2 Wafalme 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 9 (Swahili) 2nd Kings 9 (English)

Nabii Elisha akamwita mmojawapo wa wana wa manabii, akamwambia, Jikaze viuno, ukachukue chupa hii ya mafuta mkononi mwako, ukaende Ramoth-Gileadi. 2 Wafalme 9:1

Elisha the prophet called one of the sons of the prophets, and said to him, Gird up your loins, and take this vial of oil in your hand, and go to Ramoth-gilead.

Utakapofika huko, mtafute Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, ukaingie, ukamtoe miongoni mwa ndugu zake, ukamchukue katika chumba cha ndani. 2 Wafalme 9:2

When you come there, look out there Jehu the son of Jehoshaphat the son of Nimshi, and go in, and make him arise up from among his brothers, and carry him to an inner chamber.

Kisha, ukatwae ile chupa ya mafuta, ukayamimine juu ya kichwa chake, ukaseme, Bwana asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. Kisha ufungue mlango ukakimbie, wala usikawie. 2 Wafalme 9:3

Then take the vial of oil, and pour it on his head, and say, Thus says Yahweh, I have anointed you king over Israel. Then open the door, and flee, and don't wait.

Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Ramoth-Gileadi. 2 Wafalme 9:4

So the young man, even the young man the prophet, went to Ramoth-gilead.

Naye alipofika, tazama, majemadari wa jeshi walikuwa wamekaa; naye akasema, Nimetumwa na neno kwako, Ee jemadari; Yehu akasema, Kwa yupi miongoni mwetu sote? Akasema, Kwako wewe, Ee jemadari. 2 Wafalme 9:5

When he came, behold, the captains of the host were sitting; and he said, I have an errand to you, captain. Jehu said, To which of us all? He said, To you, O captain.

Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Bwana, yaani, juu ya Israeli. 2 Wafalme 9:6

He arose, and went into the house; and he poured the oil on his head, and said to him, Thus says Yahweh, the God of Israel, I have anointed you king over the people of Yahweh, even over Israel.

Nawe utawapiga nyumba ya Ahabu, bwana wako, ili nijilipize kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa Bwana, mkononi mwa Yezebeli. 2 Wafalme 9:7

You shall strike the house of Ahab your master, that I may avenge the blood of my servants the prophets, and the blood of all the servants of Yahweh, at the hand of Jezebel.

Kwa maana nyumba yote ya Ahabu wataangamia; nami nitamkatilia mbali kila mwanamume wa nyumba ya Ahabu, yeye aliyefungwa, na yeye asiyefungwa, katika Israeli. 2 Wafalme 9:8

For the whole house of Ahab shall perish; and I will cut off from Ahab every man-child, and him who is shut up and him who is left at large in Israel.

Nami nitaifanya nyumba ya Ahabu kuwa kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya. 2 Wafalme 9:9

I will make the house of Ahab like the house of Jeroboam the son of Nebat, and like the house of Baasha the son of Ahijah.

Na mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli, wala hapatakuwa na mtu wa kumzika. Akaufungua mlango, akakimbia. 2 Wafalme 9:10

The dogs shall eat Jezebel in the portion of Jezreel, and there shall be none to bury her. He opened the door, and fled.

Ndipo Yehu akatoka akawaendea watumishi wa bwana wake. Mmoja wao akamwuliza, Je! Ni amani? Huyu mwenye wazimu amekujia kwa nini? Akawaambia, Ninyi mnamjua mtu huyu na habari ya maneno yake. 2 Wafalme 9:11

Then Jehu came forth to the servants of his lord: and one said to him, Is all well? why came this mad fellow to you? He said to them, You know the man and what his talk was.

Wakasema, Ni uongo; haya, tuambie. Akasema, Aliniambia haya na haya, akisema, Bwana asema hivi, Nimekutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli. 2 Wafalme 9:12

They said, It is false; tell us now. He said, Thus and thus spoke he to me, saying, Thus says Yahweh, I have anointed you king over Israel.

Basi wakafanya haraka, kila mtu akalitwaa vazi lake, na kulitia chini yake juu ya madaraja, wakapiga baragumu wakasema, Yehu ni mfalme. 2 Wafalme 9:13

Then they hurried, and took every man his garment, and put it under him on the top of the stairs, and blew the trumpet, saying, Jehu is king.

