2 Wafalme 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 18 (Swahili) 2nd Kings 18 (English)

Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia, mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala. 2 Wafalme 18:1

Now it happened in the third year of Hoshea son of Elah king of Israel, that Hezekiah the son of Ahaz king of Judah began to reign.

Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria. 2 Wafalme 18:2

He was twenty-five years old when he began to reign; and he reigned twenty-nine years in Jerusalem: and his mother's name was Abi the daughter of Zechariah.

Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya Daudi, baba yake. 2 Wafalme 18:3

He did that which was right in the eyes of Yahweh, according to all that David his father had done.

Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani 2 Wafalme 18:4

He removed the high places, and broke the pillars, and cut down the Asherah: and he broke in pieces the brazen serpent that Moses had made; for to those days the children of Israel did burn incense to it; and he called it Nehushtan.

Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia. 2 Wafalme 18:5

He trusted in Yahweh, the God of Israel; so that after him was none like him among all the kings of Judah, nor [among them] that were before him.

Maana alishikamana na Bwana, hakuacha kumfuata, bali alizishika amri zake Bwana alizomwamuru Musa. 2 Wafalme 18:6

For he joined with Yahweh; he didn't depart from following him, but kept his commandments, which Yahweh commanded Moses.

Naye Bwana akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia. 2 Wafalme 18:7

Yahweh was with him; wherever he went forth he prospered: and he rebelled against the king of Assyria, and didn't serve him.

Akawapiga Wafilisti mpaka Gaza na mipaka yake, tangu mnara wa walinzi hata mji wenye boma. 2 Wafalme 18:8

He struck the Philistines to Gaza and the borders of it, from the tower of the watchmen to the fortified city.

Hata katika mwaka wa nne wa Hezekia, ndio mwaka wa saba wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Shalmanesa, mfalme wa Ashuru, akakwea ili kupigana na Samaria, akauhusuru. 2 Wafalme 18:9

It happened in the fourth year of king Hezekiah, which was the seventh year of Hoshea son of Elah king of Israel, that Shalmaneser king of Assyria came up against Samaria, and besieged it.

Wakautwaa baada ya miaka mitatu; yaani, katika mwaka wa sita wa Hezekia, ndio mwaka wa kenda wa Hoshea, mfalme wa Israeli, ndipo Samaria ulipotwaliwa. 2 Wafalme 18:10

At the end of three years they took it: in the sixth year of Hezekiah, which was the ninth year of Hoshea king of Israel, Samaria was taken.

Mfalme wa Ashuru akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala, na katika Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi; 2 Wafalme 18:11

The king of Assyria carried Israel away to Assyria, and put them in Halah, and on the Habor, the river of Gozan, and in the cities of the Medes,

kwa sababu hawakuitii sauti ya Bwana, Mungu wao, bali waliyahalifu maagano yake, mambo yote ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwaamuru, wasikubali kuyasikiliza, wala kuyatenda. 2 Wafalme 18:12

because they didn't obey the voice of Yahweh their God, but transgressed his covenant, even all that Moses the servant of Yahweh commanded, and would not hear it, nor do it.

Ikawa katika mwaka wa kumi na nne wa kumiliki kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa. 2 Wafalme 18:13

Now in the fourteenth year of king Hezekiah did Sennacherib king of Assyria come up against all the fortified cities of Judah, and took them.

Basi Hezekia, mfalme wa Yuda, akapeleka wajumbe waende Lakishi kwa mfalme wa Ashuru, kusema, Nimekosa; uniache ukarudi kwako; cho chote utakachoweka juu yangu, nitakichukua. Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia, mfalme wa Yuda, talanta za fedha mia tatu, na talanta za dhahabu thelathini. 2 Wafalme 18:14

Hezekiah king of Judah sent to the king of Assyria to Lachish, saying, I have offended; return from me: that which you put on me will I bear. The king of Assyria appointed to Hezekiah king of Judah three hundred talents of silver and thirty talents of gold.

Hezekia akampa fedha yote iliyoonekana katika nyumba ya Bwana, na katika hazina za nyumba ya mfalme. 2 Wafalme 18:15

Hezekiah gave [him] all the silver that was found in the house of Yahweh, and in the treasures of the king's house.

Wakati huo Hezekia aliiondoa dhahabu iliyokuwa juu ya milango ya hekalu la Bwana, na juu ya nguzo, ambazo Hezekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amezitia dhahabu, akampa mfalme wa Ashuru. 2 Wafalme 18:16

At that time did Hezekiah cut off [the gold from] the doors of the temple of Yahweh, and [from] the pillars which Hezekiah king of Judah had overlaid, and gave it to the king of Assyria.

Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na amiri wake toka Lakishi ,kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Nao wakakwea wakafika Yerusalemu. Na walipokwisha kufika , wakaja wakasimama karibu na mfereji wa birika la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea uwanda wa dobi. 2 Wafalme 18:17

The king of Assyria sent Tartan and Rabsaris and Rabshakeh from Lachish to king Hezekiah with a great army to Jerusalem. They went up and came to Jerusalem. When they were come up, they came and stood by the conduit of the upper pool, which is in the highway of the fuller's field.

Na walipokwisha kumwita mfalme, wakatokewa na Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe. 2 Wafalme 18:18

When they had called to the king, there came out to them Eliakim the son of Hilkiah, who was over the household, and Shebnah the scribe, and Joah the son of Asaph the recorder.

Yule amiri akawaambia ,haya mwambieni Hezekia,kusema ,Mfalme mkuu,mfalme wa Ashuru, asema hivi, Ni tumaini gani hili unalolitumainia? 2 Wafalme 18:19

Rabshakeh said to them, Say you now to Hezekiah, Thus says the great king, the king of Assyria, What confidence is this in which you trust?

