Mathayo 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 28 (Swahili) Matthew 28 (English)

Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Mathayo 28:1

Now after the Sabbath, as it began to dawn on the first day of the week, Mary Magdalene and the other Mary came to see the tomb.

Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. Mathayo 28:2

Behold, there was a great earthquake, for an angel of the Lord descended from the sky, and came and rolled away the stone from the door, and sat on it.

Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Mathayo 28:3

His appearance was like lightning, and his clothing white as snow.

Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Mathayo 28:4

For fear of him, the guards shook, and became like dead men.

Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. Mathayo 28:5

The angel answered the women, "Don't be afraid, for I know that you seek Jesus, who has been crucified.

Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Mathayo 28:6

He is not here, for he has risen, just like he said. Come, see the place where the Lord was lying.

Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia. Mathayo 28:7

Go quickly and tell his disciples, 'He has risen from the dead, and behold, he goes before you into Galilee; there you will see him.' Behold, I have told you."

Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. Mathayo 28:8

They departed quickly from the tomb with fear and great joy, and ran to bring his disciples word.

Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. Mathayo 28:9

As they went to tell his disciples, behold, Jesus met them, saying, "Rejoice!" They came and took hold of his feet, and worshiped him.

Kisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona. Mathayo 28:10

Then Jesus said to them, "Don't be afraid. Go tell my brothers{The word for "brothers" here may be also correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} that they should go into Galilee, and there they will see me."

Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka. Mathayo 28:11

Now while they were going, behold, some of the guards came into the city, and told the chief priests all the things that had happened.

Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, Mathayo 28:12

When they were assembled with the elders, and had taken counsel, they gave a large amount of silver to the soldiers,

wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. Mathayo 28:13

saying, "Say that his disciples came by night, and stole him away while we slept.

Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi. Mathayo 28:14

If this comes to the governor's ears, we will persuade him and make you free of worry."

Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo. Mathayo 28:15

So they took the money and did as they were told. This saying was spread abroad among the Jews, and continues until this day.

Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Mathayo 28:16

But the eleven disciples went into Galilee, to the mountain where Jesus had sent them.

Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Mathayo 28:17

When they saw him, they bowed down to him, but some doubted.

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Mathayo 28:18

Jesus came to them and spoke to them, saying, "All authority has been given to me in heaven and on earth.

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; Mathayo 28:19

Therefore go, and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father and of the Son and of the Holy Spirit,

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Mathayo 28:20

teaching them to observe all things that I commanded you. Behold, I am with you always, even to the end of the age." Amen.