Mithali 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mithali 27 (Swahili) Proverbs 27 (English)

Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mithali 27:1

Don't boast about tomorrow; For you don't know what a day may bring forth.

Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe. Mithali 27:2

Let another man praise you, And not your own mouth; A stranger, and not your own lips.

Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili. Mithali 27:3

A stone is heavy, And sand is a burden; But a fool's provocation is heavier than both.

Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu. Mithali 27:4

Wrath is cruel, And anger is overwhelming; But who is able to stand before jealousy?

Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika. Mithali 27:5

Better is open rebuke Than hidden love.

Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. Mithali 27:6

Faithful are the wounds of a friend; Although the kisses of an enemy are profuse.

Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu. Mithali 27:7

A full soul loathes a honeycomb; But to a hungry soul, every bitter thing is sweet.

Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake. Mithali 27:8

As a bird that wanders from her nest, So is a man who wanders from his home.

Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake. Mithali 27:9

Perfume and incense bring joy to the heart; So does earnest counsel from a man's friend.

Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Mithali 27:10

Don't forsake your friend and your father's friend. Don't go to your brother's house in the day of your disaster: Better is a neighbor who is near than a distant brother.

Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu; Ili nipate kumjibu anilaumuye. Mithali 27:11

Be wise, my son, And bring joy to my heart, Then I can answer my tormentor.

Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Mithali 27:12

A prudent man sees danger and takes refuge; But the simple pass on, and suffer for it:

Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya. Mithali 27:13

Take his garment when he puts up collateral for a stranger; Hold it for a wayward woman!

Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake. Mithali 27:14

He who blesses his neighbor with a loud voice early in the morning, It will be taken as a curse by him.

Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa; Mithali 27:15

A continual dropping on a rainy day And a contentious wife are alike:

Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta. Mithali 27:16

Restraining her is like restraining the wind, Or like grasping oil in his right hand.

Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. Mithali 27:17

Iron sharpens iron; So a man sharpens his friend's countenance.

Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa. Mithali 27:18

Whoever tends the fig tree shall eat its fruit. He who looks after his master shall be honored.

Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake. Mithali 27:19

As water reflects a face, So a man's heart reflects the man.

Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. Mithali 27:20

Sheol and Abaddon are never satisfied; And a man's eyes are never satisfied.

Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake. Mithali 27:21

The crucible is for silver, And the furnace for gold; But man is refined by his praise.

Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka. Mithali 27:22

Though you grind a fool in a mortar with a pestle along with grain, Yet his foolishness will not be removed from him.

Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng'ombe zako. Mithali 27:23

Know well the state of your flocks, And pay attention to your herds:

Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi? Mithali 27:24

For riches are not forever, Nor does even the crown endure to all generations.

Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, Na maboga ya milimani hukusanyika. Mithali 27:25

The hay is removed, and the new growth appears, The grasses of the hills are gathered in.

Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba Mithali 27:26

The lambs are for your clothing, And the goats are the price of a field.

Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako. Mithali 27:27

There will be plenty of goats' milk for your food, For your family's food, And for the nourishment of your servant girls.