2 Wafalme 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 17 (Swahili) 2nd Kings 17 (English)

Katika mwaka wa kumi na mbili wa Ahazi mfalme wa Yuda Hoshea mwana wa Ela alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka kenda. 2 Wafalme 17:1

In the twelfth year of Ahaz king of Judah began Hoshea the son of Elah to reign in Samaria over Israel, [and reigned] nine years.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, ila si kama wafalme wa Israeli waliomtangulia. 2 Wafalme 17:2

He did that which was evil in the sight of Yahweh, yet not as the kings of Israel who were before him.

Naye Shalmanesa mfalme wa Ashuru akakwea juu yake, Hoshea akawa mtumishi wake, akampa kodi. 2 Wafalme 17:3

Against him came up Shalmaneser king of Assyria; and Hoshea became his servant, and brought him tribute.

Mfalme wa Ashuru akaona fitina katika huyo Hoshea; kwa maana alikuwa ametuma wajumbe kwa So, mfalme wa Misri, wala hakumletea kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka kwa mwaka; kwa hiyo mfalme wa Ashuru akamfunga, akamtia kifungoni. 2 Wafalme 17:4

The king of Assyria found conspiracy in Hoshea; for he had sent messengers to So king of Egypt, and offered no tribute to the king of Assyria, as he had done year by year: therefore the king of Assyria shut him up, and bound him in prison.

Ndipo mfalme wa Ashuru akakwea katikati ya nchi yote, akaenda Samaria, akauhusuru miaka mitatu. 2 Wafalme 17:5

Then the king of Assyria came up throughout all the land, and went up to Samaria, and besieged it three years.

Katika mwaka wa kenda wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi. 2 Wafalme 17:6

In the ninth year of Hoshea the king of Assyria took Samaria, and carried Israel away to Assyria, and placed them in Halah, and on the Habor, the river of Gozan, and in the cities of the Medes.

Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya Bwana, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakawaacha miungu mingine. 2 Wafalme 17:7

It was so, because the children of Israel had sinned against Yahweh their God, who brought them up out of the land of Egypt from under the hand of Pharaoh king of Egypt, and had feared other gods,

Wakaziendea sheria za mataifa, ambao Bwana aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli, na sheria za wafalme wa Israeli walizozifanya. 2 Wafalme 17:8

and walked in the statutes of the nations, whom Yahweh cast out from before the children of Israel, and of the kings of Israel, which they made.

Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma. 2 Wafalme 17:9

The children of Israel did secretly things that were not right against Yahweh their God: and they built them high places in all their cities, from the tower of the watchmen to the fortified city;

Wakajisimamishia nguzo na maashera juu ya kila mlima mrefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 2 Wafalme 17:10

and they set them up pillars and Asherim on every high hill, and under every green tree;

wakafukiza uvumba huko katika kila mahali pa juu, kama mataifa walivyofanya, ambao Bwana aliwafukuza mbele yao; wakaunda mambo mabaya, ili wamkasirishe Bwana; 2 Wafalme 17:11

and there they burnt incense in all the high places, as did the nations whom Yahweh carried away before them; and they worked wicked things to provoke Yahweh to anger;

wakatumikia sanamu, ambazo Bwana aliwakataza, akasema, Msitende jambo hili. 2 Wafalme 17:12

and they served idols, of which Yahweh had said to them, You shall not do this thing.

Pamoja na hayo Bwana aliwashuhudia Israeli, na Yuda, kwa kinywa cha kila nabii, na cha kila mwonaji, akisema, Geukeni, na kuziacha njia zenu mbaya, mkazishike amri zangu na hukumu zangu, sawasawa na ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, nikawapelekea kwa kinywa cha manabii watumishi wangu. 2 Wafalme 17:13

Yet Yahweh testified to Israel, and to Judah, by every prophet, and every seer, saying, Turn you from your evil ways, and keep my commandments and my statutes, according to all the law which I commanded your fathers, and which I sent to you by my servants the prophets.

Walakini hawakutaka kusikia, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, kama shingo za baba zao, wasiomwamini Bwana, Mungu wao. 2 Wafalme 17:14

Notwithstanding, they would not hear, but hardened their neck, like the neck of their fathers, who didn't believe in Yahweh their God.

Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao Bwana alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao. 2 Wafalme 17:15

They rejected his statutes, and his covenant that he made with their fathers, and his testimonies which he testified to them; and they followed vanity, and became vain, and [went] after the nations that were round about them, concerning whom Yahweh had charged those who they should not do like them.

Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali. 2 Wafalme 17:16

They forsook all the commandments of Yahweh their God, and made them molten images, even two calves, and made an Asherah, and worshiped all the host of the sky, and served Baal.

Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 2 Wafalme 17:17

They caused their sons and their daughters to pass through the fire, and used divination and enchantments, and sold themselves to do that which was evil in the sight of Yahweh, to provoke him to anger.

Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake. 2 Wafalme 17:18

Therefore Yahweh was very angry with Israel, and removed them out of his sight: there was none left but the tribe of Judah only.

Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya Bwana, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe. 2 Wafalme 17:19

Also Judah didn't keep the commandments of Yahweh their God, but walked in the statutes of Israel which they made.

Basi Bwana akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake. 2 Wafalme 17:20

Yahweh rejected all the seed of Israel, and afflicted them, and delivered them into the hand of spoilers, until he had cast them out of his sight.

