2 Wafalme 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 8 (Swahili) 2nd Kings 8 (English)

Basi Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke, ambaye alimfufulia mwanawe, akasema, Ondoka, ukaende wewe na jamaa yako, ukae hali ya kigeni utakakoweza kukaa; kwa sababu Bwana ameiita njaa; nayo itakuja juu ya nchi hii muda wa miaka saba. 2 Wafalme 8:1

Now Elisha had spoken to the woman, whose son he had restored to life, saying, Arise, and go you and your household, and sojourn wherever you can sojourn: for Yahweh has called for a famine; and it shall also come on the land seven years.

Akaondoka yule mwanamke, akafanya kama alivyosema mtu wa Mungu; akaenda, yeye na jamaa yake, akakaa katika nchi ya Wafilisti miaka saba. 2 Wafalme 8:2

The woman arose, and did according to the word of the man of God; and she went with her household, and sojourned in the land of the Philistines seven years.

Ikawa miaka saba ilipoisha, yule mwanamke akarudi kutoka nchi ya Wafilisti; akatokea amlilie mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. 2 Wafalme 8:3

It happened at the seven years' end, that the woman returned out of the land of the Philistines: and she went forth to cry to the king for her house and for her land.

Basi mfalme alikuwa akizungumza na Gehazi, mtumishi wa mtu wa Mungu, akinena, Uniambie, nakusihi, mambo makuu yote aliyoyafanya Elisha. 2 Wafalme 8:4

Now the king was talking with Gehazi the servant of the man of God, saying, Please tell me all the great things that Elisha has done.

Ikawa, alipokuwa katika kumwambia mfalme jinsi alivyomfufua mtu aliyekufa, tazama, huyo mwanamke aliyemfufulia mwanawe, alimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, Bwana wangu mfalme, huyu ndiye mwanamke, na huyu ndiye mwanawe, ambaye Elisha alimfufua. 2 Wafalme 8:5

It happened, as he was telling the king how he had restored to life him who was dead, that behold, the woman, whose son he had restored to life, cried to the king for her house and for her land. Gehazi said, My lord, O king, this is the woman, and this is her son, whom Elisha restored to life.

Na mfalme alipomwuliza yule mwanamke, yeye akamweleza. Basi mfalme akamtolea akida, akasema, Mrudishie yote aliyokuwa nayo, na mapato yote ya shamba lake tangu siku aliposafiri, hata leo. 2 Wafalme 8:6

When the king asked the woman, she told him. So the king appointed to her a certain officer, saying, Restore all that was hers, and all the fruits of the field since the day that she left the land, even until now.

Kisha, Elisha akaenda Dameski; na Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, alikuwa hawezi; akaambiwa ya kwamba, Yule mtu wa Mungu amefika hapa. 2 Wafalme 8:7

Elisha came to Damascus; and Benhadad the king of Syria was sick; and it was told him, saying, The man of God is come here.

Mfalme akamwambia Hazaeli, Chukua zawadi mkononi mwako, ukaende ili kumlaki yule mtu wa Mungu, ukamwulize Bwana kwa kinywa chake, kusema, Je! Nitapona ugonjwa huu? 2 Wafalme 8:8

The king said to Hazael, Take a present in your hand, and go, meet the man of God, and inquire of Yahweh by him, saying, Shall I recover of this sickness?

Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, za kila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mizigo ya ngamia arobaini, akaenda, akasimama mbele yake akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, amenituma kwako, kusema, Je nitapona ugonjwa huu? 2 Wafalme 8:9

So Hazael went to meet him, and took a present with him, even of every good thing of Damascus, forty camels' burden, and came and stood before him, and said, Your son Benhadad king of Syria has sent me to you, saying, Shall I recover of this sickness?

Elisha akamwambia, Enenda, ukamwambie, Bila shaka utapona; lakini Bwana amenionyesha ya kwamba bila shaka atakufa. 2 Wafalme 8:10

Elisha said to him, Go, tell him, You shall surely recover; however Yahweh has shown me that he shall surely die.

Akamkazia macho hata akatahayari; na yule mtu wa Mungu akalia machozi. 2 Wafalme 8:11

He settled his gaze steadfastly [on him], until he was ashamed: and the man of God wept.

Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawaseta-seta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua. 2 Wafalme 8:12

Hazael said, Why weeps my lord? He answered, Because I know the evil that you will do to the children of Israel: their strongholds will you set on fire, and their young men will you kill with the sword, and will dash in pieces their little ones, and rip up their women with child.

