2 Wafalme 23 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 23 (Swahili) 2nd Kings 23 (English)

Kisha, mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. 2 Wafalme 23:1

The king sent, and they gathered to him all the elders of Judah and of Jerusalem.

Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 23:2

The king went up to the house of Yahweh, and all the men of Judah and all the inhabitants of Jerusalem with him, and the priests, and the prophets, and all the people, both small and great: and he read in their ears all the words of the book of the covenant which was found in the house of Yahweh.

Mfalme akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile. 2 Wafalme 23:3

The king stood by the pillar, and made a covenant before Yahweh, to walk after Yahweh, and to keep his commandments, and his testimonies, and his statutes, with all [his] heart, and all [his] soul, to confirm the words of this covenant that were written in this book: and all the people stood to the covenant.

Kisha, mfalme akamwamuru Hilkia, kuhani mkuu, na makuhani wa daraja ya pili, na walinzi wa mlango, kwamba watoe katika hekalu la Bwana vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali, na kwa ajili ya Ashera, na kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni; akavipiga moto nje ya Yerusalemu, katika mashamba ya Ridroni, akayachukua majivu yake mpaka Betheli. 2 Wafalme 23:4

The king commanded Hilkiah the high priest, and the priests of the second order, and the keepers of the threshold, to bring forth out of the temple of Yahweh all the vessels that were made for Baal, and for the Asherah, and for all the host of the sky, and he burned them outside of Jerusalem in the fields of the Kidron, and carried the ashes of them to Bethel.

Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. 2 Wafalme 23:5

He put down the idolatrous priests, whom the kings of Judah had ordained to burn incense in the high places in the cities of Judah, and in the places round about Jerusalem; those also who burned incense to Baal, to the sun, and to the moon, and to the planets, and to all the host of the sky.

Naye akaiondoa Ashera katika nyumba ya Bwana, nje ya Yerusalemu, mpaka Kidroni, akaipiga moto penye kijito cha Kidroni, na kuiponda-ponda iwe mavumbi, akayatupa mavumbi yake juu ya makaburi ya watu. 2 Wafalme 23:6

He brought out the Asherah from the house of Yahweh, outside of Jerusalem, to the brook Kidron, and burned it at the brook Kidron, and beat it to dust, and cast the dust of it on the graves of the common people.

Akaziangusha nyumba za mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa Bwana, wanawake walipofuma mapazia ya Ashera. 2 Wafalme 23:7

He broke down the houses of the sodomites, that were in the house of Yahweh, where the women wove hangings for the Asherah.

Akawatoa makuhani wote katika miji ya Yuda, akapanajisi mahali pa juu, makuhani walipokuwa wamefukiza uvumba, tangu Geba hata Beer-sheba; akapavunja mahali pa juu pa malango, palipokuwapo penye kuingia lango la Yoshua, liwali wa mji, palipokuwa upande wa kushoto wa mtu langoni pa mji. 2 Wafalme 23:8

He brought all the priests out of the cities of Judah, and defiled the high places where the priests had burned incense, from Geba to Beersheba; and he broke down the high places of the gates that were at the entrance of the gate of Joshua the governor of the city, which were on a man's left hand at the gate of the city.

Walakini hao makuhani wa mahali pa juu hawakupanda madhabahuni kwa Bwana katika Yerusalemu, bali wakala mikate isiyo na chachu katikati ya ndugu zao. 2 Wafalme 23:9

Nevertheless the priests of the high places didn't come up to the altar of Yahweh in Jerusalem, but they ate unleavened bread among their brothers.

Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki. 2 Wafalme 23:10

He defiled Topheth, which is in the valley of the children of Hinnom, that no man might make his son or his daughter to pass through the fire to Molech.

Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa jua, hapo pa kuingia nyumbani mwa Bwana, karibu na chumba cha Nathan-Meleki, towashi, kilichohuwako kiungani; akayapiga moto magari ya jua. 2 Wafalme 23:11

He took away the horses that the kings of Judah had given to the sun, at the entrance of the house of Yahweh, by the chamber of Nathan-melech the chamberlain, which was in the precincts; and he burned the chariots of the sun with fire.

Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya Bwana, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni. 2 Wafalme 23:12

The altars that were on the roof of the upper chamber of Ahaz, which the kings of Judah had made, and the altars which Manasseh had made in the two courts of the house of Yahweh, did the king break down, and beat [them] down from there, and cast the dust of them into the brook Kidron.

Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi. 2 Wafalme 23:13

The high places that were before Jerusalem, which were on the right hand of the mountain of corruption, which Solomon the king of Israel had built for Ashtoreth the abomination of the Sidonians, and for Chemosh the abomination of Moab, and for Milcom the abomination of the children of Ammon, did the king defile.

Akazivunja-vunja nguzo, akayakata-kata maashera, akapajaza mahali pake mifupa ya watu. 2 Wafalme 23:14

He broke in pieces the pillars, and cut down the Asherim, and filled their places with the bones of men.

Tena zaidi ya hayo, ile madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli, madhabahu hiyo aliibomoa; na mahali pa juu alipateketeza, akapaponda-ponda hata pakawa mavumbi, akaiteketeza ile Ashera. 2 Wafalme 23:15

Moreover the altar that was at Bethel, and the high place which Jeroboam the son of Nebat, who made Israel to sin, had made, even that altar and the high place he broke down; and he burned the high place and beat it to dust, and burned the Asherah.

Naye Yosia alipogeuka, aliyaona makaburi yale yaliyokuwako huko, juu ya mlima; akatuma watu, akaitoa ile mifupa katika yale makaburi, akaiteketeza juu ya madhabahu, akainajisi, sawasawa na lile neno la Bwana, alilolinena yule mtu wa Mungu, aliyetamka mambo hayo. 2 Wafalme 23:16

As Josiah turned himself, he spied the tombs that were there in the mountain; and he sent, and took the bones out of the tombs, and burned them on the altar, and defiled it, according to the word of Yahweh which the man of God proclaimed, who proclaimed these things.

Kisha akasema, Ni kumbukumbu la nani, hili ninaloliona? Na watu wa mji wakamwambia, Ni kaburi la yule mtu wa Mungu, aliyetoka Yuda, akayanena mambo hayo uliyoyatenda wewe juu ya madhabahu ya Betheli. 2 Wafalme 23:17

Then he said, What monument is that which I see? The men of the city told him, It is the tomb of the man of God, who came from Judah, and proclaimed these things that you have done against the altar of Bethel.

Akasema, Mwacheni; mtu awaye yote asiiondoe mifupa yake. Basi wakaiacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya yule nabii aliyetoka Samaria. 2 Wafalme 23:18

He said, Let him be; let no man move his bones. So they let his bones alone, with the bones of the prophet who came out of Samaria.

Na nyumba zote pia za mahali pa juu palipokuwa katika miji ya Samaria, wafalme wa Israeli walizozifanya, ili kumkasirisha Bwana, Yosia aliziondoa, akazitenda kwa mfano wa mambo yote aliyoyatenda katika Betheli. 2 Wafalme 23:19

All the houses also of the high places that were in the cities of Samaria, which the kings of Israel had made to provoke [Yahweh] to anger, Josiah took away, and did to them according to all the acts that he had done in Bethel.

Akawaua na makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu. 2 Wafalme 23:20

He killed all the priests of the high places that were there, on the altars, and burned men's bones on them; and he returned to Jerusalem.

Naye mfalme akawaamuru watu wote, akasema, Mfanyieni Bwana, Mungu wenu, pasaka, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha agano. 2 Wafalme 23:21

The king commanded all the people, saying, Keep the Passover to Yahweh your God, as it is written in this book of the covenant.

Hakika yake haikufanyika pasaka kama hiyo, tangu zamani za waamuzi waliowaamua Israeli, wala katika zamani za wafalme wa Israeli, wala za wafalme wa Yuda. 2 Wafalme 23:22

Surely there was not kept such a Passover from the days of the judges who judged Israel, nor in all the days of the kings of Israel, nor of the kings of Judah;

Bali katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia ilifanyika pasaka hii kwa Bwana ndani ya Yerusalemu. 2 Wafalme 23:23

but in the eighteenth year of king Josiah was this Passover kept to Yahweh in Jerusalem.

Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 23:24

Moreover those who had familiar spirits, and the wizards, and the teraphim, and the idols, and all the abominations that were seen in the land of Judah and in Jerusalem, did Josiah put away, that he might confirm the words of the law which were written in the book that Hilkiah the priest found in the house of Yahweh.

Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye. 2 Wafalme 23:25

Like him was there no king before him, who turned to Yahweh with all his heart, and with all his soul, and with all his might, according to all the law of Moses; neither after him arose there any like him.

Walakini Bwana hakuuacha ukali wa ghadhabu yake nyingi, ambayo kwayo hasira yake iliwaka juu ya Yuda, kwa sababu ya machukizo yote ambayo Manase amemchukiza. 2 Wafalme 23:26

Notwithstanding, Yahweh didn't turn from the fierceness of his great wrath, with which his anger was kindled against Judah, because of all the provocation with which Manasseh had provoked him.

Bwana akasema Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo. 2 Wafalme 23:27

Yahweh said, I will remove Judah also out of my sight, as I have removed Israel, and I will cast off this city which I have chosen, even Jerusalem, and the house of which I said, My name shall be there.

Basi mambo yote ya Yosia yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 23:28

Now the rest of the acts of Josiah, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Katika siku zake, Farao-neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye. 2 Wafalme 23:29

In his days Pharaoh Necoh king of Egypt went up against the king of Assyria to the river Euphrates: and king Josiah went against him; and [Pharaoh Necoh] killed him at Megiddo, when he had seen him.

Watumishi wake wakamchukua garini, amekwisha kufa, kutoka Megido, wakamleta Yerusalemu, wakamzika katika kaburi lake mwenyewe. Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, wakamtawaza awe mfalme badala ya baba yake. 2 Wafalme 23:30

His servants carried him in a chariot dead from Megiddo, and brought him to Jerusalem, and buried him in his own tomb. The people of the land took Jehoahaz the son of Josiah, and anointed him, and made him king in his father's place.

Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala; akatawala miezi mitatu katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Hamutali binti Yeremia wa Libna. 2 Wafalme 23:31

Jehoahaz was twenty-three years old when he began to reign; and he reigned three months in Jerusalem: and his mother's name was Hamutal the daughter of Jeremiah of Libnah.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote waliyoyafanya baba zake. 2 Wafalme 23:32

He did that which was evil in the sight of Yahweh, according to all that his fathers had done.

Naye Farao-neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia za fedha na talanta ya dhahabu. 2 Wafalme 23:33

Pharaoh Necoh put him in bonds at Riblah in the land of Hamath, that he might not reign in Jerusalem; and put the land to a tribute of one hundred talents of silver, and a talent of gold.

Farao-neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia awe mfalme mahali pa Yosia babaye, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu, lakini akamwondoa Yehoahazi; akaenda naye Misri, naye akafa huko. 2 Wafalme 23:34

Pharaoh Necoh made Eliakim the son of Josiah king in the room of Josiah his father, and changed his name to Jehoiakim: but he took Jehoahaz away; and he came to Egypt, and died there.

Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao-neko. 2 Wafalme 23:35

Jehoiakim gave the silver and the gold to Pharaoh; but he taxed the land to give the money according to the commandment of Pharaoh: he exacted the silver and the gold of the people of the land, of everyone according to his taxation, to give it to Pharaoh Necoh.

Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Zebida binti Pedaya wa Ruma. 2 Wafalme 23:36

Jehoiakim was twenty-five years old when he began to reign; and he reigned eleven years in Jerusalem: and his mother's name was Zebidah the daughter of Pedaiah of Rumah.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote waliyoyafanya baba zake. 2 Wafalme 23:37

He did that which was evil in the sight of Yahweh, according to all that his fathers had done.