Maana aliwatenga mbali Israeli na nyumba ya Daudi; nao wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nebati kuwa mfalme; Yeroboamu akawavuta Israeli wasimfuate Bwana, akawakosesha kosa kubwa. 2 Wafalme 17:21

For he tore Israel from the house of David; and they made Jeroboam the son of Nebat king: and Jeroboam drove Israel from following Yahweh, and made them sin a great sin.

Nao wana wa Israeli wakaendelea katika dhambi zote za Yeroboamu alizozifanya; hawakujiepusha nazo; 2 Wafalme 17:22

The children of Israel walked in all the sins of Jeroboam which he did; they didn't depart from them;

hata Bwana akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo. 2 Wafalme 17:23

until Yahweh removed Israel out of his sight, as he spoke by all his servants the prophets. So Israel was carried away out of their own land to Assyria to this day.

Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. 2 Wafalme 17:24

The king of Assyria brought men from Babylon, and from Cuthah, and from Avva, and from Hamath and Sepharvaim, and placed them in the cities of Samaria instead of the children of Israel; and they possessed Samaria, and lived in the cities of it.

Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha Bwana; kwa hiyo Bwana akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. 2 Wafalme 17:25

So it was, at the beginning of their dwelling there, that they didn't fear Yahweh: therefore Yahweh sent lions among them, which killed some of them.

Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. 2 Wafalme 17:26

Therefore they spoke to the king of Assyria, saying, The nations which you have carried away, and placed in the cities of Samaria, don't know the law of the god of the land: therefore he has sent lions among them, and, behold, they kill them, because they don't know the law of the god of the land.

Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. 2 Wafalme 17:27

Then the king of Assyria commanded, saying, Carry there one of the priests whom you brought from there; and let them go and dwell there, and let him teach them the law of the god of the land.

Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha Bwana. 2 Wafalme 17:28

So one of the priests whom they had carried away from Samaria came and lived in Bethel, and taught them how they should fear Yahweh.

Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa. 2 Wafalme 17:29

However every nation made gods of their own, and put them in the houses of the high places which the Samaritans had made, every nation in their cities in which they lived.

Watu wa Babeli wakafanya Sukoth-benothi kuwa mungu wao, watu wa Kutha wakafanya Nergali, watu wa Hamathi wakafanya Ashima, 2 Wafalme 17:30

The men of Babylon made Succoth-benoth, and the men of Cuth made Nergal, and the men of Hamath made Ashima,

Waavi wakafanya Nibhazi na Tartaki; nao Wasefarvi wakawaunguza wana wao katika moto kwa Adrameleki na Anameleki, miungu ya Sefarvaimu. 2 Wafalme 17:31

and the Avvites made Nibhaz and Tartak; and the Sepharvites burnt their children in the fire to Adrammelech and Anammelech, the gods of Sepharvaim.

Basi hivyo wakamcha Bwana, nao wakijifanyia wengine wao kuwa makuhani wa mahali pa juu, ambao waliwafanyia dhabihu katika nyumba za mahali pa juu. 2 Wafalme 17:32

So they feared Yahweh, and made to them from among themselves priests of the high places, who sacrificed for them in the houses of the high places.

Wakamcha Bwana, na kuitumikia miungu yao wenyewe, sawasawa na kawaida za mataifa ambao wao walihamishwa kutoka kwao. 2 Wafalme 17:33

They feared Yahweh, and served their own gods, after the manner of the nations from among whom they had been carried away.

Hata siku hii ya leo hufanya sawasawa na kawaida za kwanza; wala hawamwogopi Bwana, wala hawazifuati sheria zao, wala hukumu zao, wala ile torati, wala ile amri Bwana aliyowaamuru wana wa Yakobo, ambaye alimpa jina la Israeli; 2 Wafalme 17:34

To this day they do after the former manner: they don't fear Yahweh, neither do they after their statutes, or after their ordinances, or after the law or after the commandment which Yahweh commanded the children of Jacob, whom he named Israel;

hao ambao Bwana alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka; 2 Wafalme 17:35

with whom Yahweh had made a covenant, and charged them, saying, You shall not fear other gods, nor bow yourselves to them, nor serve them, nor sacrifice to them:

ila yeye Bwana, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri kwa nguvu nyingi, na kwa mkono ulionyoshwa, yeye ndiye mtakayemcha, yeye ndiye mtakayemsujudia, yeye ndiye mtakayemtolea sadaka; 2 Wafalme 17:36

but Yahweh, who brought you up out of the land of Egypt with great power and with an outstretched arm, him shall you fear, and to him shall you bow yourselves, and to him shall you sacrifice:

na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine. 2 Wafalme 17:37

and the statutes and the ordinances, and the law and the commandment, which he wrote for you, you shall observe to do forevermore; and you shall not fear other gods:

Na hilo agano nililofanya nanyi, msilisahau; wala msiche miungu mingine; 2 Wafalme 17:38

and the covenant that I have made with you you shall not forget; neither shall you fear other gods:

lakini Bwana, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote. 2 Wafalme 17:39

but Yahweh your God shall you fear; and he will deliver you out of the hand of all your enemies.

Walakini hawakusikia, bali wakafanya sawasawa na kawaida zao za kwanza. 2 Wafalme 17:40

However they did not listen, but they did after their former manner.

Basi mataifa hawa wakamcha Bwana, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.

2 Wafalme 17:41

So these nations feared Yahweh, and served their engraved images; their children likewise, and their children's children, as did their fathers, so do they to this day.