Wewe wasema, lakini ni maneno yasiyo na maana, kwamba, Lipo shauri na zipo nguvu kwa vita hivi. Basi, unamtumaini nani hata ukaniasi mimi? 2 Wafalme 18:20

You say (but they are but vain words), [There is] counsel and strength for the war. Now on whom do you trust, that you have rebelled against me?

Sasa tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo mtu akiitegemea, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio. 2 Wafalme 18:21

Now, behold, you trust on the staff of this bruised reed, even on Egypt; whereon if a man lean, it will go into his hand, and pierce it: so is Pharaoh king of Egypt to all who trust on him.

Lakini mkiniambia, Tunamtumaini Bwana, Mungu wetu; je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii hapa Yerusalemu? 2 Wafalme 18:22

But if you tell me, We trust in Yahweh our God; isn't that he whose high places and whose altars Hezekiah has taken away, and has said to Judah and to Jerusalem, You shall worship before this altar in Jerusalem?

Basi sasa, tafadhali mpe bwana wangu, mfalme wa Ashuru, dhamana, nami nitakupa farasi elfu mbili, ikiwa wewe kwa upande wako waweza kupandisha watu juu yao. 2 Wafalme 18:23

Now therefore, Please give pledges to my master the king of Assyria, and I will give you two thousand horses, if you are able on your part to set riders on them.

Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa akida mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi? 2 Wafalme 18:24

How then can you turn away the face of one captain of the least of my master's servants, and put your trust on Egypt for chariots and for horsemen?

Je! Nimepanda mimi, ili kupigana na mahali hapa na kupaangamiza, bila shauri la Bwana? Bwana ndiye aliyeniambia, Panda upigane na nchi hii na kuiangamiza. 2 Wafalme 18:25

Am I now come up without Yahweh against this place to destroy it? Yahweh said to me, Go up against this land, and destroy it.

Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule amiri, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa hao watu walio ukutani. 2 Wafalme 18:26

Then said Eliakim the son of Hilkiah, and Shebnah, and Joah, to Rabshakeh, Please speak to your servants in the Syrian language; for we understand it: and don't speak with us in the Jews' language, in the ears of the people who are on the wall.

Lakini yule amiri akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Je! Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi? 2 Wafalme 18:27

But Rabshakeh said to them, Has my master sent me to your master, and to you, to speak these words? Hasn't he sent me to the men who sit on the wall, to eat their own dung, and to drink their own water with you?

Kisha yule amiri akasimama akalia kwa sauti kuu kwa lugha ya Kiyahudi, akasema, Lisikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru. 2 Wafalme 18:28

Then Rabshakeh stood, and cried with a loud voice in the Jews' language, and spoke, saying, Hear you the word of the great king, the king of Assyria.

Mfalme asema hivi, Hezekia asiwadanganye; kwa maana, hataweza kuwaokoa katika mkono wake. 2 Wafalme 18:29

Thus says the king, Don't let Hezekiah deceive you; for he will not be able to deliver you out of his hand:

Wala Hezekia asiwatumainishe katika Bwana, akisema, Hakika Bwana atatuokoa, wala mji huu hautatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru. 2 Wafalme 18:30

neither let Hezekiah make you trust in Yahweh, saying, Yahweh will surely deliver us, and this city shall not be given into the hand of the king of Assyria.

Msimsikilize Hezekia; kwa sababu mfalme wa Ashuru asema hivi, Fanyeni suluhu na mimi, mkatoke mnijie; mkale kila mtu matunda ya mzabibu wake na matunda ya mtini wake, mkanywe kila mmoja maji ya birika lake mwenyewe; 2 Wafalme 18:31

Don't listen to Hezekiah: for thus says the king of Assyria, Make your peace with me, and come out to me; and eat you everyone of his vine, and everyone of his fig tree, and everyone drink the waters of his own cistern;

hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, Bwana atatuokoa. 2 Wafalme 18:32

Until I come and take you away to a land like your own land, a land of grain and new wine, a land of bread and vineyards, a land of olive trees and of honey, that you may live, and not die: and don't listen to Hezekiah, when he persuades you, saying, Yahweh will deliver us.

Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake wakati wo wote na mkono wa mfalme wa Ashuru? 2 Wafalme 18:33

Has any of the gods of the nations ever delivered his land out of the hand of the king of Assyria?

Iko wapi miungu ya Hamathi, na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, na ya Hena, na ya Iva? Je! Imeuokoa Samaria na mkono wangu? 2 Wafalme 18:34

Where are the gods of Hamath, and of Arpad? where are the gods of Sepharvaim, of Hena, and Ivvah? have they delivered Samaria out of my hand?

Katika miungu ya nchi hizi zote, ni miungu gani iliyookoa nchi yao na mkono wangu, hata Bwana auokoe Yerusalemu na mkono wangu? 2 Wafalme 18:35

Who are they among all the gods of the countries, that have delivered their country out of my hand, that Yahweh should deliver Jerusalem out of my hand?

Lakini hao watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana amri ya mfalme ilikuwa kwamba, Msimjibu neno. 2 Wafalme 18:36

But the people held their peace, and answered him not a word; for the king's commandment was, saying, Don't answer him.

Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia maneno ya yule amiri. 2 Wafalme 18:37

Then came Eliakim the son of Hilkiah, who was over the household, and Shebna the scribe, and Joah the son of Asaph the recorder, to Hezekiah with their clothes torn, and told him the words of Rabshakeh.