a Jewish shekel: just exactly enough to cover the half-shekel Temple Tax for two people.} Take that, and give it to them for me and you."