Hazaeli akasema, Lakini mimi mtumwa wako ni nani, mimi niliye mbwa tu, hata nifanye jambo hili kubwa? Elisha akajibu, Bwana amenionyesha ya kwamba wewe utakuwa mfalme juu ya Shamu. 2 Wafalme 8:13

Hazael said, But what is your servant, who is but a dog, that he should do this great thing? Elisha answered, Yahweh has shown me that you shall be king over Syria.

Ndipo akamwacha Elisha, akarudi kwa bwana wake; naye akamwambia, Elisha alikuambiaje? Akajibu, Aliniambia ya kuwa bila shaka utapona. 2 Wafalme 8:14

Then he departed from Elisha, and came to his master; who said to him, What said Elisha to you? He answered, He told me that you would surely recover.

Ikawa siku ya pili yake, akatwaa tandiko la kitanda, akalichovya katika maji, akalitandaza juu ya uso wake, hata akafa. Na Hazaeli akatawala badala yake. 2 Wafalme 8:15

It happened on the next day, that he took the coverlet, and dipped it in water, and spread it on his face, so that he died: and Hazael reigned in his place.

Katika mwaka wa tano wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, [Yehoshafati alipokuwa mfalme wa Yuda], alianza kutawala Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. 2 Wafalme 8:16

In the fifth year of Joram the son of Ahab king of Israel, Jehoshaphat being then king of Judah, Jehoram the son of Jehoshaphat king of Judah began to reign.

Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala miaka minane huko Yerusalemu. 2 Wafalme 8:17

Thirty-two years old was he when he began to reign; and he reigned eight years in Jerusalem.

Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa amemwoa binti Ahabu; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana. 2 Wafalme 8:18

He walked in the way of the kings of Israel, as did the house of Ahab: for he had the daughter of Ahab as wife; and he did that which was evil in the sight of Yahweh.

Walakini Bwana hakupenda kuiharibu Yuda, kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, kama alivyomwahidia akasema, kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote. 2 Wafalme 8:19

However Yahweh would not destroy Judah, for David his servant's sake, as he promised him to give to him a lamp for his children always.

Zamani zake, Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda, wakajifanyia mfalme. 2 Wafalme 8:20

In his days Edom revolted from under the hand of Judah, and made a king over themselves.

Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na maakida wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao. 2 Wafalme 8:21

Then Joram passed over to Zair, and all his chariots with him: and he rose up by night, and struck the Edomites who surrounded him, and the captains of the chariots; and the people fled to their tents.

Hivyo Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda hata leo. Na Libna wakaasi zamani zizo hizo. 2 Wafalme 8:22

So Edom revolted from under the hand of Judah to this day. Then did Libnah revolt at the same time.

Na mambo yote ya Yehoramu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 8:23

The rest of the acts of Joram, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Akalala Yehoramu na baba zake, akazikwa pamoja na baba zake mjini mwa Daudi; na Ahazia mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 8:24

Joram slept with his fathers, and was buried with his fathers in the city of David; and Ahaziah his son reigned in his place.

Katika mwaka wa kumi na mbili wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2 Wafalme 8:25

In the twelfth year of Joram the son of Ahab king of Israel did Ahaziah the son of Jehoram king of Judah begin to reign.

Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli. 2 Wafalme 8:26

Twenty-two years old was Ahaziah when he began to reign; and he reigned one year in Jerusalem. His mother's name was Athaliah the daughter of Omri king of Israel.

Akaiendea njia ya nyumba ya Ahabu, akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa alikuwa mkwe wa jamaa ya Ahabu. 2 Wafalme 8:27

He walked in the way of the house of Ahab, and did that which was evil in the sight of Yahweh, as did the house of Ahab; for he was the son-in-law of the house of Ahab.

Akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu ili kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu, huko Ramoth-gileadi; nao Washami wakamtia Yoramu jeraha. 2 Wafalme 8:28

He went with Joram the son of Ahab to war against Hazael king of Syria at Ramoth-gilead: and the Syrians wounded Joram.

Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli jeraha walizotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa hawezi. 2 Wafalme 8:29

King Joram returned to be healed in Jezreel of the wounds which the Syrians had given him at Ramah, when he fought against Hazael king of Syria. Ahaziah the son of Jehoram king of Judah went down to see Joram the son of Ahab in Jezreel, because he was sick.