Mathayo 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 2 (Swahili) Matthew 2 (English)

Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Mathayo 2:1

Now when Jesus was born in Bethlehem of Judea in the days of Herod the king, behold, wise men{The word for "wise men" (magoi) can also mean teachers, priests, physicians, astrologers, seers, interpreters of dreams, or sorcerers.} from the east came to Jerusalem, saying,

Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. Mathayo 2:2

"Where is he who is born King of the Jews? For we saw his star in the east, and have come to worship him."

Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Mathayo 2:3

When Herod the king heard it, he was troubled, and all Jerusalem with him.

Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? Mathayo 2:4

Gathering together all the chief priests and scribes of the people, he asked them where the Christ would be born.

Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Mathayo 2:5

They said to him, "In Bethlehem of Judea, for thus it is written through the prophet,

Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli. Mathayo 2:6

'You Bethlehem, land of Judah, Are in no way least among the princes of Judah: For out of you shall come forth a governor, Who shall shepherd my people, Israel.'"

Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. Mathayo 2:7

Then Herod secretly called the wise men, and learned from them exactly what time the star appeared.

Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. Mathayo 2:8

He sent them to Bethlehem, and said, "Go and search diligently for the young child. When you have found him, bring me word, so that I also may come and worship him."

Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. Mathayo 2:9

They, having heard the king, went their way; and behold, the star, which they saw in the east, went before them, until it came and stood over where the young child was.

Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Mathayo 2:10

When they saw the star, they rejoiced with exceedingly great joy.

Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Mathayo 2:11

They came into the house and saw the young child with Mary, his mother, and they fell down and worshiped him. Opening their treasures, they offered to him gifts: gold, frankincense, and myrrh.

Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. Mathayo 2:12

Being warned in a dream that they shouldn't return to Herod, they went back to their own country another way.

Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. Mathayo 2:13

Now when they had departed, behold, an angel of the Lord appeared to Joseph in a dream, saying, "Arise and take the young child and his mother, and flee into Egypt, and stay there until I tell you, for Herod will seek the young child to destroy him."

Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; Mathayo 2:14

He arose and took the young child and his mother by night, and departed into Egypt,

akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu. Mathayo 2:15

and was there until the death of Herod; that it might be fulfilled which was spoken by the Lord through the prophet, saying, "Out of Egypt I called my son."

Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi. Mathayo 2:16

Then Herod, when he saw that he was mocked by the wise men, was exceedingly angry, and sent out, and killed all the male children who were in Bethlehem and in all the surrounding countryside, from two years old and under, according to the exact time which he had learned from the wise men.

Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Mathayo 2:17

Then that which was spoken by Jeremiah the prophet was fulfilled, saying,

Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako. Mathayo 2:18

"A voice was heard in Ramah, Lamentation, weeping and great mourning, Rachel weeping for her children; She wouldn't be comforted, Because they are no more."

Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, Mathayo 2:19

But when Herod was dead, behold, an angel of the Lord appeared in a dream to Joseph in Egypt, saying,

akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. Mathayo 2:20

"Arise and take the young child and his mother, and go into the land of Israel, for those who sought the young child's life are dead."

Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. Mathayo 2:21

He arose and took the young child and his mother, and came into the land of Israel.

Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, Mathayo 2:22

But when he heard that Archelaus was reigning over Judea in the place of his father, Herod, he was afraid to go there. Being warned in a dream, he withdrew into the region of Galilee,

akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo. Mathayo 2:23

and came and lived in a city called Nazareth; that it might be fulfilled which was spoken through the prophets: "He will be called a Nazarene."