2 Wafalme 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 11 (Swahili) 2nd Kings 11 (English)

Na Athalia, mama yake Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaharibu wazao wote wa kifalme. 2 Wafalme 11:1

Now when Athaliah the mother of Ahaziah saw that her son was dead, she arose and destroyed all the seed royal.

Ila Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu, umbu lake Ahazia ,akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia ,akamwiba miongoni mwa hao wana wa mfalme waliouawa ,yeye na mlezi wake ,na kuwatia katika chumba cha kulala;wakamficha usoni pa Athalia,basi kwa hiyo hakuuawa. 2 Wafalme 11:2

But Jehosheba, the daughter of king Joram, sister of Ahaziah, took Joash the son of Ahaziah, and stole him away from among the king's sons who were slain, even him and his nurse, [and put them] in the bedchamber; and they hid him from Athaliah, so that he was not slain;

Alikuwako pamoja naye, amefichwa nyumbani mwa Bwana, miaka sita. Naye Athalia akaitawala nchi. 2 Wafalme 11:3

He was with her hid in the house of Yahweh six years. Athaliah reigned over the land.

Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya Bwana; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa Bwana, akawaonyesha huyo mwana wa mfalme. 2 Wafalme 11:4

In the seventh year Jehoiada sent and fetched the captains over hundreds of the Carites and of the guard, and brought them to him into the house of Yahweh; and he made a covenant with them, and took an oath of them in the house of Yahweh, and shown them the king's son.

Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoingia siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya mfalme; 2 Wafalme 11:5

He commanded them, saying, This is the thing that you shall do: a third part of you, who come in on the Sabbath, shall be keepers of the watch of the king's house;

na theluthi mtakuwapo mlangoni pa Suri; na theluthi langoni nyuma ya walinzi; hivyo mtayalinda malinzi ya nyumba, kuzuia watu wasiingie. 2 Wafalme 11:6

A third part shall be at the gate Sur; and a third part at the gate behind the guard: so shall you keep the watch of the house, and be a barrier.

Na sehemu mbili zenu, yaani, wote watokao siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya Bwana kumzunguka mfalme. 2 Wafalme 11:7

The two companies of you, even all who go forth on the Sabbath, shall keep the watch of the house of Yahweh about the king.

Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia. 2 Wafalme 11:8

You shall compass the king round about, every man with his weapons in his hand; and he who comes within the ranks, let him be slain: and be you with the king when he goes out, and when he comes in.

Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani. 2 Wafalme 11:9

The captains over hundreds did according to all that Jehoiada the priest commanded; and they took every man his men, those who were to come in on the Sabbath, with those who were to go out on the Sabbath, and came to Jehoiada the priest.

Naye yule kuhani akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao zilizokuwa za mfalme Daudi, zilizokuwamo nyumbani mwa Bwana. 2 Wafalme 11:10

The priest delivered to the captains over hundreds the spears and shields that had been king David's, which were in the house of Yahweh.

Walinzi wakasimama, kila mtu na silaha zake mkononi, kutoka pembe ya kuume ya nyumba mpaka pembe ya kushoto ya nyumba, kando ya madhabahu na nyumba, wakimzunguka mfalme pande zote. 2 Wafalme 11:11

The guard stood, every man with his weapons in his hand, from the right side of the house to the left side of the house, along by the altar and the house, by the king round about.

Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, mfalme na aishi. 2 Wafalme 11:12

Then he brought out the king's son, and put the crown on him, and [gave him] the testimony; and they made him king, and anointed him; and they clapped their hands, and said, [Long] live the king.

Na Athalia alipoisikia sauti ya walinzi na ya watu, aliingia kwa watu nyumbani kwa Bwana; 2 Wafalme 11:13

When Athaliah heard the noise of the guard [and of] the people, she came to the people into the house of Yahweh:

akatazama, na tazama, mfalme amesimama karibu na nguzo kama ilivyokuwa desturi, nao wakuu na wapiga baragumu karibu na mfalme; na watu wote wa nchi wakafurahi, wakapiga baragumu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akalia, Fitina! Fitina! 2 Wafalme 11:14

and she looked, and, behold, the king stood by the pillar, as the manner was, and the captains and the trumpets by the king; and all the people of the land rejoiced, and blew trumpets. Then Athaliah tore her clothes, and cried, Treason! treason!

Naye Yehoyada kuhani akawaamuru wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye ye yote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa Bwana. 2 Wafalme 11:15

Jehoiada the priest commanded the captains of hundreds who were set over the host, and said to them, Have her forth between the ranks; and him who follows her kill with the sword. For the priest said, Don't let her be slain in the house of Yahweh.

Basi wakampisha njia; akaenda kwa njia ya kuingia kwa farasi nyumbani mwa mfalme; akauawa huko. 2 Wafalme 11:16

So they made way for her; and she went by the way of the horses' entry to the king's house: and there was she slain.

Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya Bwana na mfalme na watu, ili wawe watu wa Bwana; tena kati ya mfalme na watu. 2 Wafalme 11:17

Jehoiada made a covenant between Yahweh and the king and the people, that they should be Yahweh's people; between the king also and the people.

Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka maakida juu ya nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 11:18

All the people of the land went to the house of Baal, and broke it down; his altars and his images broke they in pieces thoroughly, and killed Mattan the priest of Baal before the altars. The priest appointed officers over the house of Yahweh.

Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa Bwana, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme. 2 Wafalme 11:19

He took the captains over hundreds, and the Carites, and the guard, and all the people of the land; and they brought down the king from the house of Yahweh, and came by the way of the gate of the guard to the king's house. He sat on the throne of the kings.

Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia. Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme. 2 Wafalme 11:20

So all the people of the land rejoiced, and the city was quiet. Athaliah they had slain with the sword at the king's house.

Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala. 2 Wafalme 11:21

Jehoash was seven years old when he began to reign.