Hivyo Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akafanya fitina juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiulinda Ramoth-Gileadi, yeye na Israeli wote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu. 2 Wafalme 9:14

So Jehu the son of Jehoshaphat the son of Nimshi conspired against Joram. (Now Joram was keeping Ramoth-gilead, he and all Israel, because of Hazael king of Syria;

Lakini mfalme Yoramu mwenyewe alikuwa amerudi, apate kupona jeraha zake alizotiwa na Washami, alipokuwa akipigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Yehu akasema, Kama hii ndiyo nia yenu, basi, msimwache hata mtu mmoja atoke mjini, ili aende kupeleka habari Yezreeli. 2 Wafalme 9:15

but king Joram was returned to be healed in Jezreel of the wounds which the Syrians had given him, when he fought with Hazael king of Syria.) Jehu said, If this be your mind, then let none escape and go forth out of the city, to go to tell it in Jezreel.

Basi Yehu akapanda gari lake kwenda Yezreeli; kwa maana Yoramu alikuwa amelala huko; na Ahazia mfalme wa Yuda alikuwa ameshuka ili kumtazama Yoramu. 2 Wafalme 9:16

So Jehu rode in a chariot, and went to Jezreel; for Joram lay there. Ahaziah king of Judah was come down to see Joram.

Basi mlinzi alikuwa anasimama juu ya mnara wa Yezreeli, akaliona lile kundi la watu wa Yehu, alipokuwa akija, akasema, Naona kundi la watu. Yoramu akasema, Haya! Mtwae mpanda farasi mmoja, ukampeleke aende kuwalaki, na kuwauliza, Je! Ni amani? 2 Wafalme 9:17

Now the watchman was standing on the tower in Jezreel, and he spied the company of Jehu as he came, and said, I see a company. Joram said, Take a horseman, and send to meet them, and let him say, Is it peace?

Basi mpanda farasi mmoja akatoka awalaki, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate. Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Yule mjumbe amewafikilia, lakini harudi tena. 2 Wafalme 9:18

So there went one on horseback to meet him, and said, Thus says the king, Is it peace? Jehu said, What have you to do with peace? turn you behind me. The watchman told, saying, The messenger came to them, but he isn't coming back.

Ndipo akapeleka mpanda farasi wa pili, naye akawafikilia, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate. 2 Wafalme 9:19

Then he sent out a second on horseback, who came to them, and said, Thus says the king, Is it peace? Jehu answered, What have you to do with peace? turn you behind me.

Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Amewafikilia wala harudi tena; na mwendo huu ni kama mwendo wa Yehu mwana wa Nimshi; maana analiendesha gari kwa kasi. 2 Wafalme 9:20

The watchman told, saying, He came even to them, and isn't coming back: and the driving is like the driving of Jehu the son of Nimshi; for he drives furiously.

Yoramu akasema, Tandika gari. Wakalitandika gari lake. Yoramu mfalme wa Israeli akatoka, na Ahazia mfalme wa Yuda, kila mtu katika gari lake. Wakatoka ili kumlaki Yehu, wakamkuta katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli. 2 Wafalme 9:21

Joram said, Make ready. They made ready his chariot. Joram king of Israel and Ahaziah king of Judah went out, each in his chariot, and they went out to meet Jehu, and found him in the portion of Naboth the Jezreelite.

Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi? 2 Wafalme 9:22

It happened, when Joram saw Jehu, that he said, Is it peace, Jehu? He answered, What peace, so long as the prostitution of your mother Jezebel and her witchcraft abound?

Yoramu akageuza mikono yake, akakimbia, akamwambia Ahazia, Ni uhaini, Ahazia. 2 Wafalme 9:23

Joram turned his hands, and fled, and said to Ahaziah, There is treachery, Ahaziah.

Yehu akavuta upinde wake kwa nguvu zake zote, akampiga Yoramu kati ya mikono yake, hata mshale ukamtoka penye moyo wake, akaanguka katika gari lake. 2 Wafalme 9:24

Jehu drew his bow with his full strength, and struck Joram between his arms; and the arrow went out at his heart, and he sunk down in his chariot.

Ndipo Yehu akamwambia Bidkari, akida wake, Mtwae ukamtupe katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli; maana kumbuka, hapo mimi na wewe tulipokuwa tumepanda farasi zetu, na kumfuata Anabu baba yake, Bwana alimwekea mzigo huu, akasema; 2 Wafalme 9:25

Then said [Jehu] to Bidkar his captain, Take up, and cast him in the portion of the field of Naboth the Jezreelite; for remember how that, when I and you rode together after Ahab his father, Yahweh laid this burden on him:

Hakika, jana nimeiona damu ya Nabothi, na damu ya wanawe, asema Bwana; nami nitakulipa katika kiwanja hiki, asema Bwana. Basi sasa mtwae huyu ukamtupe katika kiwanja hicho, sawasawa na neno la Bwana. 2 Wafalme 9:26

Surely I have seen yesterday the blood of Naboth, and the blood of his sons, says Yahweh; and I will requite you in this plat, says Yahweh. Now therefore take and cast him into the plat [of ground], according to the word of Yahweh.

Na Ahazia mfalme wa Yuda alipoona hayo, akakimbia kwa njia ya nyumba ya bustanini. Yehu akamfuatia, akasema, Mpigeni huyu naye katika gari lake; wakampiga hapo penye kupandia Guri, karibu na Ibleamu. Akakimbilia Megido, akafa huko. 2 Wafalme 9:27

But when Ahaziah the king of Judah saw this, he fled by the way of the garden-house. Jehu followed after him, and said, Smite him also in the chariot: [and they struck him] at the ascent of Gur, which is by Ibleam. He fled to Megiddo, and died there.

Na watumishi wake wakamchukua garini mpaka Yerusalemu, wakamzika katika kaburi lake pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. 2 Wafalme 9:28

His servants carried him in a chariot to Jerusalem, and buried him in his tomb with his fathers in the city of David.

Katika mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu, Ahazia alianza kutawala juu ya Yuda. 2 Wafalme 9:29

In the eleventh year of Joram the son of Ahab began Ahaziah to reign over Judah.

Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani. 2 Wafalme 9:30

When Jehu was come to Jezreel, Jezebel heard of it; and she painted her eyes, and attired her head, and looked out at the window.

Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako? 2 Wafalme 9:31

As Jehu entered in at the gate, she said, Is it peace, you Zimri, your master's murderer?

Akainua uso wake kulielekea dirisha, akasema, Aliye upande wangu ni nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia. 2 Wafalme 9:32

He lifted up his face to the window, and said, Who is on my side? who? There looked out to him two or three eunuchs.

Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga. 2 Wafalme 9:33

He said, Throw her down. So they threw her down; and some of her blood was sprinkled on the wall, and on the horses: and he trod her under foot.

Alipoingia, akala, na kunywa; kisha akasema, Haya! Mwangalieni mwanamke huyu aliyelaaniwa, mkamzike; kwa maana ni binti mfalme. 2 Wafalme 9:34

When he was come in, he ate and drink; and he said, See now to this cursed woman, and bury her; for she is a king's daughter.

Wakaenda ili kumzika; lakini hawakuona kitu ila kifuvu cha kichwa chake, na miguu yake, na vitanga vya mikono yake. 2 Wafalme 9:35

They went to bury her; but they found no more of her than the skull, and the feet, and the palms of her hands.

Basi wakarudi, wakampasha habari. Akasema, Hili ndilo neno la Bwana, alilolinena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya, Mtishbi, kusema, Katika kiwanja cha Yezreeli mbwa wataila nyama ya Yezebeli. 2 Wafalme 9:36

Therefore they came back, and told him. He said, This is the word of Yahweh, which he spoke by his servant Elijah the Tishbite, saying, In the portion of Jezreel shall the dogs eat the flesh of Jezebel;

Na mzoga wa Yezebeli utakuwa kama mavi juu ya uso wa mashamba, katika kiwanja cha Yezreeli; hata wasipate kusema, Huyu ni Yezebeli. 2 Wafalme 9:37

and the body of Jezebel shall be as dung on the face of the field in the portion of Jezreel, so that they shall not say, This is Jezebel.